Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2015

Help for Underserved Communites (HUC) Waomba mchango wako

Bofya hapa   https://www.gofundme.com/duar96hs "Give a Gift of Education" Please help us in the quest to Empower Rural and Underserved Communities in Tanzania. This year we got a special request from Steven Kibona Secondary School and Kalembo Primary School Located in Ileje District, Mbeya Region in Tanzania (East Africa). These schools need Textbooks to ensure their students are able to get the education they deserve. We are working hard to make this request a success, but we cannot do it without your help. Anything you can give will be so helpful, more than you can imagine. HUC is a 501(c)(3) non-profit organization, your contribution will be tax deductable to extend allowed by USA Law.  Nelson Mandela said " Education Is The Most Powerful Weapon Which You Can Use To Change The World".  From HUC Board Members we thank you! "Everyone Deserves a Better Life"  http://myhuc.org/

PATA ELIMU NA UCHUNGUZI WA AFYA YA TEZI DUME

KUPATA HUDUMA HII ENEO LA DMV KWA ASIYE NA BIMA YA AFYA CALL 240 672 1788 Tezi Dume, ni tezi yenye  umbile la donati iliyoko chini ya kibofu cha mkojo.Tezi hii huzungukwa na  mirija  ya mkojo na uhusika na urutubishaji wa mbegu za kiume (semen). Mabadiliko ya kimaumbile katika tezi ya prostate kama uvimbe,ongezeko la ukubwa au kushamiri kwa saratani, hupelekea hitilafu katika mfumo wa mkojo kwa kufinya mrija wa mkojo na hivyo mkojo kupita kwa shida,hukwama au kuacha mabaki.Hali hii humpelekea mgojwa uhitaji wa kutumia bafu mara kwa mara na hata kushindwa kuzia mkojo kuchuruzika. (Maumbile yote mwilini, yamekadiriwa kulingana na nafasi iliyoko, hivyo umbile linapoongezeka ukubwa, huleta hitilafu kwa mfumo mwingine). Saratani ya Prostate yaweza sambaa katika mifupa na tishu za jirani na hata kubana mishipa ya mgongo na kuleta maumivu sehemu za mgongo,hip na pelvic.  Yashauriwa kufanya uchunguzi wa afya ya tezi dume kuanzia “ miaka 45 kwa wale walio na historia ya saratani ya te

KONGAMANO LA UFUMBUZI WA TIBA YA SARATANI BARANI AFRICA

 Kongamano hilo linaloendelea sasa  nchini Morocco, limehuidhuriwa na wanasayansi wenye asili ya nchi mbalilmbali za ki-Africa ili kujadili mikakati itayowezesha kupambana na gojwa la saratani ambalo ni  tishio kubwa kwa jamii hasa katika nchi zinazoendelea.                             Mazungumzo hayo yaligusia uhaba wa mashine za mionzi barani Africa na elimu endelevu kwa wahudumu wa saratani,jambo ambalo litawezekana kwa njia ya technolojia ya mawasilino na   wanayasansi waliomo nje ya nchi. Nia ni kuboresha tiba na ufumbuzi wa changamoto za ugojwa wa saratani.   Majadiliano zaidi yalisisitizia umuhimu wa elimu ya utumiaji na utunzaji wa vifaa vya  mionzi , upatikanaji wa vifaa katika vituo vya tiba ya saratani na mikakati ya kuelimisha jamii katika kufuata ushauri wa daktari ili kuepusha saratani za aina mbali mbali kama saratani ya shingo ya kizazi kwa kutoa chanjo kwa watoto wa kike kuanzia umri wa miaka 11 au 12,  uvutaji wa sigara unaoongeza hatari za kupata sara

SALAMU ZA RAMBIRAMBI

Kwa majonzi makubwa,tumepokea taarifa  za msiba wa dada yetu mpenzi, rafiki yetu,mhudumu wa taifa letu na aliyekuwa mgeni wetu wa kwanza kujitolea kupima Malaria na kuzungumzia huduma za afya katika kipindi cha NesiWangu na JENGA Tanzania,Malaria-Kit. Salamu za rambirambi TUNAOMBA ziwafikie ndugu, jamaa, marafiki na wote tulioguswa na maisha ya mdogo wetu mpenzi, dada Nyamiti Ivan Lusinde MWENYEZI MUNGU AKUPOKEE NA KUKUWEKA PEMA PEPONI DADA YETU NYAMI LUSINDE

Mh. Rais Magufuli Katika Uwanja wa Huduma za Afya

        ASANTE SAANA BABA! Shukrani Images  www.ippmedia.com Video/Source Unknown

CHILD SERVIVAL INTERNATIONAL (CSI)

Yaomba mchango wako wa Socks na Kofia kwa watoto wachanga! Kwa Maelezo Zaidi  piga simu; 240 672 1788 Shukrani;Image CSI

CATCH UP WITH THE LATEST CAREERS IN THE IT WORLD !

  Montgomery College's Leap Tech Program great pathway to the latest careers in the IT world .   take advantage of the opportunity particularly because scholarships are involved.  Visit;  http://www2.montgomerycollege. edu/departments/iti/techleap/ index.html  I nformation session scheduled for 11/23 from 10 am to 12 pm where questions will be answered. Please invite friends whom you think will be a perfect fit as the program is selective with individuals with a bachelors degree or IT background. Confirmation to attend is highly recommended FOR MORE INFO                                                                                      Call 240 672 1788,    240-688-7559 or  301-213-1972 anita.mwalui@ montgomerycollege.edu   or jean-yves.dalle@ montgomerycollege.edu or

ISAIAH WASHINGTON ATUA DMV KUSHEHEREKEA SEIRRA LEONE FREE OF EBOLA!

Mwigizaji maarufu wa Television Series, Grays Anatomy 'Isaiah Washington' alishiriki  katika misa ya kutoa shukrani na kusheherekea rasmi tamko lililotolewa na  Shirika la Afya Duniani WHO, tarehe 7/11/2015  'Sierra Leone, Ebola- Free' .Misa hiyo iliyofanyikia katika Kanisa la  City of Light, Randolph Rd. Silver Spring, MD  na  ilijumuisha  Balozi wa Sierra Leone nchini Marekani,  H.E Bockari Stevens, Wajane walipoteza waume zao  miongoni wakiwa madaktari walioenda katika mapambano ya Ebola. Mayatima,Ndugu na Marafiki. Waumini wengi walishiriki wakiwemo  Wanadiaspora waliojitoa katika usafirishaji wa vyombo vya hospitali,ambulances,vyakula,fedha, pamoja na timu kuu ya wanadiaspora iliyohusika na mapambano dhidi  ya Ebola  Isaiah Washington ni mzaliwa wa Marekani,aliyegundulika kuwa  na mizizi ( DNA) kutoka Siera Leonne. Historia hiyo, ilimplekea mapenzi makubwa na nchi hiyo hadi kuchukuwa Passport  rasmi na kushiriki  katika kusukuma gurudumu la maendelea, pamoja na

SIERRA LEONE, EBOLA - FREE !

Tarehe 7/11/2015, Shirika la Afya Duniani  “WHO”  lilitangaza ushindi katika uthibiti wa maambukizi ya Ebola nchini Sierra Leone. Tamko hilo lilifuata baada ya siku 42 kupita, pasipo na tokeo la maambukizi ya ugojwa wa Ebola nchini Sierra Leone. Mgojwa wa mwisho kunusurika na Ugojwa huo ni 'Mama Adama Sankof'(katikati) ambaye alipata maambukizi hayo wakati akimlea mwanae wa umri wa miaka 23 aliepoteza uhai. WANANCHI WAKISHEHEREKEA MAFANIKIO KATIKA KUTHIBITI MAAMBUKIZI  YA EBOLA SIERRA LEONE HATUA  MUHIMU  ZIKIENDELEA KATIKA UTHIBITI WA MAAMBUKIZI YA EBOLA. WANANCHI WAKIOSHA MIKONO KWA SABANU NA BLEACH Shukrani za dhati kwa wauguzi ,wanavijiji,viongozi,mashirika mbali mbali, wanadiaspora,nchi za mbali na za jirani,vyombo vya habari na wale wote waliopoteza wapendwa wao  kwa ajili ya kuokoa maisha.