Ripoti nyingi za wanasayansi zinaonyesha kwamba tatizo la upungufu wa damu mwilini ni tatizo linalosumbuwa zaidi jamii ya watu weusi. Tatizo hili lijulikanalo kwa jina la Anemia, husababishwa na upungufu wa iron au madini ya chuma mwilini yanayohusika katika utengenezaji wa chembechembe nyekundu za damu ( hemoglobin)
Kazi kubwa ya chembechembe hizi mwilini ni kusafirisha hewa ya Oxygen kutoka kwenye mapafu kuelekea kwenye tishu au sehemu mbali mbali za mwilini. Hivyo upungufu wa chembechembe nyekundu za dam mwilini hutupelekea uhafifu wa mgao wa oxygen kwenye damu na hivyo kuulazimisha moyo kufanya kazi kwa nguvu zaidi ili kufikisha oxygen katika viungo mbali mbali. Hali hii hupelekea moyo kuongeza kasi ya mapigo japo mgao wa damu bado ni hafifu; hali hii hutuacha na hisia za kuishiwa pumzi na hata kupelekea maumivu ya kifua hasa wakati wa zoezi kama kutembea,kupanda ngazi nk. uchovu wa mwili, maumivu ya kichwa, kizunguzungu, kichefuchefu na mengine mengi.
Kazi ingine ya chembe chembe nyekundu za damu mwilini ni kusafirisha hewa ya Carbon kutoka mwilini kuelekea kwenye mapafu ambapo hutolewa nje tunapopumua.
BAADHI YA SABABU ZINAZOSABABISHA ANEMIA
- Hitilafu katika jenetiki (mfano ugojwa wa sickle cell anemia)
- kupoteza damu nyingi mwilini,
- magonjwa ya uboho (bone marrow diseases)
- Ukosefu wa vyakula vyenye madini ya iron
- Utumiaji sugu wa pombe (Alcoholism)
- Hitiliafu ya mfumo wa chakula inayozuia kufozwa kwa virutubisho
Hali hii hujitokeza zadi kwa wanawake kwa ujumla hasa wajaa wazito, watoto,na wasichana kati ya miaka 11 hadi 19 (kundi hili hujulikana kwa uhafifu wa mlo kamilifu japo wanapoteza damu nyingi katika siku za mwezi) Wakifwatiwa na wazee kwani mfumo wa chakula hupunguza umahiri uzeeni na hivyo kuvyonza virutubisho pungufu zaidi ya mahitaji
BAADHI ya DALILI ZA UPUNGUFU WA MADINI YA CHUMA( IRON DEFICIENCY ) ANEMIA KWA WATU WAZIMA
- Uchovu usioisha (chronic fatique syndrome)
- Kuhisi kama unatobolewa na visindano kwenye miguu au vidole au ganzi (tingling)
- Udhaifu mwilini
- Kuishiwa pumzi katika shughuli ya kawaida kama kutembea ( Shortness of breath)
- Maumivu ya kifua (hasa wakati wa kutembea au kupanda ngazi )
- Kuumwa kichwa
- Kizunguzungu hasa unaposimama ghafla (orthostatic hypotension)
- Maambukizi ya mara kwa mara
- Kucha hafifu na zenye kuvunjika mara kwa mara
- Ubaridi wa mikono, miguu pamoja na kuhisi ganzi
- Mapigo ya moyo ya haraka haraka na hata yenye hitilafu
- Hamu ya kula vitu visivyo chakula kama udongo,chaki,mchele au unga mbichi. Hali hii hujulikana kisayansi kwa jina la “ PICA”
- Ongezeko la weupe wa macho
DALILI ZA ANEMIA KWA WATOTO WADOGO
- Kupoteza hamu ya chakula
- Dalili za kuzubaa au kuzorota katika utendaji,kama kutembea,kutambaa au kucheza
- Mahangaiko na hasira au (irritability)
- Ongezeko la weupe wa macho au kucha
- Mapigo ya moyo ya harakaharaka na hata yenye hitilafu
MAHITAJI YA IRON KWA WATOTO
- Mtoto mchanga hupata kiwango cha Iron kinachohitajika kutoka kwa maziwa ya mama. Mama hushauriwa kuendelea na Prenatal vitamins ili kukidhi mahitaji haya. Kwa upande wa mtoto anayetumia fomula ,hushauriwa kutumia fomula iliyorutubishwa na iron au (iron fortified formula)
- Mtoto anapofikia umri wa miezi 4-6 huwa tayari kuanza uji au ceral laini,Hivyo umri huu hadi mwaka mmoja twashahuriwa kutumia cereal iliyorutubishwa na iron ili kukidhi ongezeko la majitaji ya mwili pamoja na maziwa ya mama au fomula iliyorutubishwa na iron
- Mwaka 1 - 3 (Toddler) 7 mg za iron kwa siku
- Miaka 4 -8 10 mg za iron kwa siku
- Miaka 9-13 8 mg za iron kwa siku
- 13 - 19 ni umri wa kuwa makini sana kwani mahitaji huongezeka kwa watoto wa kike hadi 15 mg. kutokana na upotezaji wa damu wakati wa mwezi.
- Yashauriwa kutumia vyakula vya makundi yote kwa kiwango sahihi; kwani baadhi ya virutubisho kama vitamin C ni muhimu sana na huwezesha ufyozwaji wa virutubisho vya iron mwilini.
BAADHI YA VYAKULA VYENYE MADINI YA IRON
|
SAMAKI , MAYAI NA MAHARAGE |
MAINI |
BAADHI YA MBEGU NA NUTS |
TAHADHARI
Iron yawezapatikana katika mfumo wa vidonge vya nyongeza( suppliments)
Chukuwa tahadhari kubwa kwani iron ikizidia mwilini huwa ni sumu (toxic) na hivyo huwezasababisha kifo. Hakikisha umeongea na daktari wako kabla ya kutimia vidonge vya iron au dawa kwa ujumla.
Ni vyema kuzingatia vyakula vyenye virutubisho husika na pale inapolazimika tu, chini ya mwongozo wa daktari ndio kutumia dawa.
NB.Hifadhi vidonge vya iron (na dawa zote ) mbali na upeo wa mazingira ya watoto kwani rangi yake vyekundu uwavutia watoto wakifikiri ni pipi na kuhatarisha maisha.
Shukrani;
Ignatavicius, D.D. & Workman, M.L. (2010). Medical-Surgical Nursing: Patient-Centered Collaborative Care (6th ed.).
IMAGES;
Comments
Post a Comment