Mazungumzo hayo yaligusia uhaba wa mashine za mionzi barani Africa na elimu endelevu kwa wahudumu wa saratani,jambo ambalo litawezekana kwa njia ya technolojia ya mawasilino na wanayasansi waliomo nje ya nchi. Nia ni kuboresha tiba na ufumbuzi wa changamoto za ugojwa wa saratani.
Majadiliano zaidi yalisisitizia umuhimu wa elimu ya utumiaji na utunzaji wa vifaa vya mionzi , upatikanaji wa vifaa katika vituo vya tiba ya saratani na mikakati ya kuelimisha jamii katika kufuata ushauri wa daktari ili kuepusha saratani za aina mbali mbali kama saratani ya shingo ya kizazi kwa kutoa chanjo kwa watoto wa kike kuanzia umri wa miaka 11 au 12, uvutaji wa sigara unaoongeza hatari za kupata saratani ya mapafu na nyinginezo.
Zaidi, walisisitiza umuhimu wa elimu afya kwa jamii na uchunguzi ili saratani kuweza kugundulika mapema kabla haijasambaa mwilini ikiwemo saratani ya tezi dume nk. .
Baadhi ya mashirika yenye vyombo vya mionzi yalishiriki na kutoa fafanuzi za mashine hizo wakisema kuwa, uuzaji wa mashine hizo utaambatana na elimu ya utumiaji na utunzaji,ujenzi wa chumba cheye uwezo wa kuhimili na kukabili mionzi pamoja na mkataba wa utengenezaji endapo inaharibika pasipo kusudi,uzembe au (neglegence nikinukuu).
Kwa ufahamu na elimu kwa jamii.
Comments
Post a Comment