0
TIBA YA HARAKA KWA UPUNGUFU WA SUKARI MWILINI (HYPOGLYCEMIA)
Ubongo wa binadamu unahitaji sukari kwa mda wote ili kuwa na nguvu ya kufanya kazi .
Sukari hii yategemewa kutoka kwenye mzunguko wa damu kwani ubongo hauna uwezo wa kuzalisha au kuhifadhi sukari ya kutosha matumizi ya baadaye.
Kutokana na hitilafu ya kingosho(dysfunctional pancreas) wagowja wa kisukari huwa na hali ngumu ya kuweka sukari katika vipimo vinavyohitajikana hivyo
mara nyingi sukari huwa juu (Hyperglycemia) au chini (Hypoglycemia) na huhitaji tiba.
Hivyo basi ni muhimu sana kwa ndugu au rafiki wa karibu kujua machache ili kuwa msaada pale mpendwa wako anapojikuta katika hali ya kuishiwa sukari kwani inahitaji huduma ya haraka kuokoa maisha.
DALILI ZA UPUNGIFU WA SUKARI MWILINI (Hypoglycemia)
Kipimo cha sukari chini ya 70 mg/dL au 3.9 mmol/L
chaweza hatarisha maisha ya mpendwa wako mwenye kisukari. ;
- Njaa
- kuumwa kwa kichwa
- Kutokwa kwa jasho
- Hasira
- Mwili au ngozi baridi na nyevu
- Kizunguzungu
- Mapigo kasi ya moyo
- Kushuka kwa pressure ya damu
- Kutoa sauti kubwa au kulia endapo yu usingizini
- Uhafifu wa kuona
- Upungufu wa ufahamu ( kuchanganyikiwa )au kusema vitu visivyoeleweka
- Ugumu wa kuongea
- Kuzimia
TIBA YA HARAKA KWA UPUNGUFU WA SUKARI MWILINI (HYPOGLYCEMIA)
Kinywaji au kitafunio hutumika kwa usalama kwa wale wanye fahamu na kuweza kumeza, kwa waliopoteza fahamu wahitaji kupata msaada wa haraka kwa mtaalamu
Serving Size (15 grams)
|
Carbohydrate Food
|
1/2 cup
|
Regular soda pop/
|
1 cup
|
Skim or 1% milk
|
1/2 cup
|
Fruit juice
|
3-4
|
Glucose tablets
|
4 teaspoons
|
Sugar
|
1 Tablespoon
|
Honey, syrup, or jam
|
5-6
|
Hard candies (i.e. Lifesavers or peppermints)
|
Baada ya treatment hii subiri kwa dakika 15 na pima sukari ambayo inatakiwa kuwa kati ya 70-110 mg/dl au 3.9 - 6.2 mmol/L . Kwa kipimo kilicho chini zaidi, waweza kurudia treatment hii hadi mara tatu na kupima tena sukari, kama bado kipimo cha ashiria sukari iliyo chini pata msaada wa haraka na kumwona daktari au call 911..
UPUGUFU WA SUKARI MWILINI KWA WAGONJWA WA KISUKARI WAWEZA KUSABABISHWA NA ;
- Insulin complications
- Kupitiliza saa za mlo na ukosefu wa chakula
- Utumiaji wa pombe
- Baadhi ya dawa ( eg. quinine,....)
- Kwa wale wenye diabetes Type 1 ni muhimu sana kupima na kutumia kitafunio kabla ya mazoezi, kwani mazoezi ya mda mrefu yaweza kukuweka kwenye hatari ya upungufu wa sukari mwilini.
Insulin ni hormone ambayo huzalishwa na chembe za kingosho(pancreas) pale ambapo umekula au sukari iko juu kwenye damu.Hivyo insulin husisimua chembe za mwili kunyonya sukari na kuhifadhi kama mafuta au nguvu ya akiba huku ikibakisha kiwango cha kutosha katika mzunguko wa damu. (kwa wale wenye ugojwa wa sukari umbile hili halifanyi kazi vizuri na hivyo yabidi kutegemea insulin ya bandia ili kuweza simamia(kucontrol) kiwango cha sukari kwenye mzunguko wa damu )
Na vile vile Kingosho hichi, husisimua uzalishaji wa glucagon ambayo ni kama chakula,nguvu au sukari pale upungufu unapotokea; kwa mfano wakati wa njaa,mafungo au kupungukiwa na sukari kwenye damu. Hivyo sukari au glucose huongezeka katika mzunguko wa damu.
Tatizo ni pale tunapochanganya haya mawili, kwani wengi wamepoteza maisha kwa kuwekewa Insulin pale wanapoonyesha dalili za kuishiwa na sukari mwilini. Insulin siyo ya mtu aliyehishiwa sukari kwani insulin huzidi kunyonya sukari kutoka kwenye damu na kutuweka katika hifadhi ya mwili,hivyo damu inakaukiwa sukari na kumweka mgojwa kwenye hatari ya kuishiwa nguvu,kupoteza ufahamu au kuzimia na pale isipopata suluhishi coma hata kifo hutokea. Mtu aliyeishiwa sukari anahitaji kuongezewa kama maelezo yaliyotangulia na pale anapokuwa amepoteza ufahamu na kushidwa kunywa au kula kitafunio, mtaalamu wake hutoa sindano ya glucagon ya kuongeza sukari mwilini .
Ushauri kwa wagojwa wa kisukari
- Kuvaa bangili inayoashiria tatizo lako yaweza kukusaidia, kwani itatoa ufafanuzi zaidi kuhusu cha kufanya au kuepuka kufanya endapo umepoteza fahamu.
- Ni vizuri kutembea na kitafunio au kuweka glucose,pipi,hasali au juice katika office au nyumbani kwani huwezi jua ni lini itahitajika kwa haraka.
- Ni vyema kukaa chini na familia yako na mufunzane kuhusu ugojwa huu na namna ya kukabiliana nao, kwani huwezi jua lini na ni wapi itatokea.
- Fuata masharti ya daktari wako; epuka mikate, nyama nyekundu,mikaango, wali mweupe na pombe, kwani vyazidi kukuumiza.
- Tumia brown rice(ile yenye makapi yake, loeka kabla ya kupika), kunde,oatmeal na mboga za majani (hasa salads husaidia kunyonya sukari mwilini).
- Pata mazoezi ya kutembea kila siku ,hii husaidia sana kupunguza sukari katika mzunguko wa damu bila kuihifandhi mwilini na kuongeza uzito,kurahisisha mzunguko wa damu mwilini,kupunguza ongezeko la cholesterol na kudumisha umahiri wa vishipa kwani hili ni tatizo kubwa kwa wagojwa wa kisukari na ndio maana wengi huwa na matatizo ya vidonda visivyopona.
- Kagua miguu na vidole mara kwa mara, kwani wengi wenye kisukari,hupoteza hisia ya sehemu mbali mbali mwilini na kutojua kama wanakidonda. Hii yaweza chelewesha huduma ya haraka na kusababisha kidonda sugu na infection ambacho mara nyingi ndio chanzo cha kukatwa kwa kiungo hicho.
- Epuka viatu vya kubana na kuchubua ngozi
- Kata kucha mara kwa mara na hakikisha usafi wake.
- Pima wa joto la maji kabla ya kuogea. Ugojwa wa kisukari una hatua tofauti na pale unapodhuru mishipa ya mwili (diabetic neuropathy) mgojwa anaweza kuwa anaunguwa na maji ya mot bila kuhisi maumivu na hivyo kuwa kwenye matatizo makubwa.
.
I
Shukrani;
Ignatavicius, D.D. & Workman, M.L. (2010). Medical-Surgical Nursing: Patient-Centered Collaborative Care (6th ed.). Philadelphia: Elsevier/Saunders.
www.webmd.com/a-to-z.../symptoms-of-low-blood-sugar-topic-overvie
Nimefurahi sana Kwa jinsi mtaalamu ulivyo elezea juu ya msaada wa tatizo hili ila hiyo lugha iliyo tumia kwenye jedwali la vyakula siyo lugha rafiki Kwa mtu kama mm nisiye jua lugha za kitabubu
ReplyDelete