Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2014

JIANDIKISHE KUPATA HUDUMA YA BURE YA KUPIMA SARATANI YA MATITI (MAMMOGRAM).

AFRICAN WOMEN CANCER AWARENESS ASSOCIATION IS COMING TO OUR COMMUNITY. JIANDIKISHE KUPATA HUDUMA YA BURE YA KUPIMA SARATANI YA MATITI (MAMMOGRAM). AFRICAN WOMEN CANCER AWARENESS ASSOCIATION (AWCAA) Imejitolea kusaidia upimaji wa saratani ya matiti (mammogram), kutoa elimu ya bure kuhusu ugonjwa huu na huduma nyingine nyingi kwa kina mama wanaoishi hapa Washington DC, Maryland na Virginia (DMV). Tunaomba kina mama mnaoishi hapa DMV kujiandikisha ili muweze kupata huduma hii ya bure kwa kila mwanamke kuanzia umri wa miaka 25 na kuendelea. Saratani ya matiti inatibika cha muhimu ni kuhakikisha tunafanya uchunguzi wa afya mapema. Kwa kujiandikisha wasiliana na Asha Hariz (703) 624-2409 or ashahariz@yahoo.com au Asha Nyang’anyi (301) 793-2833 or ashany2@yahoo.com. http://www.awcaa.org/ Shukrani AFRICAN WOMEN CANCER AWARENESS ASSOCIATION;

IJUWE SARATANI YA TEZI YA PROSTATE ( PROSTATE CANCER )

Tezi ya prostate ni tezi yenye umbile la donati, iliyoko chini ya kibofu cha mkojo.Tezi hii huzungukwa na  mirija  ya mkojo na uhusika uzalishaji wa maji maji yanayohusika na urutubishaji na usafirishaji wa mbegu za kiume (semen). Mabadiliko ya kimaumbile katika tezi dume kama; uvimbe au ongezeko la ukubwa huleta hitilafu katika mfumo mzima wa mkojo kutokana na ukaribu wa maumbile hayo. Uvimbe katika tezi dume husukuma mirija ya mkojo kwa kuibana na kufanya mkojo upite kwa shida, ukwame au kuchuruzika bila kukusidia. Hali hii humpelekea mgojwa uhitaji wa kutumia bafu mara kwa mara. Zaidi huwa vigumu kwa mgojwa kuzuia mkojo usichuruzika au kukwama .  (Maumbile ya mwili, yamekadiriwa kulingana na nafasi iliyopo, hivyo umbile moja linapoongezeka ukubwa kinyume cha taratibu huleta hitilafu kwa mfumo mwingine jirani). BAADHI YA MATATIZO YA TEZI YA PROSTATE Prostate Cancer ( Saratani ya tezi ya Prostate )
JE WAJUA NAMNA YA KUMHUDUMIA MGOJWA WA KISUKARI? NesiWangublogpost ikishirikiana na " African American Health Program" inawakaribisha katika mafunzo ya afya ya huduma kwa ugonjwa wa kisukari .Tutazungumzia athari zake,dalili, kinga na njia mbali mbali za kukabiliana na ugojwa wa kisukari. Mafunzo yatafanyika; Wapi? Downtown Silver Spring MD, Civic Building. Tarehe: 12/7/2014, Saa: 4:00 asubuhi hadi 7:00 mchana Anuani: 1 Veterans Plaza, Silver Spring MD 20910 Kwa maelezo zaidi piga simu 301 213 1973 au 240 672 1788 Email: anitamwalui@gmail.com au NesiWangublog@gmail.com  Kwa maelezo zaidi angalia tovuti ya www.Onehealthylife.org                                                 KARIBUNI NYOTE "The African American Health Program is dedicated to serve the AA and African communities in Montgomery County through diabetes prevention and control awareness and education. The program sponsors 2 African American Healthy Living Dining clubs, an African

SWALI KWA WASOMAJI WANGU !.

JE KUNA MTU ANAYEFAHAMU VITUO MBALI MBALI NCHINI TANZANIA VINAVYOFANYA UCHUNGUZI KWA AFYA ZA WANAWAKE KAMA   PAP-SMEAR TEST ? Tafadhali wasiliana nami kupitia NesiWangublog@Gmail.com Asanteni sana Shukrani www.ihealthrn.com