Mchezaji wa Cinema Will Smith katika movie ya Hitch akionyesha ukweli wa allergy za vyakula |
Wengi wenye allergy za vyakula hasa karanga hugundua hata pale wanaposikia harufu kwani macho yaanza kutoa machozi au wanapiga chafya. Mbaya zaidi ni pale wanapotumia vyakula vyenye mchanganyiko wa karanga kwani hali zao huwa ni mbaya na uhitaji matibabu ya haraka. Allergy ya chakula kilichoingia mwilini huweka mwili mzima katika hatari kwani mwili mzima huingia katika kujibu mashambulizi ya kile kisichokubalika mwilini kwa dalili zifuatazo;
BAADHI YA DALILI ZA (ANAPHYLAXIS) ALLERGY MBAYA INAYOHUSIHA
MWILI MZIMA NA KUHATARISHA MAISHA;
- Vipele vya harara mwilini,kuwashwa,kuwa mwekundu
- Mafua ya ghafla ya maji
- Kuvimba kwa mwili
- Kupumua kwa shida na kukohoa
- Ugumu wa kuongea
- Kuumwa tumbo
- Kizunguzungu
- Kuhisi kitu kibaya kitakotea au wasiwasi mkubwa
- Kuvimba mwili,nje na ndani na hasa njia ya hewa na kusababisha kushidwa kupumua
- Ongezeko la mapigo ya moyo
- Kushuka kwa pressure ya damu na kupoteza fahamu
- kichefuchefu,kutapika au kuarisha
Dalili hizi zisipokabiliwa kwa haraka huweka mwili kwenye hatari kubwa kwani mwili huvimba na hata kufunga njia ya hewa . Wengi wenye allergy mbaya wapatapo dalili hizi hutumia Epipen ambayo ni prescripiton kutoka kwa daktari inayosadia kupunguza na kuzuia shock ya mwili,kusimamia pressure ya damu na kupunguza kubanwa kwa njia ya hewa na kuruhusu mapafu kuruhusu pumzi pale ambapo allergy inaongeza uvimbe, kufunga njia hiyo na mwishowe kuweka mwili kwenye shock.
KWA WATOTO WENYE ALLERGY HII NI MUHIMU:
- Kumfundisha mtoto kuhusu allergy yake
- Kutomruhusu mtoto kulishwa au kula chakula usichokijua viungo vyake
- Kutembea na dawa zake kwa wakati wote
- Kujua namna ya kutumia dawa zake endapo anajikuta mbali na msaada wako
- Ni vyema wote kama familia mnaweka jitihada za kuepuka vyakula hivyo ndani ya nyumba na kufunza kila mmoja wenu namna ya kutoa huduma ya haraka kutokana na ushauri wa daktari.
BAADHI YA DAWA ZITUMIKAZO;
Benadrly na Epi-Penn -kwa maelezo kamilifu ongea na DAKTARI wako
Benadrly na Epi-Penn -kwa maelezo kamilifu ongea na DAKTARI wako
Shukrani;
http://gotmymoxie.blogspot.com
Comments
Post a Comment