Skip to main content

DRIVE-BY-SHOOTING!

Ni uhalifu  unaojumuisha gari lililo katika mwendo huku likimwaga risasi kwa raia. Uhalifu huu wa kinyama ni sugu katika baadhi ya maeneo, hasa kwa ndugu zetu wanaoshiriki katika Magenge ya vurugu au gangs. Mbaya zaidi, uhalifu huu hutokea ghafla na kuchukuwa maisha ya raia wasio na hatia.

Leo nilinusurika maisha nikiwa  katika eneo la 7th st. NW DC. Ilikuwa  mida ya saa kumi jioni ambapo shambulizi la ghafla la risasi zilizolia kama kifaru zilimiminika kutoka kwa gari isiyojulikana. Raia  walikimbia , wengine kujificha na hata kulala chini ili kuokoa maisha .

Baada ya dakika chache, kikosi kikubwa cha Police na Emergency Response 911, kiwasili  na kutoa huduma ya haraka kwa majeruhi. Taarifa ya baadaye  ya Fox 5 News, iliripoti kuwa kijana wa umri wa miaka 23,Mathew Shlonsky ambaye alikuwa mpita njia  alifariki dunia baada ya kufikishwa hospitalini.

 photo
                  Polisi wakiongea na raia ili kupata machache yatakayoweza saidia uchunguzi wao.
     
                                                Mtaa huu ulifungwa kwa mda wa masaa

                                         Baadhi ya Ambulance zilizofika katika eneo hilo

Magari yaliyokuwa katika eneo hilo yalijumuishwa katika tukio  la uhalifu na hivyo haikuruhusiwa kwa  mtu yeyote kufika kwenye gari yake au  kuichukuwa  hadi uchunguzi utakapomalizika. Japo malalamiko yalitoka kwa walionyimwa ruska ya kuchukuwa gari zao, wengi tulishukuru Mungu kwa kunusurika katika uhalifu huo wa kutisha.


Comments

Popular posts from this blog

HUDUMA YA HARAKA KWA UPUNGUFU WA SUKARI MWILINI (HYPOGLYCEMIA)

0 Ubongo wa binadamu unahitaji sukari kwa mda wote ili kuwa na nguvu ya kufanya kazi . Sukari hii yategemewa kutoka kwenye mzunguko wa damu kwani ubongo hauna uwezo wa kuzalisha au kuhifadhi sukari ya kutosha  matumizi ya  baadaye. Kutokana na hitilafu ya kingosho(dysfunctional pancreas) wagowja wa kisukari huwa na hali ngumu ya kuweka sukari katika vipimo vinavyohitajikana hivyo mara nyingi  sukari huwa juu (Hyperglycemia) au chini  (Hypoglycemia) na huhitaji tiba. Hivyo basi ni muhimu sana kwa ndugu au rafiki wa karibu kujua machache ili kuwa msaada pale mpendwa wako anapojikuta katika hali ya kuishiwa sukari kwani  inahitaji huduma ya haraka kuokoa maisha. DALILI ZA UPUNGIFU WA SUKARI MWILINI (Hypoglycemia) Kipimo cha sukari  chini ya    70 mg/dL au 3.9 mmol/L   chaweza hatarisha maisha ya mpendwa wako  mwenye kisukari. ; Njaa kuumwa kwa kichwa Kutokwa kwa jasho kutikisika kwa mwili...

UPUNGUFU WA POTASSIUM MWILINI, WAWEZA KUWA TISHIO KWA USALAMA WA MOYO !.

NDIZI HUSIFIKA KWA UTAJIRI WAKE WA MADINI YA POTASSIUM Potassium ni moja  kati  ya madini muhimu ya chumvi chumvi mwilini.Ikisaidiana na chumvu chumvi nyingine kama Calcium, Magnesium na Sodium. Potassium ni muhimu sana kwenye usimamiaji wa kiwango sahihi cha maji mwilini, utendaji wa cell na kikubwa zaidi  uanzishaji wa mwendo ( conduction of  electricity) katika  misuli ya mwili yenye mwendo hiari na mwendo usio wa hiari. Hivyo, hupelekea mwamko katika mishipa ya moyo inayohusika na huwa ndio chanzo cha mapigo yanahusika na msukumo wa  damu mwilini. ( generates heart bit) Mahitaji ya Potassium kwa mtu mzima ni kati ya milligram zisizopungua 3,500 ml. kwa siku kutoka kwenye lishe. Ili mwili wa binadamu uweze kuendelea na utendaji wake, potassium iliyoko katika mzunguko wa damu yahitaji kuwa kati ya 3.5-5.0mEg/L. Kiwango hiki kikipopunguwa hutupelekea hali ijulikanayo kama; Hypokalemia au Upungufu wa Potassium katika damu. Vile vile kiwang...

.KUKABWA NA JINAMIZI A.K.A "SLEEP APNEA"

Je unahisi dalili zifuatazo? Kukoroma  kwa sauti kubwa hata kusumbua  mwenzio Uchovu unapoamka japo umelala usiku kucha  Maumivu ya kichwa unapoamka Mdomo au koo kuwa kavu unapoamka  Kusimamisha pumzi usingizini Kuzinduka mara kwa mara usingizini ukitafuta pumzi, kukabwa au kukohoa.? Usingizi wa mara kwa mara unaoingiliana na kazi,masomo,usalama barabarini. Ugumu wa kukaa macho kwa mda wakati wa vikao, kujisomea au kutazama TV Dalili kubwa ya Sleep Apnea ni kukoroma kwa sauti ya kuzidia na hata kukera mwezio Pict.Courtesy  of http://always-healthy.com/sleep-apnea  Harvard School of Medicine  yatoa ufafanuzi zaidi kuhusu ‘Kukabwa na Jinamizi’ a.k.a 'Obstructive Sleep Apnea'  (Ukosefu wa pumzi Usingizini) Video courtesy of Harvard School of Medicine UFAFANUZI NA ATHARI ZA UKOSEFU WA PUMZI USINGIZINI Binadamu yeyote anaposinzia mwili hulegea na viungo hupumzika.Ulegevu...