Shinikizo la damu hujullikana kama 'Silent Killer' kwani ni wengi wenye tatizo hili na huishi nalo hata miaka paasipo kulitambua. Shinikizo la damu hutuweka katika hatari za kiharusi (stroke), mshituko na hata kushidwa kwa moyo (heart attack and/or heart failure), upofu wa macho, pamoja na kushindwa kwa figo ambayo kazi yake kubwa ni kuchuja uchafu mwilini.
Ili kugundua tatizo la shinikizo la damu mapema, ni budi kupata kipimo na kujenga tabia ya kujichunguza mara kwa mara . Uchunguzi na ufumbuzi wa mapema husaidia kupunguza madhara yatokanayo na shinikizo la damu.
Baadhi ya dalili chache pale tatizo hili linapozidia ni pamoja na;
- maumivu ya kichwa,
- kizunguzungu,
- kichefuchefu,
- uhafifu wa kuona,
- kupoteza uwezo wa kutambua na hata kuzimia.
VIJISHIPA VIDOGO KATIKA UBONGO VILIVYOPASUKA NA KUVUJA DAMU.
TATIZO LITOKALO NA SHINIKIZO LA DAMU LILIKOSA UANGALIZI .
Vile vile, Mishipa ya damu huweza athirika kutokana na ongezeko la cholesterol mbaya mwilini (Low density lipoprotein au LDL) na kusababisha mkusanyiko wa uchafu ujulikanao kama Plaque; mkusanyiko wa mafuta, chembe za damu na uchafu katika kuta za mishipa ya damu. Uchafu huu wenye mnato mzito, hugandamana na kuta za mishipa ya damu na kufanya kuta hizo kuwa nono, na ngumu hali ijulikanayo kama Atherosclerosis. Jambo hili husababisha njia ya damu kupunguza umahiri kwa kuwa nyembamba kinyume na maumbile, kupenyeka kwa shida, ngumu na isiyotanuka na kunywea kama kawaida ili kukabiliana na kipondo cha mzunguko wa damu, kuziba kabisa na kutoruhusu damu kupenya, hali ijulikanayo kama Ischemic Stroke
Njia hafifu ya mishipa ya damu, hupelekea damu kupenya kwa shida na hivyo kuhitaji msukumo mkubwa na wenye nguvu zaidi, hali hii hulazimu moyo kuongeza nguvu ya utendaji na kasi ili kutimiza jukumu la msukumo na mzunguko wa damu
Ongezeko hilo la utendaji wa moyo likiendelea kwa muda mrefu, hudhoofisha misuli ya moyo, kuifanya itanuke, ilegee na kupunguza umahiri wake. Hali hii yaweza pelekea msukumo hafifu wa damu, kushindwa kwa moyo au heart failure.
Vile vile ongezeke la kipondo cha mzunguko wa damu katika mishipa laweza sababisha vijishipa vidogo dogo kupasuka na kuchuruzika damu na kuleta majeraha. Kama ilivyokuwa kawaida kwa mwili kukarabati majereha yake, kwa haraka sana chembe za damu na madini hujikusanya katika eneo lililoathirika na kutoa mvuto zaidi kwa cholesterol mbaya (LDL) kugandamana pamoja namabaki ya calcium katika jeraha na kusababisha uwepo wa kovu. Kovu katika mshipa wa damu hupunguza umahiri wa mishipa(flexibility) kuifanya migumu na isiyopenyeka kwa urahisi na kudhoofisha usafirishaji wa damu.
Picha hizi zaashiria mishipa iliyogandamana kwa mkusanyiko (plaque) cholesterol mbaya na uchafu wa chembe nyingine mwilini,migumu na yenye nafasi ndogo kwa damu kupenya. (Atheroslcerosis).
Plaque;
Tatizo la uchafu (plaque) unaogandamana na ukuta wa mishipa ya damu ni uwezo wake wa kumegeka kwa ghafla au wakati wowote na kusafiri katika mishipa ya damu. Uchafu huu huwa ni kizuizi kwani waweza kukwama kwenye njia inayosafirisha damu sehemu mbali mbali mwilini.
Hatari zaidi ni pale uchafu huu unapokwama kwenye mshipa usafirisha damu kwenye ubongo kwani hupunguza mgao wa damu inayokwenda kwenye ubongo au kuikatiza kwa ghafla na kusababisha ukosefu wa damu safi ya oxygen, na virutubisho katika ubongo. Hali hii na kutuweka katikahatari za stroke (Ischemic Stroke ).
Maafa ya mishipa iliyo na uchafu sehemu za moyo hutoa maumivu makali sehemu ya moyo pale mgao wa damu unapokuwa hafifu (Angina) na shambulizi la moyo au Heart Attack pale mgao wa damu unapokosekana kabisa. Kwani mishipa ya moyo inihitaji damu yenye kugawa oxygen na virutubisho muda wote ili kuweza fanya kazi yake vizuri.
Kwa upande wa mishipa inayosafirisha damu sehemu za miguu, ikiwa na kizuizi au (plaque) maumivu ya miguu huwa makali baada ya kutembea kwa mda mfupi. Hali hii hujitokeza pale mishipa inaposhidwa kupitisha damu yenye oxygen ya kutosha inayoendana na ongezeko la uhitaji wa damu safi ya oxygen, kutokana na zoezi. Na mara nyingi mgojwa hujihisi nafuu pale anapopumzika au kuacha matembezi. Pia hushauriwa kuninginiza miguu pembeni ya kitanda (dangle the feet) ili kurahisisha upenyaji wa damu yenye oxygen. Hali hii hujulikana kama (Peripheral Artery Disease)
SHINIKIZO LA DAMU LAWEZA SABABISHWA NA YAFUTAYO;
- Umri
- Ongezeko la cholesterol mbaya mwilini
- Diet ya vyakula vya mafuta,nyama nyekundu,chumvi au vyakula hafifu (processed foods na sukari nyingi)
- Hasili ya rangi takwimu zaonyesha weusi ni wengi kuliko wazungu
- Historia ya shinikizo la damu kifamilia
- Aina tofauti za dawa
- Kisukari
- Gout
- Magojwa ya figo
- Uvutaji wa sigara au tobacco.
- Ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi au Potassium kidogo.
- Ukosefu wa mazoezi ya mwili .
- Unene wa mwili.
- Utumiaji wa pombe kupita kiasi (>2/siku, kwa mme au >1/siku kwa mke)
KINGA AU TIBA
Wengi tunakubali kwamba kinga ni bora kuliko tiba kwani mti haunyauki siku moja, huwanza na tawi hatimaye mti huporomoka. Mbali na dawa za shinikizo la damu, hatuna budi kubadili mfumo wa maisha kama;
- kupunguza chumvi, mafuta,sukari au processed foods.
- Acha uvutaji wa sigara,
- Punguza pombe
- Punguza uzito wa mwili.
- Fanya mazoezi ya mwili walau mara 4 kwa wiki
- Ongeza mboga,matunda na vyakula asilia (ambavyo havijakobolewa na sio vya makopo)
- Epuka nyama nyekundu
Shukrani;
http://www.cdc.gov/bloodpressure/
http://www.cdc.gov/stroke/types_of_stroke.htm
http://www.nhlbi.nih.gov/health/health-topics/topics/atherosclerosis
http://watchlearnlive.heart.org/CVML_Player.php?moduleSelect=hemstrh
Comments
Post a Comment