Skip to main content

Posts

Showing posts from 2018

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ambayo hutokana na mabadiliko ya mfumo wa chembechembe au cells zilizoko  katika shingo ya kizazi.Mabadiliko haya hupelekea chembe chembe hizo kushamiri na kuzaliana kwa kasi kinyume na mpangilio wa maumbile. Saratani ya Shingo ya kizazi yasemekana kuwa ni saratani inayoongoza kwa kusababisha vifo vya  wanawake katika nchi zinazoendelea. Repoti ya 2012 ya shirika la afya duniani 'WHO' imesema kati ya matukio 75,000 ya waathirika wa saratani ya kizazi barani Afrika, 50,000 walifariki dunia.Namba za matukio haya zinawakilisha waathirika waliopata fursa ya utafiti jabo NINI KINACHOSABISHA SARATANI YA SHINGO YA UZAZI ? Ripoti za utafiti wa kisayansi zimeafiki kuwa asilimia 99%  ya saratani za shingo ya kizazi hutokana na maambukizi ya virusi vya ' Human Papillomavirus' au HPV vilivyoko katika jamii ya papilloma. Baadhi ya virusi hivi vyenye aina zaidi ya mia moja huambukizwa kwa njia ya  kujamiana. BAADHI YA MAMBO