Skip to main content

Posts

Showing posts from 2014

NEsiWangu Show- Home Malaria Kit

NesiWangu Show ni kipindi kinachokusudia kuongeza mwako katika uwanja wa Afya, upatikanaji wa huduma zake na elimu-afya kwa jamii. Katika kipindi hiki, tunazungumza na Mkurugenzi wa Jenga Tanzania Foundation, Nassor Basalama anayezungumzia kuhusu kipimo cha Malaria ambacho Jenga Tanzania Foundation inapanga kukisambaza bure kwa watu wa kipato cha chini nchini Tanzania. Karibu uungane nasi Attachments area Preview YouTube video NesiWangu Show. Malaria Kit NesiWangu Show. Malaria Kit

TIMU YA NesiWangu INA FURAHI KUWATAKIA HERI NA FANAKA ZA MWAKA MPYA.

Shukrani Image; coachwhittaker.wordpress.com

MSIMU WA MAFUA MAKALI MAREKANI

Hab ari kutoka  kituo cha kudhibiti magojwa nchini Marekani  “Center for Disease Control” ( CDC) 2014 -2015, inatufahamisha kuhusu kipindi cha mafua makali ( Severe FLU Season). Kipindi hiki kilichotawaliwa  zaidi na virusi vya A H3N2,hujulikana  kwa kuleta homa kali, ongezeko la  wagojwa mahospitalini na hata vifo. CDC inatukumbushia umuhimu wa kila mmoja kupata Chanjo  ya Flu na  tiba ya haraka ya kupamba na  virusi (Anti-viral drugs  treatment)  hasa kwa watu walio na kinga hafifu.  Anti-viral drugs husemekana kuwa mahiri zaidi kati ya masaa 48 baada ya dalili za flu kujitokeza mwilini . Mabadiliko ya virusi kimaumbile (genetic) huchangia kupunguza umahiri wa chanjo japo wengi  waliofanikiwa kupata chanjo huwa na maambukizi  afueni.   CDC imeongeza kusema, FLU ya kipindi hiki iliyotawaliwa na  Influenza A H3N2 ilitokea  miaka ya 2012-1213, 2007-2008 na 2003-2004  vipindi ambavyo viliongoza  kwa idadi ya vifo katika ya miaka 10 iliyopita. NINI DALILI  ZA FLU Kukohoa au kuk

NOT ONLY SHOULD WE PREPARE OUR CHILDREN FOR THE WORLD, BUT WE MUST PREPARE THE WORLD FOR OUR CHILDREN TO LIVE IN. FIGHT THE STIGMA, FIGHT THE DISEASE!

                                     With Sincere Thanks; Ambassador of  Elizabeth Glaser Pediatric Aids Foundation,Ms.'Fortunata  Kasege'

FORTUNATA KASEGE THE LIVING MOM WITH A MOVING STORY AND AN AMBASSADOR OF ELIZABETH GLASER PEDIATRIC AIDS FOUNDATION.

The Health of Moms and Babies By Fortunata Kasege | May 2, 2014   EGPAF Ambassador Fortunata Kasege is living with HIV, but she doesn’t let it stop her from embracing life and expanding her family. EGPAF Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation Ambassador Fortunata Kasege shared her journey with HIV and pregnancy with POZ Magazine on May 1, 2013.  You can read the original article here . I was only 22 years old when I learned I was living with HIV. The news was a devastating blow. I was a newlywed with a baby on the way and I had just immigrated to the United States from Tanzania to enroll in journalism school. I thought my life was just about to start, but suddenly, I felt like it was over. That was more than 17 years ago. I underwent a long and challenging journey, but today I am happy, healthy, and expecting my second child. When I was first diagnosed in 1997, I didn’t know that it was possible for someone living with HIV to have an HIV-negative child. Growi

TIMU YA NesiWangu INATOA SHUKRANI ZA DHATI KWA KAZI KUBWA IFANYWAYO NA BAADHI YA MAKUNDI KATIKA JAMII!.

Shukrani; www.topeducationdegrees.org www.grandparents.com www.accessnorthga.com

WANAUME KUSHAURIWA KUTUMIA KINGA KWA MDA WA MIEZI 3 BAADA YA MAAMBUKIZI YA UGOJWA WA EBOLA

Ripoti ya shirika la afya duniani 'WHO'  yashauri utumiaji wa kinga wakati wa tendo la ndoa  kwa mda wa miezi 3 kwa wanaume baada ya maambukizi ya Ebola.  shukrani; WHO page www.dezeen.com

UNAKARIBISHWA KATIKA JITIHADA ZA KUPAMBANA NA EBOLA

                     Montgomery County's African Affairs Advisory Group in Partnership with The Coalition Against Ebola Invites you to a Conference Ebola: Get Informed, Get Involved Tuesday, November 25, from 6PM-8:30PM Silver Spring Civic Building 1 Veterans Pl. Silver Spring, MD 20910 Expert Panel discussions on Needs and Challenges, State Efforts in Countering Stigma,      Behavioral Health and Psycho-Social Impact within the African Community, and Support Services Available . Breakout Sessions on Good Donation Practices and Fund-raising Guidelines, Stigma, REBOUND (Short term focus and long term investment strategies and economic development). For more information please contact Josephine Garnem │ jgarnem@gmail.com │  310.666.3375 Linda Aldridge │ linda.aldredge@gmail.com │ 443.333.8771

JUMUIYA YA WATANZANIA DMV INAOMBA USHIRIKANO WAKO KATIKA JUHUDI ZA KUPAMBANA NA EBOLA

WAGONJWA WA MALARIA WAPIMWA KWA MACHO !.

BY BEATRICE SHAYO 9th November 2014 Email Print Ukosefu wa vifaa tiba katika baadhi ya zahanati na vituo vya afya vya Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, umewalazimu wauguzi wa vituo hivyo kuwatibu wagonjwa wa malaria kwa kutumia uzoefu wa kuwaangalia. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika zahanati ya Mtepeche kata ya Kilimani Hewa, tarafa ya Nambambo na zahanati ya Kihuwe kata ya Naipingo, tarafa ya Naipanga wilaya ya Nachingwea, umebaini kuwepo kwa tatizo hilo. Waganga wa zahanati hizo, walisema kukosekana kwa vipimo vya kupimia ugonjwa wa malaria kunawalazimu kutibia wagonjwa kwa kutumia uzoefu wa kuwaangalia kwa macho. Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Mtepeche, Ibrahimu Mpini, alisema hutumia uzoefu kwa kumwaangalia mgonjwa kwa macho na kumpatia huduma. Alisema njia hiyo ni hatari kwa kuwa unaweza kutoa dawa za malaria wakati mgonjwa ana tatizo hilo. Alisema ukosefu wa vipimo ni changamoto ka

DAWA BANDIA ZINAANGAMIZA, WANANCHI WAFUNZWE KUZITAMBUA

BY GAUDENSIA MNGUMI 8th November 2014 Email Print Biashara ya dawa feki au bandia ni  moja ya uwekezaji haramu lakini unawapa wahusika utajiri mwingi licha ya kwamba inaweza kuwa chanzo kikubwa cha  maangamizi na mauaji duniani. Athari za biashara hii  ni nyingi lakini inasababisha usugu kwa maradhi na vifo na kuhujumu afya ya mtumiaji kwa kuwa anatumia fedha lakini haponi na matokeo yake ni kifo. MADHARA Matokeo mabaya katika eneo hili ni kutumia dawa lakini isiyokupa tiba hali inayojulikana  kitaalamu  kama Therapeutic failure. Hali hii inatokea kwa sababu dawa zinashindwa kutimiza lengo la tiba kutokana na ama kuwa na kiasi kidogo cha dozi kilichomo ndani yake au hakuna dawa inayokusudiwa kuua vimelea vya maradhi yanayomsumbua mhusika licha ya kwamba anatumia dawa hizo. Kwa ujumla dawa hizi bandia zikitumika zinashindwa kuleta tiba au kumponyesha mgonjwa kunasababisha pengine aache au kusimamisha matumizi ya dawa hiyo na

PATA HUDUMA YA MENO 50% OFF!

KAMATI YA AFYA YA WATANZANIA DMV, YAWALETEA HUDUMA YA AFYA YA MENO KUTOKA KWA MWANADIASPORA MTANZANIA AMBAYE NI MMILIKI WA AVATAR DENTAL CLINIC " DR. TAALIB ALI" DR. TAALIB NI MWANADIASPORA ALIYEGUSWA KUSAIDIA JAMII ZA WAHAMIAJI KUPATA HUDUMA YA MENO KWA BEI NAFUU. DR. TAALIB  AMEAHIDI KUTOA HUDUMA HII 50% OFF KWA KILA MTANZANIA        Dr.Taalib katika jengo la Avatar Dental Clinic Dr.Taalib na muhudumu wa Avatar Dental Clinic Avatar Dental Clinic hutoa huduma hata kwa watoto                                                            Machine ya X-ray na ya  kuua vijidudu                                                                                                Dr. Taalib akiwa Kazini KARIBUNI NYOTE UONGOZI DMV ASANTE SANA 545 G. East Market Street Leesburg, VA 20176 703-669-8600 Shukrani;Images Avatar Dental Care ATC Metro DC.

JENGA TANZANIA FOUNDATION YAKULETEA KIPIMO CHA MALARIA PAPO HAPO !

Mwanadiaspora Mtanzania na Mkurugenzi wa  JENGA TANZANIA FOUNDATION   Bw. Nasoro Ally akitambulisha rasmi Home Malaria Kit katika mkutano wa  Africa Diaspora Market Place (ADMP III) uliofanyika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani tarehe 10/27/2014. Akizungumza katika mkutano huo, Bw.. Nasoro Ally alieleza  kuwa  bado Malaria ni tishio kubwa la uhai kwa Sub-Sahara Africa na ni chanzo cha vifo vya watoto wadogo hasa chini ya umri wa miaka 5 .  Kipimo hicho chenye uwezo wa kugundua vijidudu vya Malaria mwilini kati ya dakika 5 hadi 10 kimekubalika na shirika la World Health Organization (WHO) kama kipimo sahihi na cha haraka kwa upimaji wa Malaria nyumbani.  Bw. Nassoro aliongeza kusema, kipimo hicho kitatolewa bure nchini Tanzania kwa familia zisizojiweza na kuhakikisha kinafika  sehemu mbali mbali za ndani hasa mikoani na vijijini ili kurahisisha upatikanaji wa huduma sahihi za afya na kufupisha safari ndefu na zenye milolongo. Mkurugenzi wa JENGA TANZANIA foundati

TAHARUKI YA UGOJWA WA EBOLA KUFIKA MJINI MOSHI, MKOANI KILIMANJARO

         KILIMANJARO  wakazii wa kata ya Shirimatunda, katika manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, wamejikuta katika hali ya taharuki kufuatia taarifa za kuwepo kwa mgonjwa anayedhaniwa kuwa anaugua ugonjwa hatari  wa Ebola, ambaye amelazwa katika zahanati ya shirimatunda iliyopo kwenye kata hiyo. Mgonjwa huyo aliyefikishwa katika Zahanati hiyo Juzi majira ya Jioni, ambapo hali hiyo ilisababisha huduma za afya katika zahanati hiyo kusitishwa kwa muda usiojulikana, ambapo wagonjwa waliokuwa wakipatiwa matibabu kutoka ndani na nje ya kata hiyo kuondolewa na watoto waliokuwa wakipata chanzo katika zahanati hiyo walihamishiwa katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata hiyo.   Taarifa za awali zinadai kuwa, mgonjwa ni Raia wa Tanzania mzaliwa wa Marangu wilayani Moshi, mwenye makazi yake jijini Dar es Salaam, alipokelewa katika uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro (KIA), akitokea nchini Senegal kikazi, ambapo alisafirishwa hadi kwenye zahanati hiyo baada ya kudai ku

PATA CHANJO YA FLUE BURE NA HUDUMA NYINGENE ZA AFYA KWA BEI NAFUU

KAMATI YA AFYA DMV INAWATANGAZIA HUDUMA MUHIMU  YA AFYA

WATAFITI WA DAWA YA EBOLA, A.MANGHARIBI

Kampeni ya Ebola Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema dawa ya Ebola ambayo imetengenezwa kwa mchanganyiko na damu ya watu waliambukizwa na kisha kupona ugonjwa wa Ebola inatarajiwa kuanza kupatikana wiki chache zijazo huko Afrika Magharibi. Afisa mwandamizi wa W.H.O. Dr Marie Paule Kieny amesema vifaa vimetolewa Liberia kwaajili ya kupata damu na vifaa vya kufanyia utafiti huo wa dawa ili kupata dawa Serum. Dr Kieny akizungumza mjini Geneva amesema kuwa kazi ya mapambano dhidi ya Ebola harakati za upatikanaji chanjo ya ugonjwa huo . Maelfu ya watu wanatarajiwa kutumiwa katika majaribio hayo yanayolenga kupatikana kwa chanjo na dawa ya ugonjwa huo. Shukrani,  Swahili,BBC