Wapendwa wasomaji wangu, leo naomba turudi tena darasani ili tuendelea na makala yetu iliyotangulia tukiongelea 'Tezi ya Thyroid' na matitizo yake.
Kwanza tufahamu tofauti ya maneno yafuatayo;
- HYPO yamaanisha Chini au Iliyochini (low)
- HYPER yamaanisha Juu au Iliyojuu (high)
'HYPERTHYROIDISM' ugojwa ambao mara nyingi hutokea kwa wanawake kati ya umri wa miaka “20 hadi 40” (Davies & Larsen, 2008).Japo ugojwa huu waweza tokea kwa wanaume,watoto na wanawake wa umri wowote, Hyperthyroidism hutokea pale tezi ya thyroid inapozalisha homoni za thyroid kwa kiwango cha juu kupitiliza kipimo sahihi mwilini (thyrotoxicosis)
Kama tulivyoona kazi ya homoni za thyroid mwilini, zikihusika na usimamiaji na utendaji wa metaboli wa mifumo mbali mbali kama; usagaji wa chakula,mapigo ya moyo, utumiaji wa calori na mingineyo, mgojwa wa hyperthyrodism anapozalisha homoni nyingi kupitiliza kipimo,hali hiyo humpelekea dalili zifuatazo ;
Upande wa Ngozi
- Kutokwa kwa jasho kupita kiasi
- Nywele nan vinyweleo huwa nyepesi vilaini
- Ngozi ya mwili huwa laini,ya joto na yenye unyevu
Upande wa Mapafu
- Kuhishiwa kwa pumzi bila shunguli yeyote ( Shortness of breath)
- Pumzi nzito na ya haraka haraka
- Kupungukiwa kwa uwezo wa kuipumua hewa baada ya kuivuta ( decrease vital capacity)
Upande wa Moyo
- Mapigo ya moyo yenye kiherehere ( Kamusi translation of Palpitation…...)
- Mapigo ya moyo ya kasi
- Mapigo ya moyo yaliyotoka nje ya mpangilio na yenye hitilafu
- Maumivu ya kifua
- Ongezeko la shinikizo la damu hasa namba ya juu (systolic pressure >120 mmHg )
Upande wa Tumbo
- Ongezeko la njaa na hamu ya kula
- Ongezeko la haja kubwa
- Kupungua kwa mwili
- Kupungua kwa protein kwenye damu
- Ongezeko la sukari kwenye mzunguko wa damu
Upande wa Misuli ya Kiunzi cha Mifupa ( Musculoskeletal )
- Udhaifu wa misuli
- Kupotea kwa umahiri wa misuli
Upande wa Mishipa ya fahamu
- Kuona maruerue au maono mara mbili( double vision,blurred vision)
- Ochovu wa macho na uguu wa kustahimili mwanga mkali
- Kupatwa kwa kidonda ndani ya jicho au maambukizi
- Ongezeko la machozi,wekundu wa jicho
- Kuzama kwa sehemu ya juu ya jicho na kuzorota (eyelid)
- Kutetemeka kwa mwili (tremors)
- Ukosefu wa usingizi
- Exophalomous
Exophalomous au Kutokwa kwa macho kwa tatizo lililozidai |
Upande wa Metaboli
- Ongezeko la kasi ya metaboli
- ugumu wa kustahimili mazingira ya joto
- Homa ya chini au homa ndogo kati ya 99 -101 F
- Uchovu
Upande wa Kisaikolojia
- Upungufu wa umakini
- Ukosefu wa utulivu au kuwa na mahangaiko
- Hisia zilizo ngumu kuzizatiti au za kupita kiwaida
Upande wa Mfumo wa Uzazi
- Kutoweka kwa siku za mwezi au kupungua
- Ongezeko la msukumo wa tendo la ndo
Dalili Nyinginezo
- Goiter (kuvimba kwa tezi ya thyroid) japo yaweza kutokea hata kwa asiyekuwa na hyperthyroidism, mfano ukosefu wa madini Iodine,ujaa uzito,ugojwa wa Hashimitosh, na mengineyo mengi
Hyperthyroidism na Hypothyroidism ni ugojwa ambao unasimamiwa na mtaalamu ajulikanaye kama “Endocrinologist” ikimaanisha mtaalamu wa tezi zinazozalisha homoni ndani ya mwili na kutumika katika mzunguko wa damu.
DALILI NA MAFUNZO YA TOVUTI HII NI JITIHADA ZA KUELIMISHANA NA KUJIFAHAMU ZAIDI, USHAURI WA DAKTARI NA VIPIMO VYAKE NDIO UHAKIKA SAHIHI WA UGOJWA ULIO MWILINI.
Ignatavicius, D.D. & Workman, M.L. (2010). Medical-Surgical Nursing: Patient-Centered Collaborative Care (6th ed.).
IMAGES;
www.medrevise.co.uk,blog.destroydiseases.com, blog.grannytherapy.comdxline.infonisarvtr.blogspot.com ,
Comments
Post a Comment