Skip to main content

MATATIZO YA THYROID KWA WANAWAKE .





Thyroid ni mojawapo ya tezi zilizo mwilini zinazozalisha  homoni  (hormones) zake ndani ya mwili  na kutumika  kwenye mfumo wa  damu. Miongoni mwa kazi za homoni ya thyroid ni    kusimamia  utendaji wa shughuli  mwilini kama mwendo wa mapigo ya moyo,( heart rate),  usagaji wa chakula (digestion) ,mwendo na utendaji wa metaboli (metabolism)  na kusimamia matumizi ya calorie mwilini.



Ili tezi ya thyroid iweze kufanya kazi yake ya uzalishaji homoni  huitaji madini ya Iodine.Madini  hayo hupatikana katika vyakula vya mimea vilivyotoka  kwenye udongo wenye virutubisho vya iodine ya kutosha, chumvi yenye iodine na vyakula vya baharini.
Tezi ya thyroid inapozalisha homoni pungufu na kipimo kinachohitajika  husababisha  hali ijulikanayo kama  “Hypothyrodism”. Tezi hii  ikizalisha  homoni kupita kipimo kinachohitajika mwilini huitwa “Hyperthyrodism”



LEO NINAPENDA KUZUNGUMZA NANYI KUHUSU UGONJWA WA HYPOTHYRODISM


Hypothyrodism ni ugojwa ambao huwapata  wanawake zaidi kuliko wanaume. Kama tulivyoona hapo juu hali hii hutokana na upungufu wa uzalishaji wa homoni za  thyroid  mwilini na vile vile  yaweza kutokea endapo  tezi ya thyroid imetolewa mwilini.

x-mas.jpg
Mimi nikiwa miongoni mwa watu waliotolewa tezi ya thyroid,kutokana na kugunduliwa kwa  chembechembe  za  saratani,nilijikuta nikisumbuliwa na  mabadiliko makubwa mwilini,kama vile ongezeko la  uzito wa mwili kutoka pound 200 hadi  260 lb, upotevu wa  kumbukumbu kiasi kwamba iliniwia vigumu kuendesha gari kutokana na kusahau njia na mahali  ninapotakiwa kwenda . Hali hii ilinipelekea ugumu wa kuelewa masomo na na kujikuta katika darasa la walemavu wa akili.Pia nilisumbuliwa na mapigo dhaifu  ya moyo, uchovu wa mwili na baridi wakati wote. Baada ya kuanza matibabu kwa kipindi cha miezi miwili nilishuhudia mabadiliko makubwa   ya mwili na akili. Nilimshukuru sana Mwenyezi  Mungu na huku  nikiendelea na dawa ambazo  itanibidi kuzitumia kwa maisha yote ili kufidia homoni ambazo zilikuwa zikizalishwa na tezi ya thyroid.






DALILI NYINGINE  ZA  HYPOTHYRODISM NI PAMOJA NA ;


  • Kuvimba kwa uso au (puffy face)  hasa chini ya macho
  • uhafifu wa utendaji wa metaboli mwilini.
  • Ongezeko la mwili na ugumu wa kupungua mwili mbali na jitihada
  • Upungufu wa mapigo ya moyo  < 60 bm
  • Uhafifu wa kumbukumbu
  • Hasira na mzongo wa mawazo ( depression)
  • Uchovu usiopungua hata kwa usingizi wa siku na usiku mzima
  • Uhafifu na umegekaji wa  kucha  
  • Kudhoofika kwa  nywele na kunyonyoka
  • Kuhisi baridi kwa haraka tofauti na wenzako walioko katika mazingira yako
  • Ukavu wa ngozi
  • Mabadiliko ya siku za mwezi,na kuzidia kwa damu katika siku za mwezi
  • Kuhadimika kwa haja kubwa( constipation)
  • Udhaifu wa  misuli na maumivu ya viungo
  • Ongezeko la cholesterol mbaya mwilini ( na chanzo cha shinikizo la damu)
  • Kukwaruza kwa sauti


Makala inayofwatia tutaangalia kuhusu ugojwa wa hyperthyrodism,dalili na madhara yake.



Shukrani;

.mayoclinic.org
Ignatavicius, D.D. & Workman, M.L. (2010). Medical-Surgical Nursing: Patient-Centered Collaborative Care (6th ed.).
 I


Comments

  1. Asante kwa somo Ila nilitaka kujua homoni hii ndo inasababisha goita

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

HUDUMA YA HARAKA KWA UPUNGUFU WA SUKARI MWILINI (HYPOGLYCEMIA)

0 Ubongo wa binadamu unahitaji sukari kwa mda wote ili kuwa na nguvu ya kufanya kazi . Sukari hii yategemewa kutoka kwenye mzunguko wa damu kwani ubongo hauna uwezo wa kuzalisha au kuhifadhi sukari ya kutosha  matumizi ya  baadaye. Kutokana na hitilafu ya kingosho(dysfunctional pancreas) wagowja wa kisukari huwa na hali ngumu ya kuweka sukari katika vipimo vinavyohitajikana hivyo mara nyingi  sukari huwa juu (Hyperglycemia) au chini  (Hypoglycemia) na huhitaji tiba. Hivyo basi ni muhimu sana kwa ndugu au rafiki wa karibu kujua machache ili kuwa msaada pale mpendwa wako anapojikuta katika hali ya kuishiwa sukari kwani  inahitaji huduma ya haraka kuokoa maisha. DALILI ZA UPUNGIFU WA SUKARI MWILINI (Hypoglycemia) Kipimo cha sukari  chini ya    70 mg/dL au 3.9 mmol/L   chaweza hatarisha maisha ya mpendwa wako  mwenye kisukari. ; Njaa kuumwa kwa kichwa Kutokwa kwa jasho kutikisika kwa mwili Hasira Mwili au ngozi baridi na nyevu K

UPUNGUFU WA POTASSIUM MWILINI, WAWEZA KUWA TISHIO KWA USALAMA WA MOYO !.

NDIZI HUSIFIKA KWA UTAJIRI WAKE WA MADINI YA POTASSIUM Potassium ni moja  kati  ya madini muhimu ya chumvi chumvi mwilini.Ikisaidiana na chumvu chumvi nyingine kama Calcium, Magnesium na Sodium. Potassium ni muhimu sana kwenye usimamiaji wa kiwango sahihi cha maji mwilini, utendaji wa cell na kikubwa zaidi  uanzishaji wa mwendo ( conduction of  electricity) katika  misuli ya mwili yenye mwendo hiari na mwendo usio wa hiari. Hivyo, hupelekea mwamko katika mishipa ya moyo inayohusika na huwa ndio chanzo cha mapigo yanahusika na msukumo wa  damu mwilini. ( generates heart bit) Mahitaji ya Potassium kwa mtu mzima ni kati ya milligram zisizopungua 3,500 ml. kwa siku kutoka kwenye lishe. Ili mwili wa binadamu uweze kuendelea na utendaji wake, potassium iliyoko katika mzunguko wa damu yahitaji kuwa kati ya 3.5-5.0mEg/L. Kiwango hiki kikipopunguwa hutupelekea hali ijulikanayo kama; Hypokalemia au Upungufu wa Potassium katika damu. Vile vile kiwango hiki kinapozidia huitwa H