Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2014

MAFUNZO YA NesiWangu KATIKA SHEREHE ZA MUUNGANO WA TANZANIA

Tukisheherekea siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, katika Ubalozi wa Tanzania,Washington DC,  timu yetu kutoka  NesiWangu Blog Ilishiriki katika kutoa Elimu Afya kwa wageni na wenyeji walisioshiriki. Zoezi hili limetupatia uelewa wa ndani hasa kwani kuna magojwa mengi yakiwemo "Sleep Apnea" a.k.a Kukabwa na Jinamizi, yanayosumbuwa wengi katika jamii na wengi wetu hatuyatambui japo madhara yake ni makubwa katika miili na afya zetu, Mbali na magojwa,tuligusia vyakula vyetu vya asili na viburudisho ambavyo bila kipimo na usahihi wa mapishi au maandalizi yake vyaweza kuwa chanzo cha magojwa   sugu yanayosumbuwa jamii zetu. Maandishi haya yamewekwa katika lugha ya kingereza  bila tafsiri kwani ndio Lugha iliyoyumika kutoa  mafunzo siku ya Muungano kutokana na mchanganyiko mkubwa wa watu waliyotumia lugha hiyo.  shukrani; picha  SwahilivillaBlog

MAAMUZI YA KIAFYA YA RAIS WA WATANZANIA DMV

Raisi wa Watanzania DMV Bw. Iddy Sandaly Akizungumza na blog ya NesiWangu, Raisi Iddy Sandaly alitueleza kwamba amefikia uwamuzi na mkakati wa kuanza zoezi kutokana na ushauri wa daktari katika siku ya maangalizi ya afya DMV. Nia kubwa ya mazoezi haya  ni kupunguza mwili na hatari za magojwa sugu  yanayonyemelea mwili kama Kisukari,Shinikizo la damu, Kukabwa na jinamizi usingizini au (sleep apnea) na mengine mengi. Ili kuitunza afya vyema, ni vizuri kupata vipimo,uchunguzi wa afya na ushauri wa daktari walau  mara moja kila mwaka.Hii itatusaidia kujua ni jambo lipi tushughulikie mapema kwani kinga ni bora kuliko tiba.   Shukrani; NesiWanguBlog;

MAKALA YA PILI YA TATIZO LA THYROID 'HYPERTHYRODISM'

Wapendwa wasomaji wangu, leo naomba turudi tena  darasani ili tuendelea na makala yetu iliyotangulia tukiongelea ' Tezi ya Thyroid' na matitizo yake. Kwanza  tufahamu tofauti ya maneno yafuatayo; HYPO yamaanisha   Chini au Iliyochini (low ) HYPER yamaanisha Juu  au Iliyojuu (high) 'HYPERTHYROIDISM' u go jwa ambao mara nyingi hutokea kwa wanawake  kati ya umri wa miaka “20 hadi 40” (Davies & Larsen, 2008).Japo ugojwa huu waweza tokea kwa wanaume,watoto na wanawake wa umri wowote, Hyper thyroidism hutokea pale tezi ya thyroid inapozalisha homoni za  thyroid kwa kiwango cha juu kupitiliza kipimo sahihi mwilini ( thyrotoxicosis) Kama tulivyoona kazi ya homoni za thyroid mwilini, zikihusika na  usimamiaji na utendaji wa metaboli wa mifumo  mbali mbali kama;  usagaji wa chakula,mapigo ya moyo, utumiaji wa calori na mingineyo, mgojwa wa hyperthyrodism anapozalisha homoni nyingi kupitiliza kipimo,hali hiyo humpelekea dalili zifuatazo ; Upan

HABARI NJEMA KWA NESI ALIYESOMA NJE YA NCHI !

TANGAZO LA HUDUMA MBALI MBALI ZA JAMII

ILIVYOKUWA SIKU YA MAANGALIZI YA AFYA DMV !.

                               Dr.Carol Jagdeo na Dr.Rashid Ahmed  wakiongoza timu ya HCP Metro DC                           

VIDEO YA MAANGALIZI YA AFYA DMV.

SHUKRANI; HCP Metro DC na NesiWangublog inapenda kutoa shukrani za dhati  kwa wataalamu wa afya waliojitolea, TanoLadies,uongozi wa University Methodist Church,jumuiya ya Watanzania 'ATC' pamoja na mchungaji  Shideko na wengine wote mliojitoa kufanikisha huduma  hii ya msingi kwa jamii. Shukrani kwa picha ya Video; Swahilivilla

MATATIZO YA THYROID KWA WANAWAKE .

Thyroid ni mojawapo ya tezi zilizo mwilini zinazozalisha  homoni  (hormones) zake ndani ya mwili  na kutumika  kwenye mfumo wa  damu. Miongoni mwa kazi za homoni ya thyroid ni    kusimamia  utendaji wa shughuli  mwilini kama mwendo wa mapigo ya moyo,( heart rate),  usagaji wa chakula (digestion) ,mwendo na utendaji wa metaboli (metabolism)  na kusimamia matumizi ya calorie mwilini. Ili tezi ya thyroid iweze kufanya kazi yake ya uzalishaji homoni  huitaji madini ya Iodine.Madini  hayo hupatikana katika vyakula vya mimea vilivyotoka  kwenye udongo wenye virutubisho vya iodine ya kutosha, chumvi yenye iodine na vyakula vya baharini. Tezi ya thyroid inapozalisha homoni pungufu na kipimo kinachohitajika  husababisha  hali ijulikanayo kama   “Hypothyrodism”. Tezi hii  ikizalisha  homoni kupita kipimo kinachohitajika mwilini huitwa “Hyperthyrodism” LEO NINAPENDA KUZUNGUMZA NANYI KUHUSU UGONJWA WA HYPOTHYRODISM Hypothyrodism ni ugojwa ambao huwapata  wanawake zaidi kuliko

TUNAOMBA MIKONO NA ROHO ZENU KARIMU KWA MAANGALIZI YA AFYA DMV!.

Tarehe; 04/12/2014   Saa;3:00 asubuhi hadi mchana 7:00 (waweza kuja hata kwa lisaa limoja)  3621 Campus Drive,College Park MD 20740 Mikono ni kiungo cha mwili kilichojaliwa  uwezo mkubwa  na vipaji vingi. Ikitumika  vizuri yaweza kujenga hekalu na kwa maamuzi yaweza kulibomoa. Mikono hiyo hiyo, inapokutana na roho karimu miujiza hutendeka duniani na maisha huwa mazuri. Leo hii wadau wetu tunaomba tutumie mikono na roho zenu karimu kwa chochote kile mtakachoweza kufanya katika mchakato huu wa maangalizi ya afya kwa wadau wa DMV.  Iwe ni kumsadia mtu usafiri, kumwandikisha jina, kubeba meza  au kushiriki katika timu ya kitaalam Kina mama zetu wengi,,dada,kaka na baba zetu,wanakesha wakitamani  watu wenye  roho karimu na mikono kama ya kwako ili kupata huduma ya afya. Pengine hii ndio huduma yenyewe kwa mwaka huu.  Shukrani zetu kwa ukarimu wenu na m sisite kuwasiliana nasi  @ Nesiwangublog@gmail.com ili tuweze kupata idadi na uhakika wa msaada wako. UZIMA TULI