NDIZI HUSIFIKA KWA UTAJIRI WAKE WA MADINI YA POTASSIUM |
Mahitaji ya Potassium kwa mtu mzima ni kati ya milligram zisizopungua 3,500 ml. kwa siku kutoka kwenye lishe. Ili mwili wa binadamu uweze kuendelea na utendaji wake, potassium iliyoko katika mzunguko wa damu yahitaji kuwa kati ya 3.5-5.0mEg/L. Kiwango hiki kikipopunguwa hutupelekea hali ijulikanayo kama;
Hypokalemia au Upungufu wa Potassium katika damu.Vile vile kiwango hiki kinapozidia huitwa Hyperkalemia au ongezeko la potassium katika damu.
Kiwango cha potassium kikizidi mwilini au kupunguwa ni hatari kwa usalama kwani huleta hitilafu katika mapigo na utendaji wa moyo na hivyo huhitaji maangalizi ya haraka.
Hypokalemia au Upungufu wa Potassium katika damu.Vile vile kiwango hiki kinapozidia huitwa Hyperkalemia au ongezeko la potassium katika damu.
Kiwango cha potassium kikizidi mwilini au kupunguwa ni hatari kwa usalama kwani huleta hitilafu katika mapigo na utendaji wa moyo na hivyo huhitaji maangalizi ya haraka.
Ni kinachoweza sababisha Upungufu wa Pottasium Mwilini ? ( Hypokalemia)
Hali hii huweza tokea pale mwili unapopoteza chumvi chumvi mwilini hasa kwa njia zifuatazo;
- Kuharisha ,
- Kutapika,
- Kutokwa jasho kwa wingi kupita kiasi
- Baadhi ya dawa za magojwa ya moyo na shinikizo la damu hasa za kupunguza maji mwilini kupitia njia ya mkojo, kama Loop Diuretics
- Matumizi ya kuzidia ya dawa au mitishamba ya kusaidia upatikanaji wa haja ( laxatives)
Dalili za Upungufu wa Potassium mwilini
- Kuumwa kwa misuli na kuhisi uchovu wa misuli (muscle cramps and weakness)
- Uchovu
- Kuvurugika kwa tumbo
- Mapigo ya moyo yenye hitilafu katika vipimo
- Upungufu wa chumvi mwilini
- Usingizi wa mara kwa mara
- Hasira
- Uhafifu wa utendaji wa figo
- Upungufu wa umahiri wa moyo
- Kupungukiwa na kumbukumbu
- Na hata kifo pale kiwango kinapokuwa chini sana kwani moyo hushidwa kuendeleza mapigo sahihi.
Ongezeko la ziada la Potassium mwilini (Hyperkalemia)
Hali hii husababisha mapigo ya moyo yenye hitilafu na ni hatari kwa maisha na huweza sababishwa na ;
- Dawa za magojwa ya moyo zilizopo kwenye kundi la ACE inhibitor na Potassium Sparing Diuretics
- Maambukizi
- Hitilafu katika utendaji wa figo
BAADHI YA VYAKULA VYENYE MADINI YA POTASSIUM
Na vingine vingi ……………..
http://umm.edu/health/medical/altmed/supplement/potassium
Potter, P.A. & Perry, A.G. (2009)
Potter, P.A. & Perry, A.G. (2009)
Comments
Post a Comment