Skip to main content

Posts

Showing posts from March, 2015

Global Health Catalyst Cancer Summit @ Harvard Medical School 2015.

Mhe.Liberata Mulamula Balozi wa Muungano ya Jamhuri ya Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula, alipozungumza  katika kongamano  la mapambano dhidi ya gojwa la saratani duniani, aliwataka wanaDiaspora wa nchi za kiAfrika kuwa mstari wa mbele kwa kushirikiana na watalaamu wa vitengo vya afya duniani ili kuboresha upatikana wa huduma za afya barani Afrika. Mhe. Balozi Mulamula, ambaye pia ndie aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo alizungumzia faida za kutumia Teknolojia  ili kuboresha mawasiliano kati ya wataalam, utafiti na  elimu .  Nia mojawapo ya  kongamano la Global Health Catalyst Cancer Summit 2015 ni kuboresha huduma mahiri za saratani barani Afrika kwa  kutumia ( Information and Communication Technologies (ICTs); Teknolojia ya mawasiliano kati ya wataalam wa gojwa la saratani wa nchi za nchi za ng'ambo  na wataalam waliopo barani Afrika. Mhe. Balozi L. Mulamula, alikabidhi Tunzo Maalum kwa Bigwa wa Tiba ya Saraatani Dr. Twalibu Ngoma.  Dr.Ngoma ni miong

HUC - Help for Underserved Communities HUC- USA; Shirika Lililoanzishwa na Wanadiaspora waTanzania Likiwa Mstari wa Mbele Katika Kutoa Huduma ya Elimu kwa Vijana Wahitaji Nchini Tanzania

 Help for Underserved Communities Inc. (HUC) –USA imewapatia ufadhili vijana  22  wa kozi mbalimbali za ufundi katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi(VETA), Tanzania kwa mwaka 2015. Kati ya wanafunzi hao 22, wanafunzi sita wanatoka kwenye vituo vya kulea yatima, ikiwemo wanafunzi wawili kutoka  Lady Queen of Africa Orphanage ya Kurasini Convent,  Albino Charity Organisation ya Buhagija, Shinyanga na Yatima School ya Chamazi, Dar-es-Salaam, Tanzania. 2015 HUC Scholarship recipients completing admission forms for VETA.   |  Vijana wanaofadhiliwa na HUC wakijaza fomu za kujiunga na kozi mbalimbali za ufundi VETA, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kwa Maelezo zaidi pita anuwani ifwatayo;   https://www.facebook.com/ pages/Help-for-Underserved- Communities-HUC-USA/ 412893725452394

NesiWangu Show- Albinism

Katika sehemu hii ya pili, Harriet Shangarai wa NesiWangu Media anazungumza na mwanaharakati mwenye Albinism Babu Sikare kuhusu maisha yake na shirika lake la ' Afrobino'  la kupambana na changamoto inazowaguwasa walemavu wa ngozi katika nchi zinazoendelea.   Shukrani' KP; Kwanza Production

NesiWangu Show -Albinism

NesiWangu-Show Inawaletea sehemu ya kwanza ya mazungumzo na mwanaharakati Bi " Daisy Makwaiya" mwenye shirika la Albino Charity.org  ikifwatiwa na Sehemu ya pili ya  -- Mazungumzo na Mwanaharakati "Babu Sikare" mTanzania mwenye Albinism na mwanzilishi wa  shirika la Afrobino.org   wote wako mstari wa mbele  ktk utoaji wa  huduma msingi kwa jamii ya watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi nchini Tanzania. Shukrani za dhati; Kwanza Production (KP)

JUMUIYA YA WATANZANIA DMV IKISHIRIKIANA NA AWCAA INAWALETEA HUDUME YA BURE YA UCHUNGUZI WA SARATANI YA MATITI.

UJUMBE MAALUM KUTOKA KWA NDUGU ZETU WENYE ALBNISM

KARIBU USIKILIZE UWIMBO WA KUGUSA TOKA KWA WASANII MBALI MBALI KUHUSU EBOLA!

Shukrani; Artist with One voice