Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2014

UKITUNZA MIFUPA UTASAIDIKA UZEENI !

Osteoporosis ni ugojwa sugu  wa  mwili kujitafunia virutubisho vilivyo kwenye mifupa na kuvitumia kwa mahitaji  yake.Hii husababisha  upungua wa umahiri wa  mifupa(bone density)  kuifanya iwe hafifu na  kumegeka. Ugojwa huu huitwa  “ silent disease’ kwani mara nyingi hujulikana tu  pale mtu anapoanguka na kuvunjika (kwa urahisi sana au kupata   fructure )   tofauti na mtu asiye na tatizo hili.  UNDANI MDOGO KUHUSU  OSTEOPEROSIS                                                                                                                       Mifupa ya mwili kwa wakati wote huwa  na mabadiliko ya  kujingeka, kujiimarisha   na kujirepea (bone remodeling) kwa kupitia  mzunguko maalaum wa kusagika (osteoclast)  ambapo hutoa madini yake ya calcium  katika mzunguko wa damu. Osteoperosis na upungufu wa umahiri wa mifupa (low bone mass)hutokea pale ambapo usagikaji wa mifupa (Osteoclast) uko juu zaidi ya  ujengekaji wa mifupa (Osteoblast). Binadamu hufikia kilele cha ujenzi  wa m

TATIZO LA ALLERGY LAWEZA TISHIA USALAMA.

Mchezaji wa Cinema Will Smith katika movie ya Hitch akionyesha ukweli wa allergy za vyakula Wengi wenye allergy za vyakula hasa karanga hugundua hata pale  wanaposikia harufu kwani macho yaanza kutoa machozi au wanapiga chafya. Mbaya zaidi ni pale  wanapotumia  vyakula vyenye mchanganyiko wa karanga kwani hali zao huwa ni mbaya na uhitaji matibabu ya haraka. Allergy ya chakula kilichoingia mwilini  huweka mwili  mzima katika  hatari kwani mwili mzima huingia katika kujibu mashambulizi ya kile kisichokubalika mwilini kwa dalili zifuatazo; BAADHI YA  DALILI ZA (ANAPHYLAXIS) ALLERGY MBAYA INAYOHUSIHA  MWILI MZIMA NA KUHATARISHA MAISHA; Vipele vya harara mwilini,kuwashwa,kuwa mwekundu Mafua ya ghafla ya maji Kuvimba kwa mwili Kupumua kwa shida na kukohoa Ugumu wa kuongea Kuumwa tumbo Kizunguzungu Kuhisi kitu kibaya kitakotea au wasiwasi mkubwa Kuvimba mwili,nje na ndani na hasa njia ya hewa na kusababisha kushidwa kupumua Ongezeko

HUDUMA YA HARAKA KWA UPUNGUFU WA SUKARI MWILINI (HYPOGLYCEMIA)

0 Ubongo wa binadamu unahitaji sukari kwa mda wote ili kuwa na nguvu ya kufanya kazi . Sukari hii yategemewa kutoka kwenye mzunguko wa damu kwani ubongo hauna uwezo wa kuzalisha au kuhifadhi sukari ya kutosha  matumizi ya  baadaye. Kutokana na hitilafu ya kingosho(dysfunctional pancreas) wagowja wa kisukari huwa na hali ngumu ya kuweka sukari katika vipimo vinavyohitajikana hivyo mara nyingi  sukari huwa juu (Hyperglycemia) au chini  (Hypoglycemia) na huhitaji tiba. Hivyo basi ni muhimu sana kwa ndugu au rafiki wa karibu kujua machache ili kuwa msaada pale mpendwa wako anapojikuta katika hali ya kuishiwa sukari kwani  inahitaji huduma ya haraka kuokoa maisha. DALILI ZA UPUNGIFU WA SUKARI MWILINI (Hypoglycemia) Kipimo cha sukari  chini ya    70 mg/dL au 3.9 mmol/L   chaweza hatarisha maisha ya mpendwa wako  mwenye kisukari. ; Njaa kuumwa kwa kichwa Kutokwa kwa jasho kutikisika kwa mwili Hasira Mwili au ngozi baridi na nyevu K