Skip to main content

Posts

Showing posts from March, 2014

HCPMetro DC,Ikishirikiana na ATC Metro,TANO Ladies na NesiWanguBlogspot yawaletea!!!!!!!

Wapendwa wasomaji wangu,ndugu,jamaa  na marafiki. Leo nimejaa furaha kubwa kupita maelezo, kwani Wataalam wa afya DMV wanatuleta huduma ya afya kwa wale wasiokuwa na bima ya afya. Huduma hii itatolewa kwa usawa bila kujali dini,rangi,umri,uraia au uchumi. Kama una rafiki, ndugu au  mzazi asiyekuwa na bima ya afya tunaomba mushiriki ili tuwe na jamii inayoshamiri na yenye afya njema. Zoezi hili litachukuwa hatua ya kuwaona wale watakaokuwa na hali pungufu ya afya njema walau mara moja kwa mwezi. MUNGU ANATUPENDA ZAIDI TUKIJILEA,TUKILELEANA NA  HATA TUNAPOMALIZA SAFARI .!                       Asanteni sana ,tunawapendeni na kuwajali.!

UVUTAJI SIGARA HAUNA TOFAUTI NA UNYWAJI SUMU WA TARATIBU !.

        MAPAFU YA  ASIYEVUTA SIGARA                                 NA                                          MVUTA SIGARA     Uvutaji wa sigara na mazingira yaliyokuwa na moshi wa sigara ( second hand smoke) hujulikana kwa  maafa yake ya husababisha magonjwa sugu ya mapafu yajulikanayo kama  ‘Chronic Obstructive Pulmonary Diseases” (COPD) yakiwemo pumu, kifua kikuu na …?(emphysema). Magonjwa haya uhashiriwa na upungufu wa umahiri wa ubadilishaji wa hewa katika mapafu; ugumu wa kutoa  hewa chafu ya carbon katika mapafu  na uchukuaji wa hewa oxygen. Hii hujitokeza pale mgonjwa anapojihisi ugumu wa kuvuta hewa hasa wakati wa shughuli au mazoezi. Mbali na magojwa sugu ya mapafu,uvutaji wa sigara watupelekea saratani za aina mabalimbali kama :- Saratani ya mapafu Saratani ya njia ya chakula (umio au esophagus)  Utumbo,  Njia ya kutolea uchafu mwilini, Ini,figo na njia ya mkojo  Kigosho, tumbo na  koromeo. Uvutaji wa sigara waweza kupunguza

JITAHIDI USHIRIKI UCHUNGUZI WA BURE WA SARATANI MBALI MBALI MWILINI.

Shukrani; TANO Ladies Face Book Page!.

BIMA YA AFYA YA BEI NAFUU (AFFORDABLE HEALTH COVERAGE)

HAKIKISHA UMEJIPATIA  BIMA YA AFYA YA BEI NAFUU KABLA YA  TAREHE  31/03 /2014 Ratiba ya mwezi wa tatu ni pamoja na kila Jumamosi, tarehe 8,15,22,29 kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni katika anuani zifuatazo:- Montgomery County Department of Health and Human Services;  8818 Georgia Avenue, Silver Spring 12900 Middlebrook Road, Germantown Suitland Community Center 5600 Regency Lane, District Heights, MD Prince George’s County Government at Temple Hills  4235 28th Avenue, Temple Hills Kwa maelezo zaidi bofya; www.capitalhealthconnection.org   au piga simu 240-773-8250.  (Msaada wa lugha tofauti utapatikana) Shukrani kwa niaba ya :- Montgomery County, MD  Capitalhealthconnection.org

MAJI NI UHAI !.

MAJI NI UHAI Kama picha hii inavyoashiria, ardhi bila maji hunyauka na kupasuka,kadhalika mmea bila maji hunyauka na kufa. "Asilimia 60% hadi 75%  ya mwili wa binadamu imetawaliwa na maji" ( Barry M. Popkin ) . Ijapokuwa kiwango cha maji hutofautina kutokana na umri au maumbile, mwili uliokosa  maji ni tishio kubwa kwa uhai. FAIDA ZA MAJI MWILINI Kurahisisha usagaji wa chakula Kupunguza hatari za kupata mawe kwenye figo Kupunguza maumivu ya arthritis hasa sehemu za viungo  Kupunguza kuugua na maumivu ya mara kwa mara hasa kwa wagojwa wa circle cell Kuondoa sumu mwilini au toxins Kurutubisha ngozi ya mwili  Kuwezesha kupata choo( normal bowel function) Kupunguza mwili DALILI ZA KUPUNGUKIWA MAJI MWILINI Ukosefu wa mkojo au mkojo ulio wa rangi nzito ya njano Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) mara kwa mara Kiu Kupasuka kwa midomo au midomo huwa mikavu Uchovu Maumivu ya kichwa Mapigo ya moyo yenye kishindo kikubwa na ya kas

SWALI; NI KIPI KIWANGO SAHIHI CHA SHINIKIZO LA DAMU ?.

                               JIBU:               Chati ifuatayo inamaelekezo sahihi kuhusu shinikizo la damu                               Shinikizo la damu lisilopata suluhishi  mapema hutupelekea;                            Shukrani; http://lindaikeji.blogspot.com/ www.shutterstock.com    http://www.highbloodpressureinfo.org/

ATHARI ZA UKOSEFU WA USINGIZI !.

UKOSEFU WA USINGIZI MWORORO WAWEZA KUKULETEA MADHARA YAFUATAYO ; Msongo wa mawazo (Depression) Ongezeko la mwili Upungufu wa msukumo wa tendo la ndoa Hasira Usahaulifu Ugumu wa ufanisi wa kazi ( poor concentration at work or school) Kuzeeka kwa ngozi kabla ya mda wake Ongezeko la ajali Kukuweka hatarini zaidi kupata magojwa ya moyo, shinikizo la damu,kisukari,stroke na hata kifo cha ghafla NAMNA YA KUONGEZA  USINGIZI MWORORO Weka ratiba maalum ya kwenda kulala na kuamka kila siku Pata mazoezi ya mwili walau dakika 30 mara 4 hadi 5 kwa wiki Epuka mlo mkubwa kabla ya kwenda kulala. Epuka caffaine na Pombe  mda unaokaribia saa za kulala Epuka sigara au nicotine. Hakikisha chumba kina mazingira ya ukimya na yasiyo na mwanga Shukrani, atlantablackstar.com ,http://sleepfoundation.org/ Institute of Medicine. Sleep Disorders and Sleep Deprivation.

NesiWangu blog kwenye siku ya kimataifa ya mwanamke duniani

Picha zote kwa hisani ya Swahilivilla blog Katika siku ya kimataifa ya wanawake duniani iliyofanyika Jumamosi ya Machi 8, 2014, blog ya NesiWangu ilipata fursa ya kuzungumza na wanawake na hadhira nzima kuhusu kazi za blogu kwa jamii. Maelezo Kutoka kwa NesiWangu kwa Mhe. Balozi Mulamula                                                  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nchi za Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mmula alijumuika nasi pamoja na  wanawake wengi toka majimbo mbalimbali wakieleza na  kuonyesha kazi zao na pia kutumia muda mfupi kuongea na wananchi waliohudhuria kuhusu kazi hizo.                                      Maadhimisho hayo yaliandaliwa na Tano Ladies          yalifanyika katika ukumbu wa Hampton Inn uliopo College Park jimbo la Maryland Haya ni maelezo yangu kwenye sherehe hiyo . Shukrani;  Jamii and Media Group Production

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI (CERVICAL CANCER)

Saratani ya Shingo ya Kizazi (cervical cancer)yasemekana kuwa yaongoza kwa kusababisha vifo vya  wanawake nchini Tanzania .  Kati ya wanawake 6,210 waliopata nafasi ya kugundulika kwa ugojwa huu 4,355 wasemekana kufariki dunia.   (Imaworldhealth, 2010) Saratani ya shingo ya kizazi ni ugonjwa ambao hutokana na mabadiliko ya mfumo wa  chembe zilizoko  katika shingo ya kizazi, kubadilika zikishamiri na kuzaliana kwa kasi kinyume na mpangilio wa kimaumbile na hivyo kupelekea ongezeko la upatikanaji wa saratani. NINI KISABABISHACHO SARATANI YA SHINGO YA UZAZI ? Utafiti wa kisayansi umeafiki kwamba 99%  ya saratani za shingo ya uzazi hutokana na maambukizi ya virusi vya ' Human Papillomavirus' (HPV). Virusi hivi vilivyoko katika jamii ya papilloma vina aina zaidi ya 100,ambazo baadhi yake huambukizwa kwa njia ya  kujamiana. BAADHI YA MAMBO YANAYOONGEZA  HATARI  ZA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI? Kushiriki tendo ndoa katika  umr