Binadamu ni kiumbe anayependa kukubalika. Pengine, hata zaidi ya anavyojikubali mwenyewe.Iwapo mwanadamu anahisi kutokukubalika katika jamii inayomzunguka, huwa mpweke,mnyonge na mwenye msongo wa mawazo.
Hisia ya kutaka kukubalika humfanya binadamu afanye lolote hata ikibidi kubadilisha muonekano wake ilimradi akubalike katika jamii inayomzunguka.Hali hii inaonyesha wazi kwamba mazingira yetu yana nguvu kubwa katika kuchangia fikra, matendo na imani zinazobobea katika tamaduni zetu.
Faida za hisia hizi ni kwamba, zikiambatana na utashi mzuri, ufahamu binafsi na upeo, huleta mafanikio makubwa kwa mtu na kwa jamii .Hasara za hisia hizi ni pale zinapoambatana na ukosefu wa ufahamu binafsi, mwongozo potofu na upeo duni, kwani huwa ni chanzo cha majanga yanayotuongezea uduni wa maisha.
Baadhi ya mitazamo duni inayotuathiri ilisababishwa na ukoloni uliotufunza chuki binafsi na kutuacha na pigo kubwa la fikra. Pigo hili limetuletea imani potofu na madhari mengi katika jamii zetu .
KABLA BAADA
BAADHI YA TEKINOLOJIA,DAWA NA VIPODOZI VYA KUBADILI RANGI
TANNING BOOTH AU JOKOFU LA KUBADILISHA RANGI YA NGOZI
SINDANO NA VIDONGE VYA GLUTATHIONE VYA KUBADILI RANGI YA NGOZI
VIKIFWATIWA NA BAADHI YA ATHARI NA MADHARA YAKE MWILINI
Stevens-Johnsons Syndrome
Hali hii hutokana na Jibu la Mwili kwa Dawa au Maambukizi
|
Toxic Epidermal Necrolysis BAADHI YA VIPODOZI VITUMIKAVYO NA VYENYE MCHANGANYIKO WA MADAWA MAKALI |
- Hydroquinone’
Dawa hii huuwa chembe zinazohusika na uzalishaji wa rangi ya mwili Melanin na kuondoa ganda la nje lenye kutukinga na mionzi mikali ya jua na hivyo kuruhusu ganda la ndani ‘‘Dermis layer’ kupokea mionzi mikali ya jua na kutupelekea hatari za kupata saratani ya ngozi.
Madhara ya Matumizi Hydroquinone kwa Mda Mrefu;
- Madoa sugu ya bluu au meusi mwilini
- Upungufu wa ulaini na umahiri wa ngozi ( loss of natutre skin elasticity)
- Ugumu wa majeraha kuponya
- Pamoja na kupata mkojo na jasho lenye harufu ya samaki.
Baadhi ya majina tofauti yatumikayo kwenye vipodozi vyenye hydorqunine ni 1,4 Benzenediol,QuinolBenzene-1,4-Diol,p-Diphenol,p-Dihydroxyl,benzene,Hydrochinonep,Hydroxylhenol,Hydrochinonium,Hydroquinol,Tequinol,Monobenzyl eth.
Makala Itakayofuata tutaangali madawa mengine kama Mercury,Steroids na madhara yake mwilini.
SHUKRANI
http://www.kanyetothe.com/
http://www.kanyetothe.com/
Comments
Post a Comment