Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2016

Je Watambua Dawa Ijulikanayo kwa Jina la PrEP au Truvada?.

Shirika la utawala wa vyakula na madawa nchini Marekani lijulikanalo kama FDA, lilihakiki dawa ijulikanayo kama Prep ( Pre - Exposure Prophylaxis) yenye uwezo wa kupunguza hatari za maambukizi ya ugojwa wa Ukimwi. Shirika hilo limeitambua dawa hii na kuruhusu matumizi yake ili kupunguza maambukizi ya ugojwa wa ukimwi kwa watu walio katika mazingira ya hatari na maambukizi mfano; mahusiano ya watu wawili ikiwa mmoja yupo  Positive na mwenzie yupo Negative, watu wenye kutumia au kujidunga dawa za kulevya, na wale walio katika mahusiano ya jinsia moja.                                                       Dawa hii yenye muonekano wa kidonge hushauriwa kutumika mara moja kwa siku bila kukosa dozi kwani kusahau dozi hupunguza kiwango cha dawa katika mzunguko wa damu na kudhoofisha kinga dhidi ya virusi vya ukimwi. Habari hii imezua gumzo na maswali katika jamii..k wa maelezo zaidi pitia mitandao ifuatayo:  http://www.whatisprep.org/ AIDS.gov  - PrEP information page  (aids.gov/