Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2014

AJICHUBUAE HUKUSUDIA KUTATUA TATIZO LA MTAZAMO NA SIO TATIZO LA RANGI YA NGOZI !!.

Binadamu ni kiumbe anayependa kukubalika. Pengine, hata zaidi ya anavyojikubali mwenyewe.Iwapo mwanadamu anahisi kutokukubalika katika jamii inayomzunguka, huwa mpweke,mnyonge na  mwenye msongo wa mawazo. Hisia ya kutaka kukubalika humfanya binadamu afanye lolote hata ikibidi kubadilisha muonekano wake ilimradi akubalike katika jamii inayomzunguka.Hali hii inaonyesha wazi kwamba mazingira yetu yana nguvu kubwa katika kuchangia fikra, matendo na imani zinazobobea katika  tamaduni zetu. Faida za hisia hizi ni kwamba, zikiambatana na utashi mzuri, ufahamu binafsi na upeo, huleta mafanikio makubwa kwa mtu na kwa jamii .Hasara za hisia hizi ni pale zinapoambatana na ukosefu wa ufahamu binafsi, mwongozo potofu na  upeo duni,  kwani huwa ni chanzo cha  majanga yanayotuongezea uduni wa maisha. Baadhi ya mitazamo duni inayotuathiri ilisababishwa na ukoloni uliotufunza chuki binafsi na kutuacha na pigo kubwa la fikra. Pigo hili limetuletea imani potofu na madhari mengi k

PATA MSAADA WA CHETI CHA ELIMU YA HUDUMA YA AFYA 'CNA, .

Mwisho wa Msaada huu ni tarehe 12/05/ 2014 Kwa maelezo zaidi wasiliana na Kimberly Brown @ 240-567-1409 saa 7 mchani hadi saa 9 mchana au waweza kwenda Montgomery College kwenye office husika Accelerating Connections to Employment Grant Certified Nursing CNA Career Benefi Disclosure Statement: ACE Project: This project is funded by the US Department of Labor under contract #IF-23245-12-61-A-24. It is part of a national evaluation being conducted by Abt Associates (Bethesda, MD). The ACE evaluation is being conducted by ICF International (Fairfax, VA) and the evalua- tion design has been reviewed and approved by the ICF Institutional Review Board, #4292013. This project is a partnership between Montgomery College and the Montgomery Count Workforce Investment Board.

WIKI YA MANESI DUNIANI 2014 !.

Wiki hii   ni wiki rasmi ya kuwatambua Manesi wote duniani na kuwashukuru kwa mchango wao mkubwa katika jamii.Historia inatueleza kuwa  tarehe 12 mwezi wa tano,ikiwa siku ya mwisho ya kuadhimisha wiki ya Manesi,  ni siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa elimu ya juu ya unesi ‘Florence Nightingale’. Mbali na mchango wake wa nadharia  katika kitengo cha malezi ya afya, Florence Nightingale alipewa jina la   “ The Lady with a lamp”  kwa umaarufu  wake wa kubeba taa ya chemli na kutembea usiku wa manane akishughulika na majeruhi wa vita vya Crimean mnamo mwaka 1853 – 1856.   Leo pia, ni vyema tuwakumbuke watabibu wa jadi waliojitolea kutibu wagojwa kwa dawa za miti shamba na kutoa huduma ya ukunga.Japo hatuwatambui kwa majina, tunawapongeza kwa maarifa  na kazi nzuri waliofanya katika mazingira ya nyakati zile.                             KAZI YA MANESI NI KAZI YENYE CHANGAMOTO NYINGI;   Kutokana na uhaba wa manesi,wengi wao hulazimika kufanya kazi zaidi ya m