Skip to main content

WAGONJWA WA MALARIA WAPIMWA KWA MACHO !.



9th November 2014
Print
Ukosefu wa vifaa tiba katika baadhi ya zahanati na vituo vya afya vya Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, umewalazimu wauguzi wa vituo hivyo kuwatibu wagonjwa wa malaria kwa kutumia uzoefu wa kuwaangalia.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika zahanati ya Mtepeche kata ya Kilimani Hewa, tarafa ya Nambambo na zahanati ya Kihuwe kata ya Naipingo, tarafa ya Naipanga wilaya ya Nachingwea, umebaini kuwepo kwa tatizo hilo.

Waganga wa zahanati hizo, walisema kukosekana kwa vipimo vya kupimia ugonjwa wa malaria kunawalazimu kutibia wagonjwa kwa kutumia uzoefu wa kuwaangalia kwa macho.

Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Mtepeche, Ibrahimu Mpini, alisema hutumia uzoefu kwa kumwaangalia mgonjwa kwa macho na kumpatia huduma.
Alisema njia hiyo ni hatari kwa kuwa unaweza kutoa dawa za malaria wakati mgonjwa ana tatizo hilo.

Alisema ukosefu wa vipimo ni changamoto katika utendaji kazi wao.
Hata hivyo, alisema wamekuwa wakiomba vifaa hivyo kwenye Bohari ya Madawa (MSD) lakini wanapata vichache ukilinganisha na mahitaji yao.

Alisema MSD huwapatia vifaa hivyo kila baada ya miezi mitatu na wakati mwingine havifiki muda uliopangwa.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Kihuwe, Rajabu Nassor, alisema  kituo chake kinapa idadi ndogo ya vifaa vya  kupimia malaria.

Alisema kutokana na uchache huo huwa vinaisha katika kipindi cha mwezi mmoja na nusu wakati MSD hupita kila baada ya miezi mitatu.

Nassor alisema wanachokiandika na kile kinachotolewa na MSD ni tofauti, hivyo kuna umuhimu wa jambo hilo kuangaliwa kwani kuwatibu wagonjwa kwa macho si jambo zuri kiafya.

Alisema zahanati yake inawatibia wagonjwa kutoka katika kata tano na vifaa hivyo vinapokwisha mapema inawalazimu kufanyakazi katika mazingira magumu.

Aliishauri serikali kuhakikisha zahanati hizo zinakuwa na vifaa muhimu ili wananchi hao wasipate usumbufu wa kupata huduma za afya.
SOURCE: NIPASHE JUMAPILI

Comments

Popular posts from this blog

HUDUMA YA HARAKA KWA UPUNGUFU WA SUKARI MWILINI (HYPOGLYCEMIA)

0 Ubongo wa binadamu unahitaji sukari kwa mda wote ili kuwa na nguvu ya kufanya kazi . Sukari hii yategemewa kutoka kwenye mzunguko wa damu kwani ubongo hauna uwezo wa kuzalisha au kuhifadhi sukari ya kutosha  matumizi ya  baadaye. Kutokana na hitilafu ya kingosho(dysfunctional pancreas) wagowja wa kisukari huwa na hali ngumu ya kuweka sukari katika vipimo vinavyohitajikana hivyo mara nyingi  sukari huwa juu (Hyperglycemia) au chini  (Hypoglycemia) na huhitaji tiba. Hivyo basi ni muhimu sana kwa ndugu au rafiki wa karibu kujua machache ili kuwa msaada pale mpendwa wako anapojikuta katika hali ya kuishiwa sukari kwani  inahitaji huduma ya haraka kuokoa maisha. DALILI ZA UPUNGIFU WA SUKARI MWILINI (Hypoglycemia) Kipimo cha sukari  chini ya    70 mg/dL au 3.9 mmol/L   chaweza hatarisha maisha ya mpendwa wako  mwenye kisukari. ; Njaa kuumwa kwa kichwa Kutokwa kwa jasho kutikisika kwa mwili Hasira Mwili au ngozi baridi na nyevu K

UPUNGUFU WA POTASSIUM MWILINI, WAWEZA KUWA TISHIO KWA USALAMA WA MOYO !.

NDIZI HUSIFIKA KWA UTAJIRI WAKE WA MADINI YA POTASSIUM Potassium ni moja  kati  ya madini muhimu ya chumvi chumvi mwilini.Ikisaidiana na chumvu chumvi nyingine kama Calcium, Magnesium na Sodium. Potassium ni muhimu sana kwenye usimamiaji wa kiwango sahihi cha maji mwilini, utendaji wa cell na kikubwa zaidi  uanzishaji wa mwendo ( conduction of  electricity) katika  misuli ya mwili yenye mwendo hiari na mwendo usio wa hiari. Hivyo, hupelekea mwamko katika mishipa ya moyo inayohusika na huwa ndio chanzo cha mapigo yanahusika na msukumo wa  damu mwilini. ( generates heart bit) Mahitaji ya Potassium kwa mtu mzima ni kati ya milligram zisizopungua 3,500 ml. kwa siku kutoka kwenye lishe. Ili mwili wa binadamu uweze kuendelea na utendaji wake, potassium iliyoko katika mzunguko wa damu yahitaji kuwa kati ya 3.5-5.0mEg/L. Kiwango hiki kikipopunguwa hutupelekea hali ijulikanayo kama; Hypokalemia au Upungufu wa Potassium katika damu. Vile vile kiwango hiki kinapozidia huitwa H

MATATIZO YA THYROID KWA WANAWAKE .

Thyroid ni mojawapo ya tezi zilizo mwilini zinazozalisha  homoni  (hormones) zake ndani ya mwili  na kutumika  kwenye mfumo wa  damu. Miongoni mwa kazi za homoni ya thyroid ni    kusimamia  utendaji wa shughuli  mwilini kama mwendo wa mapigo ya moyo,( heart rate),  usagaji wa chakula (digestion) ,mwendo na utendaji wa metaboli (metabolism)  na kusimamia matumizi ya calorie mwilini. Ili tezi ya thyroid iweze kufanya kazi yake ya uzalishaji homoni  huitaji madini ya Iodine.Madini  hayo hupatikana katika vyakula vya mimea vilivyotoka  kwenye udongo wenye virutubisho vya iodine ya kutosha, chumvi yenye iodine na vyakula vya baharini. Tezi ya thyroid inapozalisha homoni pungufu na kipimo kinachohitajika  husababisha  hali ijulikanayo kama   “Hypothyrodism”. Tezi hii  ikizalisha  homoni kupita kipimo kinachohitajika mwilini huitwa “Hyperthyrodism” LEO NINAPENDA KUZUNGUMZA NANYI KUHUSU UGONJWA WA HYPOTHYRODISM Hypothyrodism ni ugojwa ambao huwapata  wanawake zaidi kuliko