Skip to main content

Posts

Showing posts from October, 2014

JENGA TANZANIA FOUNDATION YAKULETEA KIPIMO CHA MALARIA PAPO HAPO !

Mwanadiaspora Mtanzania na Mkurugenzi wa  JENGA TANZANIA FOUNDATION   Bw. Nasoro Ally akitambulisha rasmi Home Malaria Kit katika mkutano wa  Africa Diaspora Market Place (ADMP III) uliofanyika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani tarehe 10/27/2014. Akizungumza katika mkutano huo, Bw.. Nasoro Ally alieleza  kuwa  bado Malaria ni tishio kubwa la uhai kwa Sub-Sahara Africa na ni chanzo cha vifo vya watoto wadogo hasa chini ya umri wa miaka 5 .  Kipimo hicho chenye uwezo wa kugundua vijidudu vya Malaria mwilini kati ya dakika 5 hadi 10 kimekubalika na shirika la World Health Organization (WHO) kama kipimo sahihi na cha haraka kwa upimaji wa Malaria nyumbani.  Bw. Nassoro aliongeza kusema, kipimo hicho kitatolewa bure nchini Tanzania kwa familia zisizojiweza na kuhakikisha kinafika  sehemu mbali mbali za ndani hasa mikoani na vijijini ili kurahisisha upatikanaji wa huduma sahihi za afya na kufupisha safari ndefu na zenye milolongo. Mkurugenzi wa JENGA TANZANIA foundati

TAHARUKI YA UGOJWA WA EBOLA KUFIKA MJINI MOSHI, MKOANI KILIMANJARO

         KILIMANJARO  wakazii wa kata ya Shirimatunda, katika manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, wamejikuta katika hali ya taharuki kufuatia taarifa za kuwepo kwa mgonjwa anayedhaniwa kuwa anaugua ugonjwa hatari  wa Ebola, ambaye amelazwa katika zahanati ya shirimatunda iliyopo kwenye kata hiyo. Mgonjwa huyo aliyefikishwa katika Zahanati hiyo Juzi majira ya Jioni, ambapo hali hiyo ilisababisha huduma za afya katika zahanati hiyo kusitishwa kwa muda usiojulikana, ambapo wagonjwa waliokuwa wakipatiwa matibabu kutoka ndani na nje ya kata hiyo kuondolewa na watoto waliokuwa wakipata chanzo katika zahanati hiyo walihamishiwa katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata hiyo.   Taarifa za awali zinadai kuwa, mgonjwa ni Raia wa Tanzania mzaliwa wa Marangu wilayani Moshi, mwenye makazi yake jijini Dar es Salaam, alipokelewa katika uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro (KIA), akitokea nchini Senegal kikazi, ambapo alisafirishwa hadi kwenye zahanati hiyo baada ya kudai ku

PATA CHANJO YA FLUE BURE NA HUDUMA NYINGENE ZA AFYA KWA BEI NAFUU

KAMATI YA AFYA DMV INAWATANGAZIA HUDUMA MUHIMU  YA AFYA

WATAFITI WA DAWA YA EBOLA, A.MANGHARIBI

Kampeni ya Ebola Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema dawa ya Ebola ambayo imetengenezwa kwa mchanganyiko na damu ya watu waliambukizwa na kisha kupona ugonjwa wa Ebola inatarajiwa kuanza kupatikana wiki chache zijazo huko Afrika Magharibi. Afisa mwandamizi wa W.H.O. Dr Marie Paule Kieny amesema vifaa vimetolewa Liberia kwaajili ya kupata damu na vifaa vya kufanyia utafiti huo wa dawa ili kupata dawa Serum. Dr Kieny akizungumza mjini Geneva amesema kuwa kazi ya mapambano dhidi ya Ebola harakati za upatikanaji chanjo ya ugonjwa huo . Maelfu ya watu wanatarajiwa kutumiwa katika majaribio hayo yanayolenga kupatikana kwa chanjo na dawa ya ugonjwa huo. Shukrani,  Swahili,BBC

KESI YA PILI YA EBOLA MAREKANI !

Mfanyakazi mmoja wa hospitali ya Presbyterian huko Texas hapa Marekani ametangazwa kuwa na ugonjwa hatari wa Ebola. Mfanyakai huyo anaaminika amepata ugonjwa huo baada ya kumhudumia hayati Thomas Eric Duncan aliyekuwa mgonjwa wa kwanza hapa Marekani aliyeambukizwa nchini kwao Liberia. Taasisi ya magonjwa ya kuambukiza Marekani CDC imethibitisha habari  hizo.Hili  ndio ambukizo la kwanza la ugonjwa huu hapa Marekani. This entry was posted on October 12, 2014, in  Karibu . Shukrani; http://sundayshomari.com/

AFRICAN WOMAN CANCER ASSOCIATION (AWCAA) INAWAKARIBISHA KATIKA GALA YA KUADHIMISHA MIAKA KUMI TOKA KUANZISHWA KWA SHIRIKA HILO

AWCAA ni shirika lililoko mstari wa mbele kwa kutoa HUDUMA na ELIMU ya SARATANI YA MATITI kwa jamii ya wahamiaji ugenini na hata nyumbani . Nyote Mnakaribishwa KWA TICKET PIGA SIMU 703-624-2409

USA, MGOJWA WA KWANZA WA EBOLA AFARIKI.

USA:MGOJWA WA KWANZA AFARIKI Thomas Eric Duncan afariki Mtu wa kwanza kupatikana na ugonjwa wa Ebola nchini Marekani amefariki ,hayo ni kwa mujibu wa maafisa wa afya katika hospitali ya Texas. Thomas Eric Duncan aliyeambukizwa ugonjwa wa Ebola huko nchini Liberia ,alikuwa amewekwa katika karantini katika hospitali moja ya mjini Dallas ili kupewa dawa za majaribio. Awali ,Marekani ilitangaza masharti mapya ya usalama katika viingilio vyote vya taifa hilo ili kuwakagua wasafiri walio na dalili za ugonjwa huo. Zaidi ya watu 3000 wamefariki na wengine 7500 kuambukizwa wengi wao kutoka Afrika Magharibi katika mlipuko mbaya wa ugonjwa wa Ebola. Huku Dancun akiwa raia wa kwanza nchini Marekani kupatikana na ugonjwa huo,raia watatu wa Marekani pamoja na mpiga picha mmoja waliambukizwa virusi vya ugonjwa huo nchini Liberia. Habari hizo zilijiri mda mchache tu baada ya waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry kutoa wito kwa mataifa yote kuimarisha juhudi zao za kukabi

FAHAMU KUHUSU EBOLA.

18/08/2014 Fahamu kuhusu Ebola! Muuguzi akimfariji mgonjwa aliyethibitika kuwa na kirusi cha Ebola.(Picha: WHO/Chris Black) 1.Ugonjwa wa Ebola ni nini? Ugonjwa utokanao na kirusi cha Ebola ni ugonjwa hatari wenye uwezo wa kusababisha kifo kwa asilimia 90.  Shirika la afya duniani, WHO katika tovuti yake inasema kwa mara ya kwanza ulibainika mwaka 1976 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Sudan. Chanzo cha kirusi hiki hadi sasa hakijulikani lakini popo aina ya (Pteropodidae) wanaonekana kuwa wabebaji wa kirusi hicho,kwa mujibu wa ushahidi uliopo sasa. 2. Binadamu anaambukizwa vipi kirusi cha Ebola? Mlipuko wa sasa huko Afrika Magharibi kwa kiasi kikubwa umesababishwa na maambukizi ya binadamu kwa binadamu.  Maambukizi hutokea pindi mtu anapoambukizwa kupitia  sehemu wazi ya mwili wake majimaji ya mgonjwa wa Ebola.  Mathalani matapishi, choo,  mate,  mbegu za kiume, au Semen   damu.   Maambukizi yanaweza kutokea pia iwapo ngozi yenye uwazi ya

CHUKUWA TAHADHARI KWA KUPATA CHANJO YA MAFUA MAKALI!

KAMATI YA AFYA  DMV INATUKUMBUSHIA KUCHUKUWA  TAHADHARI KWA MAFUA MAKALI KWA KUPATA CHANJO YA MAFUA  SASA Mafua/influenza (Flu) ni ugojwa wa kuambukiza (contagious disease) ambao husambaa hapa marekani wakati wa masika kati ya mwezi wa 5 na mwezi wa 10 .Mafua haya husababishwa na virusi vilivyo katikavya kundi la Influenza 1. Influenza A (H1N1), 2. Influenza A (H3N2) 3. Influenza B. Maambukizi ya    Ifluenza A & B hupatikana pale unapokuwa karibu na mtu mwenye flu kupitia kukohoa, chafya au kugusana kwa karibu.Yashauriwa kuosha mikono mara kwa mara ili kupunguza maambukizi .Chanjo ya mafua (Flue shot) ni  mchanganyiko wa aina tatu za chanjo(Trivalent vaccine) ambazo hukinga watu dhidi ya virusi vya influenza . DALILI ZA FLU Homa ≥ 100F Mafua,chafya,kukwaruza kwa koo Maumivu ya kichwa,mwili,viungo Uchovu wa mwili Kichefuchefu,kutapika hata kuharisha FAIDA YA CHANJO a) Kukinga mwili na ugonjwa wa mafua makali / influenza (“Flu”) b)

TANO LADIES NA AWCAA WAKABIDHI MAMMOGRAM MASHINE KWA MHE.MAMA SALMA KIKWETE ITAKAYOSAIDIA UCHUNGUZI WA SARATANI YA MAZIWA NCHINI TANZANIA.

Mhe.mama Salma Kikwete Akutana na wanaharakati Kinadada wa TANO LADIES ambao wamekuwa daraja kubwa la usakaji na upatikanaji wa machine ya Mammogram itakayosaidia maelfu ya kina mama nchini Tanzania. Mhe Mama Salma akipokea machine ya Mammogram kutoka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya African Women Cancer Aweareness Association. TANO LADIES na Wawakilishi wa AWCAA katika picha ya pamoja TANO LADIES na timu TEAM TANZANIA ya kupambana na Saratani ya maziwa nchini US Washington Dc. Mwanzilishi wa Blog ya NesiWangu akiwaunga mkono Kinadada wa TANO LADIES katika jitihada zao za kuboresha upatikanaji wa huduma muhimu za afya nchini Tanzania.       Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa TANO LADIES Madam Asha Harriz             Mama Salma Kikwete akiwa na Vice-chair wa TANO LADIES Madam Asha Nyanganyi Mama Salma Kikwete na Public Relation & Coordinating Officer wa TANO LADIES Madam Tumaini Kaisi Katule.             Mama Salma Kikwete akiwa na  Tressur