Skip to main content

Posts

Showing posts from August, 2015

UDHAMINI WA ELIMU YA JUU KWA MAMA ALIYE NA NDOTO YA KUJIENDELEZA @ MONTGOMERY COLLEGE.

NAFASI MOJA IMEBAKI NA INATOLEWA KWA   Mwenyeji  wa  Montgomery County Mwanadiaspora M- Tanzania Asiye na ndoa Mwenye  mtoto/watoto  Anayeishi katika mazingira magumu akitegemea  ndugu au rafiki . Mama ni Nguzo ya Jamii WASILIANA NASI  Tel. 240- 672-1788 Email- NesiWangu@gmail.com Thanks, Image; mobile.nation.co.ke

DRIVE-BY-SHOOTING!

Ni uhalifu  unaojumuisha gari lililo katika mwendo huku likimwaga risasi kwa raia. Uhalifu huu wa kinyama ni sugu katika baadhi ya maeneo, hasa kwa ndugu zetu wanaoshiriki katika Magenge ya vurugu au gangs. Mbaya zaidi, uhalifu huu hutokea ghafla na kuchukuwa maisha ya raia wasio na hatia. Leo nilinusurika maisha nikiwa  katika eneo la 7th st. NW DC. Ilikuwa  mida ya saa kumi jioni ambapo shambulizi la ghafla la risasi zilizolia kama kifaru zilimiminika kutoka kwa gari isiyojulikana. Raia  walikimbia , wengine kujificha na hata kulala chini ili kuokoa maisha . Baada ya dakika chache, kikosi kikubwa cha Police na Emergency Response 911, kiwasili  na kutoa huduma ya haraka kwa majeruhi. Taarifa ya baadaye  ya Fox 5 News, iliripoti kuwa kijana wa umri wa miaka 23,Mathew Shlonsky ambaye alikuwa mpita njia  alifariki dunia baada ya kufikishwa hospitalini.                     Polisi wakiongea na raia ili kupata machache yatakayoweza saidia uchunguzi wao.