MAJI NI UHAI
Kama picha hii inavyoashiria, ardhi bila maji hunyauka na kupasuka,kadhalika mmea bila maji hunyauka na kufa. "Asilimia 60% hadi 75% ya mwili wa binadamu imetawaliwa na maji" (Barry M. Popkin). Ijapokuwa kiwango cha maji hutofautina kutokana na umri au maumbile, mwili uliokosa maji ni tishio kubwa kwa uhai.
FAIDA ZA MAJI MWILINI
- Kurahisisha usagaji wa chakula
- Kupunguza hatari za kupata mawe kwenye figo
- Kupunguza maumivu ya arthritis hasa sehemu za viungo
- Kupunguza kuugua na maumivu ya mara kwa mara hasa kwa wagojwa wa circle cell
- Kuondoa sumu mwilini au toxins
- Kurutubisha ngozi ya mwili
- Kuwezesha kupata choo( normal bowel function)
- Kupunguza mwili
DALILI ZA KUPUNGUKIWA MAJI MWILINI
- Ukosefu wa mkojo au mkojo ulio wa rangi nzito ya njano
- Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) mara kwa mara
- Kiu
- Kupasuka kwa midomo au midomo huwa mikavu
- Uchovu
- Maumivu ya kichwa
- Mapigo ya moyo yenye kishindo kikubwa na ya kasi
- Kizunguzungu
- Mzubao
- kuchanganyikiwa, na hasa kwa wazee
- Kupoteza fahamu
MAMBO YANAYOWEZA KUBABISHA KUPOTEZA MAJI MWILINI
- Kuharisha
- Kutapika
- Homa kali
- Pombe
- Kutoka jasho
- Kisukari
- Kutokunywa maji ya kutosha
- Baadhi ya dawa
KUNDI LINALOATHIRIKA ZAIDI
- Watoto
- Wazee
- Wagojwa wa kisukari,alzheimer na mengineyo
NI WAKATI GANI KUWAHI KWA DAKTARI ?
- Mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 0 - 3
- Kutapika au kuharisha uchafu wa rangi nyeusi au damu
- Hali hii inapoambatana na homa
- Mgojwa anapopoteza maji zaidi ya anayoweza kunywa.
- Kutopata nafuu kwa mtu mzima kwa siku mbili hadi tatu na kwa mtoto asiye pata nafuu kwa muda wa masaa 24
Shukrani
pictures
www.boloji.com http://
www.ncbi.nlm.nih.gov/
Ignatavicius, D.D. & Workman, M.L. (2010). Medical-Surgical Nursing: Patient-
Centered Collaborative Care (6th ed.).
www.ncbi.nlm.nih.gov/
Ignatavicius, D.D. & Workman, M.L. (2010). Medical-Surgical Nursing: Patient-
Centered Collaborative Care (6th ed.).
Comments
Post a Comment