Uvutaji wa sigara na mazingira yaliyokuwa na moshi wa sigara ( second hand smoke) hujulikana kwa maafa yake ya husababisha magonjwa sugu ya mapafu yajulikanayo kama ‘Chronic Obstructive Pulmonary Diseases” (COPD) yakiwemo pumu, kifua kikuu na …?(emphysema). Magonjwa haya uhashiriwa na upungufu wa umahiri wa ubadilishaji wa hewa katika mapafu; ugumu wa kutoa hewa chafu ya carbon katika mapafu na uchukuaji wa hewa oxygen. Hii hujitokeza pale mgonjwa anapojihisi ugumu wa kuvuta hewa hasa wakati wa shughuli au mazoezi.
Mbali na magojwa sugu ya mapafu,uvutaji wa sigara watupelekea saratani za aina mabalimbali kama :-
- Saratani ya mapafu
- Saratani ya njia ya chakula (umio au esophagus)
- Utumbo,
- Njia ya kutolea uchafu mwilini,
- Ini,figo na njia ya mkojo
- Kigosho, tumbo na koromeo.
Uvutaji wa sigara waweza kupunguza uwezo wa uzazi kwa mwanamke kuharibu afya ya mtoto kabla ya kuzaliwa pamoja na ;
- Kuzaliwa kwa mtoto ambaye hajatimia siku za kuzaliwa(premature)
- Kufariki kwa mtoto kabla ya kuzaliwa (stillbirth)
- Mtoto mwenye uzito mdogo au chini ya kipimo wakati wa kuzaliwa
- Kifo cha ghafla kwa mtoto mchanga ( sudden infant death syndrome; SIDS)
- Mimba iliyojipachika nje ya kizazi (Ectopic pregnancy)
- Mtoto mwenye hitilafu sehemu za midomo
ZITAKAPO MDOMO (CLEF LIP ) |
UZITO PUNGUFU WAKATI WA KUZALIWA ( Low birthweight <5.5 pounds) |
Uvutaji sigara huchangia kuharibu mbegu za kiume na kupunguza nguvu ya uzazi pamoja na kupelekea hitilafu za kuzaliwa na upoteaji wa mimba changa.Wanawake wanaovuta sigara waliopita umri wa uzazi wana ongezeko la uhafifu wa mifupa hivyo huvunjika kwa urahisi pamoja na afya duni ya meno na fizi.Uvutaji wa sigara wasemekana kwa kupelekea hatari zaidi ya kupata stoke na magonjwa ya moyo mara 2 hadi 4 na upofukaji wa macho ukilinganisha na mtu asiye mvutaji wa sigara pamoja na Burgeres disease ‘ugojwa ambao unaathiri mishipa ya damu ya mikono na miguu.
BURGERS DISEASE |
Shukrani: Thanks
http://ahealthylifefitness.blogspot.com/
DR M.A. ANSARY/SCIENCE PHOTO LIBRARY
http://www.cdc.gov/tobacco/campaign
funmasti1.blogspot.com
www.kaskus.co.id - 34Burgers Disease
article.wn.com
aboutbabyarticle.blogspot.com
http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/2644816
Comments
Post a Comment