Skip to main content

WIKI YA MANESI DUNIANI 2014 !.


Wiki hii   ni wiki rasmi ya kuwatambua Manesi wote duniani na kuwashukuru kwa mchango wao mkubwa katika jamii.Historia inatueleza kuwa  tarehe 12 mwezi wa tano,ikiwa siku ya mwisho ya kuadhimisha wiki ya Manesi,  ni siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa elimu ya juu ya unesi ‘Florence Nightingale’.

Mbali na mchango wake wa nadharia  katika kitengo cha malezi ya afya, Florence Nightingale alipewa jina la  “ The Lady with a lamp”  kwa umaarufu  wake wa kubeba taa ya chemli na kutembea usiku wa manane akishughulika na majeruhi wa vita vya Crimean mnamo mwaka 1853 – 1856.  


Leo pia, ni vyema tuwakumbuke watabibu wa jadi waliojitolea kutibu wagojwa kwa dawa za miti shamba na kutoa huduma ya ukunga.Japo hatuwatambui kwa majina, tunawapongeza kwa maarifa  na kazi nzuri waliofanya katika mazingira ya nyakati zile.


              
             KAZI YA MANESI NI KAZI YENYE CHANGAMOTO NYINGI;

 

Kutokana na uhaba wa manesi,wengi wao hulazimika kufanya kazi zaidi ya masaa kumi kwa siku.




Baadhi yao hulazimika kufanya kazi ktk mazingira hatarishi kutokana na ukosefu wa vitendea kazi na hivyo kuhatarisha afya zao.




Kazi ya Unesi ni WITO, Manesi wanatakiwa kuwa watu wenye Upendo, Ujasiri na Uvumilivu.


Timu ya NesiWangu inawatakia Heri na Baraka kwa kazi kubwa mnayofanya!.


Shukrani,Images
www.telegraph.co.uk
celsiusbloggen.se
ethnomed.org

Comments