Osteoporosis ni ugojwa sugu wa mwili kujitafunia virutubisho vilivyo kwenye mifupa na kuvitumia kwa mahitaji yake.Hii husababisha upungua wa umahiri wa mifupa(bone density) kuifanya iwe hafifu na kumegeka. Ugojwa huu huitwa “ silent disease’ kwani mara nyingi hujulikana tu pale mtu anapoanguka na kuvunjika (kwa urahisi sana au kupata fructure) tofauti na mtu asiye na tatizo hili.
UNDANI MDOGO KUHUSU OSTEOPEROSIS
Mifupa ya mwili kwa wakati wote huwa na mabadiliko ya kujingeka, kujiimarisha na
kujirepea(bone remodeling) kwa kupitia mzunguko maalaum wa kusagika(osteoclast) ambapo hutoa madini yake ya calcium katika mzunguko wa damu. Osteoperosis na upungufu wa umahiri wa mifupa (low bone mass)hutokea pale ambapo usagikaji wa mifupa (Osteoclast) uko juu zaidi ya ujengekaji wa mifupa (Osteoblast).
Binadamu hufikia kilele cha ujenzi wa mifupa kati ya umri wa miaka 25 -30,kwani kabla ya umri huu mifupa hujijenga zaidi na kusagika kwa kiwango kidogo kama inavyotakiwa.Baada ya umri wa miaka 30,usagikaji wa mifupa huuzidia kwa kina kikubwa kuliko ujengakaji wa mifupa.Hivyo upelekea upungufu wa umahiri wa mifupa( decrease bone density ).Hii inatuonyeesha jinsi gani madini ya calcium ni muhimu mwilini kwani ulaji wa chakula kisichojumuisha calcium na vitamin D (vitamin D husadia unyonyaji wa madini ya calcium kutoka kwenye chakula) husababisha mwili kutumia calcium iliyohifadhika katika mifupa. Ili calcium iweze kujitoa katika mifupa (hifadhi yake) na kutumika mwilini(ktk mzunguko wa damu), yabidi mifupa ipitie hatua ya kujisaga na kutoa kirutubisho hicho kinachohitajika na hivyo kutuacha na mifupa hafifu.
Japo Osteoperosis imekuwa ikiwapata zaidi wanawake waliyomaliza siku za mwezi (post menopausal Women) au umri wa miaka 50 na kuendelea.Leo tunaona kina dada/kaka wadogo ambao wanatunza miili yao kwa kuinyima virutubisho wakihathirika kwani umri ufikapo miaka 30, mwili unatumia hifadhi zake zaidi ya kuwekeza na hivyo hujikuta katika hatari za osteoporosis.
VIJANA WALIO HATARINI KUPATA OSTEOPEROSIS;
- Wanawake kwa wanaume wanaoingia kwenye diet kali za kupunguza mwili na kukosa viritubisho vya kutosha wakati mifupa bado inajijenga .Kwani umri chini ya miaka 25-30 bado una uwezo wa kuhifadhi calcium kwenye mifupa na kuifanya imara. Iwapo umri huu kumekuwa na upungufu wa madini haya mifupa huwa ni hafifu na kuzidia pale umri unapoongezeka.
- Kundi lingine haswa ni kwa wale wenye matatizo la kula mfano; anorexia nervosa au wanao kula na kujitapisha ili kuzuia ongezeko la mwili (bulimia)
Japo wapo ambao wanaona ni rahisi kumeza kidonge cha Calcium,vidonge hivi vinaweza kukudhuru na zinahitaji maelezo na ushauri wa daktari.vidonge vya calcium vyaweza kusababisha mawe kwenye figo na matatizo ya moyo hasa pale vinapotumika bila mpangilio .
RISK ZA OSTEOPOROSIS NI PAMOJA NA ;
- Miaka 65 au zaidi kwa mwanawake
- Miaka 75 na zaidi kwa wanaume
- Historia kifamlia
- Wanawake waliomaliza kupata siku za mwezi
- Mwili mdogo au mwembamba sana(hasa wazungu wenye mifupa midogo)
- Upungufu wa Calcium
- Utumiaji wa sigara
- Utumiaji wa pombe kwa wingi
- Ukosefu wa mazoezi ya mwili
- Kutotembea kwa mda mrefu kwa wale walio kitandani(bed ridden)
- historia ya kuvunjika baadaya miaka 50
- Baadhi ya dawa kama steroids. na magojwa tofauti kama diabetes,hyperthyroidism,bone cancer....
- Maumivu ya mgongo au tenderness,stiffiness
- Maumivu ya kiganja cha mkono wakati wa kubeba mzigo
- Maumivu ya mgongo unapojeuka au kuinama
- Maumivu yanayozidia na shughuli na kupungua ukipumzika
- Ugumu wa viungo wakati wa kuamka au maumivu
- Kuanguka na kuvunjika(hii uhashiria mifupa iliyodhoofuka)
MATUNZO YANAYOSHAURIWA KWA MIFUPA YA MWILI
- Pata mazoezi ya kutembea walau dakika 30 mara 3 - 5 kwa wiki kwani hupunguza chances za kupata osteoperosis.
- Hakikisha unapata calcium kama kutoka kwenye maziwa na mboga za rangi nzito ya kijani
- Kupata mwanga wa asubuhi wa jua ambao ni vitamin D kwani vitamin D ni muhimu sana mwilini na huwezesha unyonyaji wa calcium kutoka kwenye chakula na kuiweka katika mzunguko wa damu na hifadhi katika mifupa.
- Mazoezi laini ya vyuma (weight bearing exercises) yasemekana hupunguza usagikaji wa mifupa na kusisimua ujengekaji wa mifupa.
- Epuka utumiaji wa caffeine au vinywaji vyenye carbon kama soda nk. kwani huchangia kuondoa calcium mwilini kupitia mkojo na hivyo kuweka mwili katika ongezeko la hitaji ya calcium.
- Punguza utumiaji wa pombe na epuka sigara kwani vyote hupunguza umahiri wa mifupa kujijenga
- Utumiaji wa vyakula vya protein kwa kiwango kizuri husaidia ufanisi wa calcium mwilini kwani calcium huhitaji mazingira yenye protein ili kufanya kazi yake kimahiri.
- Pia kuwa mwangalifu kwani “high protein diet” hutuweka katika hatari za upungufu wa calcium kwani protien ikizidi sana huchangia kutoa calcium mwilini kupitia mkojo.
SHUKRANI/THANKS;
Ignatavicius, D.D. & Workman, M.L. (2010). Medical-Surgical Nursing: Patient-Centered Collaborative Care (6th ed.). Philadelphia: Elsevier/Saunders.
- Images
| Permalink
Comments
Post a Comment