Skip to main content

.KUKABWA NA JINAMIZI A.K.A "SLEEP APNEA"

Je unahisi dalili zifuatazo?

  • Kukoroma  kwa sauti kubwa hata kusumbua  mwenzio
  • Uchovu unapoamka japo umelala usiku kucha 
  • Maumivu ya kichwa unapoamka
  • Mdomo au koo kuwa kavu unapoamka 
  • Kusimamisha pumzi usingizini
  • Kuzinduka mara kwa mara usingizini ukitafuta pumzi, kukabwa au kukohoa.?
  • Usingizi wa mara kwa mara unaoingiliana na kazi,masomo,usalama barabarini.
  • Ugumu wa kukaa macho kwa mda wakati wa vikao, kujisomea au kutazama TV

Dalili kubwa ya Sleep Apnea ni kukoroma kwa sauti ya kuzidia na hata kukera mwezio






 Harvard School of Medicine  yatoa ufafanuzi zaidi kuhusu ‘Kukabwa na Jinamizi’ a.k.a 'Obstructive Sleep Apnea'  (Ukosefu wa pumzi Usingizini)

Video courtesy of Harvard School of Medicine

UFAFANUZI NA ATHARI ZA UKOSEFU WA PUMZI USINGIZINI

Binadamu yeyote anaposinzia mwili hulegea na viungo hupumzika.Ulegevu huo hutokea sehemu mbalimbali za mwili na hasa misuli ambayo kazi yake kubwa ni ushikiliaji wa njia mbalimbali mwilini kama njia ya hewa. Hivyo basi, tunaposinzia mwili na misuli hulegea na kupunguza umahiri wa kazi na hivyo kuathiri  njia ya hewa kwa kuifanya iwe nyembamba( narrow airway).


Njia hiyo yaathirika zaidi endapo kuna  hitilafu ya kimaumbile kama kilimi,ulimi au tezi kubwa.Unono wa mwili au mnene unaoongeza nyama za shingo na kwa pamoja kulalia njia ya hewa na kufanya njia hiyo izidi kuwa ndogo,yenye kizuizi kwa hewa kupenya kwa urahisi.


NINI KINACHOSABABISHA KUKOROMA ?
Sauti ya kukoroma (snore) uhashiria jitihada za pumzi kupenya kwenye njia nyembamba na yenye kizuizi.(Obstruction)

ATHARI ZA UKOSEFU WA PUMZI USINGIZINI

"Pumzi inaposhidwa kupenya, hupelekea upungufu wa hewa ya oxygen  mwilini.Upungufu huo hugundulika haraka sana katika ubongo kwani ili ubongo uweze kuishi na kufanya kazi vizuri unahitaji oxygen isiyopungua asilimia 95 hadi 100%” (Potter & Perry,2009).
Mazingira ya oxygen pungufu usingizini, yapelekea ubongo kuingia katika jukumu la kuzindua mwili ambapo mgojwa aweza kuzinduka kwa kurusha miguu,mwili,kukohoa na kuvuta pumzi ya haraka na yenye kutoa sauti kubwa ya kukoroma.
Kitendo hicho cha ubongo  kuamsha mwili kutoka usingizini, kinarudisha mwako katika wa misuli ya mwili (muslce tone) na hivyo kurejesha misuli ya njia ya hewa katika hali inayotoa nasafi ya kutosha kwa hewa kupenya. Lakini,pale mgojwa anataposinzia tena, misuli hulegea na hivyo njia ya hewa kuathirika tena na mzunguko wa kuamka na kutafuta pumzi mara kwa mara huendelea usiku kucha.Zoezi hili humwacha mgonjwa na pumziko hafifu sana na mara nyingi hujihisi mchovu sana hasa panapokucha.



ATHARI ZA UKOSEFU WA  PUMZI USINGIZINI




Ubongo unapopungukiwa na oxygen usingizini huwa ni chanzo cha wangojwa wengi kulalamika kuumwa kwa kichwa wanapoamka na pamoja na upungufu wa kumbukumbu ambao unasababishwa na kifo kwa chembechembe za ubongo ambazo hutokana na upungufu wa oxygen ”(http://news.health.com/sleep-apnea-damage-brain-memory)
 Upungufu wa hewa ya oxygen mwilini hulazimisha moyo kuongeza nguvu na kasi ili kufidia upungufu wa hewa ya oxygen mwilini. Moyo unaofanya kazi kupita kiwango chake kwa mda mrefu huleta udhoofu katika mishipa yake na kupanuka (enlarge heart) 

Bila tiba Sleep Apnea hupelekea matatizo mengi ya afya kama;
  • Shinikizo la damu
  • Kisukari,(Diabetes)

  • Stroke,

  • Magojwa ya moyo
  • Hasira

  • Msongo wa mawazo (Depression)

  • Upungufu wa umakini shuleni,kazini, hata barabarani

  • Uchovu wa mwlini na usingizi wa mara kwa mara

  • Upungufu wa msukumo wa tendo la ndoa

  • Afya duni kiujumla na kudhoofisha utendaji kwa ujumla


BAADHI YA SABABU ZINAZOONGEZA  ULEGEVU WA MISULI MWILINI ;

Umri (misuli ya mwili hupunguza umahiri  kadiri umri unavyosogea), Utumiaji wa pombe,ukosefu wa mazoezi na baadhi ya dawa na hasa za usingizi.

BAADHI YA TIBA ZITUMIKAZO ;




    Continous Positive Air Pressure (CPAP) Hii ni tiba endelevu (therapy) inayotumia mashine kusukuma hewa kupitia njia ya hewa pale tunaposinzia.Hewa hii huwa na msukumo wa nguvu kushinda kipingamizi kinachoziba njia hiyo na hivyo huruhusu  mgonjwa kupata pumzi barabara na hewa ya  kutosha kwa wakati asinziapo. Wengi waliotumia tiba hii (CPAP machine) huripoti mabadiliko makubwa kwani  huondokana na matatizo ya kusinzia mara kwa mara,uchovu na kupata ongezeko kubwa la umakini katika kazi, shule, barabani na hata  mabadiliko ya mahusiano hasa kwa wanandoa .
      FULL FACE MASK FOR MOUTH BREATHERS


NASAL CPAP MASK






 

Mouth Guard;
Tiba hii hutumika zaidi kwa wale wenye hali hiyo kwa kiwango kidogo.Ni budi kupata ushauri kutoka kwa Daktari wako kwani njia hii dhumuni lake ni kusogeza taya ya chini mbele ulalapo ili kufungua zaidi njia ya hewa.

Surgery;  Surgery option,ni ushauri wa hatua ya mwisho na pia itategemea na kinachosababisha hali hii kwako. Pata ushauri kutoka kwa wataalamu tofauti na jaribu njia nyingine kwanza. kwani nimeona wagonjwa ambao bado wana hali hii baada ya
surgery na wamenufaika kwa kutumia CPAP machine.

Weight Loss; Wengi wenye  hali hii kutokana na unono wa mwili wamerepot  nafuu kubwa sana, hasa baada ya kupunguza mwili. 

Epuka dawa za kulala na tumia dawa zote kwa makini na kwa kufuata maelezo ya daktari.
Epuka pombe walau masaa manne kabla ya kulala  kwani pombe inachangia kupunguza pumzi na kulegeza misuli ya mwili mara dufu.

Ushauri wa bure (Fuata ushauri wa mtaalamu wako wa afya)
Kwa wale wenye hali hii wakisubiri tiba waweza kupata nafuu kwa kulala upande(ubavu) au kuongeza mito ili kuruhusu njia ya hewa kufunguka zaidi, kupunguza dalili za kukoroma na kupata afueni mpaka hapo utakapotibiwa .

Shukrani ;
  • Harvard School of Medicine, TNO Staff , Drew Silverman
  • Notes Translations from , American Academy of Sleep Medicine, Darien ,IL 60561
  • Potter, P. A., & Perry, A. G. (2009). Fundamentals of nursing. St. Louis, Mo: Mosby Else
  • vier




  • NB, Kwa Ufahamu zaidi au Wataalamu  Contact us at Nesiwangublog@gmail.com


    Ushauri na ufafanuzi wa mtandao huu ni kwa ajili ya kuchangia upeo wa elimu afya. Maamuzi ya  afya yabaki mikononi  mwa mtu bisnafsi na  mtaalamu  wake. ,
    Asante sana.






    Comments

    Popular posts from this blog

    HUDUMA YA HARAKA KWA UPUNGUFU WA SUKARI MWILINI (HYPOGLYCEMIA)

    0 Ubongo wa binadamu unahitaji sukari kwa mda wote ili kuwa na nguvu ya kufanya kazi . Sukari hii yategemewa kutoka kwenye mzunguko wa damu kwani ubongo hauna uwezo wa kuzalisha au kuhifadhi sukari ya kutosha  matumizi ya  baadaye. Kutokana na hitilafu ya kingosho(dysfunctional pancreas) wagowja wa kisukari huwa na hali ngumu ya kuweka sukari katika vipimo vinavyohitajikana hivyo mara nyingi  sukari huwa juu (Hyperglycemia) au chini  (Hypoglycemia) na huhitaji tiba. Hivyo basi ni muhimu sana kwa ndugu au rafiki wa karibu kujua machache ili kuwa msaada pale mpendwa wako anapojikuta katika hali ya kuishiwa sukari kwani  inahitaji huduma ya haraka kuokoa maisha. DALILI ZA UPUNGIFU WA SUKARI MWILINI (Hypoglycemia) Kipimo cha sukari  chini ya    70 mg/dL au 3.9 mmol/L   chaweza hatarisha maisha ya mpendwa wako  mwenye kisukari. ; Njaa kuumwa kwa kichwa Kutokwa kwa jasho kutikisika kwa mwili Hasira Mwili au ngozi baridi na nyevu K

    UPUNGUFU WA POTASSIUM MWILINI, WAWEZA KUWA TISHIO KWA USALAMA WA MOYO !.

    NDIZI HUSIFIKA KWA UTAJIRI WAKE WA MADINI YA POTASSIUM Potassium ni moja  kati  ya madini muhimu ya chumvi chumvi mwilini.Ikisaidiana na chumvu chumvi nyingine kama Calcium, Magnesium na Sodium. Potassium ni muhimu sana kwenye usimamiaji wa kiwango sahihi cha maji mwilini, utendaji wa cell na kikubwa zaidi  uanzishaji wa mwendo ( conduction of  electricity) katika  misuli ya mwili yenye mwendo hiari na mwendo usio wa hiari. Hivyo, hupelekea mwamko katika mishipa ya moyo inayohusika na huwa ndio chanzo cha mapigo yanahusika na msukumo wa  damu mwilini. ( generates heart bit) Mahitaji ya Potassium kwa mtu mzima ni kati ya milligram zisizopungua 3,500 ml. kwa siku kutoka kwenye lishe. Ili mwili wa binadamu uweze kuendelea na utendaji wake, potassium iliyoko katika mzunguko wa damu yahitaji kuwa kati ya 3.5-5.0mEg/L. Kiwango hiki kikipopunguwa hutupelekea hali ijulikanayo kama; Hypokalemia au Upungufu wa Potassium katika damu. Vile vile kiwango hiki kinapozidia huitwa H

    MATATIZO YA THYROID KWA WANAWAKE .

    Thyroid ni mojawapo ya tezi zilizo mwilini zinazozalisha  homoni  (hormones) zake ndani ya mwili  na kutumika  kwenye mfumo wa  damu. Miongoni mwa kazi za homoni ya thyroid ni    kusimamia  utendaji wa shughuli  mwilini kama mwendo wa mapigo ya moyo,( heart rate),  usagaji wa chakula (digestion) ,mwendo na utendaji wa metaboli (metabolism)  na kusimamia matumizi ya calorie mwilini. Ili tezi ya thyroid iweze kufanya kazi yake ya uzalishaji homoni  huitaji madini ya Iodine.Madini  hayo hupatikana katika vyakula vya mimea vilivyotoka  kwenye udongo wenye virutubisho vya iodine ya kutosha, chumvi yenye iodine na vyakula vya baharini. Tezi ya thyroid inapozalisha homoni pungufu na kipimo kinachohitajika  husababisha  hali ijulikanayo kama   “Hypothyrodism”. Tezi hii  ikizalisha  homoni kupita kipimo kinachohitajika mwilini huitwa “Hyperthyrodism” LEO NINAPENDA KUZUNGUMZA NANYI KUHUSU UGONJWA WA HYPOTHYRODISM Hypothyrodism ni ugojwa ambao huwapata  wanawake zaidi kuliko