Skip to main content

PATA ELIMU NA UCHUNGUZI WA AFYA YA TEZI DUME


KUPATA HUDUMA HII ENEO LA DMV KWA ASIYE NA BIMA YA AFYA CALL 240 672 1788

Tezi Dume, ni tezi yenye  umbile la donati iliyoko chini ya kibofu cha mkojo.Tezi hii huzungukwa na  mirija  ya mkojo na uhusika na urutubishaji wa mbegu za kiume (semen). Mabadiliko ya kimaumbile katika tezi ya prostate kama uvimbe,ongezeko la ukubwa au kushamiri kwa saratani, hupelekea hitilafu katika mfumo wa mkojo kwa kufinya mrija wa mkojo na hivyo mkojo kupita kwa shida,hukwama au kuacha mabaki.Hali hii humpelekea mgojwa uhitaji wa kutumia bafu mara kwa mara na hata kushindwa kuzia mkojo kuchuruzika. (Maumbile yote mwilini, yamekadiriwa kulingana na nafasi iliyoko, hivyo umbile linapoongezeka ukubwa, huleta hitilafu kwa mfumo mwingine).Saratani ya Prostate yaweza sambaa katika mifupa na tishu za jirani na hata kubana mishipa ya mgongo na kuleta maumivu sehemu za mgongo,hip na pelvic. 


Yashauriwa kufanya uchunguzi wa afya ya tezi dume kuanzia “miaka 45 kwa wale walio na historia ya saratani ya tezi dume katika familia, na kwa watu wa jamii ya Kiafrika”. Kwa ujumla uchunguzi wa tezi dume hushauriwa kwa wanaume wote kuanzia umri wa miaka 50. Kwa umri wa miaka 40, ni vyema kuzungumza na daktari wako ili kuongeza ufahamu na kuripoti mabadiliko yeyote.

BAADHI YA MATATIZO YA TEZI YA PROSTATE



Prostate Cancer ( Saratani ya tezi ya Prostate ) Saratani ya prostate ni saratani inayowashambulia wanaume hasa kuanzia umri wa miaka 50 na kuendelea.Saratani hii huweza kutibika kwa mionzi (radiation), upasuaji, chemotherapy au hormonal therapy.


  • Non-Bacterial Prostatitis;Uvimbe wa tezi ya Prostate usioambatana na maambukizi.
  • Bacterial prostatitis; uvimbe wa tezi ya prostate unaosababishwa na maambukizi (infection) na hutibika  kwa dawa za  Antibiotics  chini ya mwongozo wa daktari.

  • Enlarge Prostate  au Benign Prostate Hypertrophy (BPH) Ongezeko la ukubwa wa tezi ya prostate  Hali hii  hutokea kwa wanaume wengi hasa waliopita  umri wa miaka 50 na kundelea na huwa chanzo cha kusababisha hitilafu katika mfumo mkojo. Ongezeko la size ya umbile la tezi ya prostate hufinya njia ya mkojo na hupelekea kizuizi katika mirija na kibofu cha mkojo ( Bladder Obstruction) . Hali hii hutibika kwa dawa au upasuaji

Dalili za ongezeko la ukubwa wa tezi ya prostate;
  • Maambukizi ya mfumo wa mkojo mara kwa mara ( Urinary Tract Infection au UTI) Mabaki ya mkojo kwenye kibofu au mkojo uliosimama kwa muda mrefu  ni chanzo cha maambukizi ya mfumo wa mkojo
  • Mawe katika njia ya mkojo
  • Mkojo wenye matone ya damu
  • Kukojoa mara kwa mara(mabaki ya mkojo katika kibofu hupelekea mtu kuhisi anahitaji kukojoa mara kwa mara japo mkojo unaopatikana ni kidogo sana
  • Mkojo unaosita
  • Mkojo unaoshindikana kuzuia wa haraka na ghafla
  • Kuvuja kwa mkojo kidogo kidogo
  • Mkojo unaokatika katika
  • Mkojo wa mara kwa mara usiku( Nocturia)
  • Mkojo unaokulazimu kujikakamua

BAADHI YA VIPIMO VYA SARATANI YA TEZI YA PROSTATE
  • Prostate Specific Antigen (PSA); Kipimo hiki huchunguza kiwango cha antigen za prostate  kwenye damu ambacho kwa mtu wa kawaida, huwa kati ya  4 mg/ml. au pungufu. Testi hii huhitaji ushauri wa daktari
.
Prostate Specific Antigen (PSA); Kipimo hiki huchunguza kiwango cha antigen za prostate  kwenye damu ambacho kwa mtu wa kawaida, huwa kati ya  4 mg/ml. au pungufu. Testi hii huhitaji ushauri wa daktari



    Digital Rectal Exam ni testi ambayo hufanyika ili kugundua mabadiliko ya ukubwa au hitilafu inayoleta mabadiliko katika maumbile ya  tezi ya prostate













    Mara nyingi Prostate cancer haina dalili pale inapoanza lakini baadaye dalili zifuatazo huweza kujitokeza.
    • Damu kwenye mkojo
    • Ongezeko la ukubwa wa tezi ya prostate
    • Kupungua uzito wa mwili
    • Uchovu
    • Anemia (Upungufu wa chembe chembe nyekundu za damu)
    • Mkojo wa mara kwa mara usiku
    • Kuvuja kwa mkojo kidogo kidogo
    • Maumivu wakati wa kukojoa

    Dalili nyingine ;
    • Maumivu  wakati wa kukojoa
    • Kuhisi uhitaji wa kukojoa kwa ghafla
    • Damu kwenye mbegu za kiume (bloody semen)
    • Ugumu wa kufanya tendo la ndoa au kupungukiwa na nguvu katika uwezo huo
    • Maumivu katika utoaji wa mbegu za kiume
    • Uvimbe katika sehemu ya miguu au hip na sehemu za uume au pelvic
    • Kuhisi ganzi na maumivu ya mgongo, hip au miguu
    • Maumivu ya mifupa ya mda mrefu na yasiyo na nafuu

    Shukrani,

    Anatomy and Physiology: From Science to Life / Edition 1by Gail Jenkins, Christopher Kemnitz, Gerard J. Tortora, Gerard J. Tortora, Christopher Kemnit;:http://www.cancer.gov/cancertopics/pdq/treatment/prostate/PatientNational Kidney and Urologic Diseases Information Clearinghouse web site: “What I Need to Know About Prostate Problems.”http://web.archive.org/web/20020601194638/http://www.niddk.nih.gov/health/urolog/pubs/prospro/prospro.htm#1
    Prostate Cancer Foundation web site: “About the Prostate.”http://www.prostatecancerfoundation.org/site/c.itIWK2OSG/b.68230/k.DAE7/What_Is_the_Prostate.htmNetter, F. Atlas of Human Anatomy, 3rd edition, Saunders, 2002.
    Young, B. Wheater’s Functional Histology, 4th edition, Churchill Livingstone, 2000.American Cancer Society web site: “Overview: Prostate Cancer.”http://www.cancer.org/docroot/CRI/content/CRI_2_2_1X_How_many_men_get_prostate_cancer_36.asp?sitearea(University of Texas MD.Anderson Cancer Center) Images







    Comments

    Popular posts from this blog

    HUDUMA YA HARAKA KWA UPUNGUFU WA SUKARI MWILINI (HYPOGLYCEMIA)

    0 Ubongo wa binadamu unahitaji sukari kwa mda wote ili kuwa na nguvu ya kufanya kazi . Sukari hii yategemewa kutoka kwenye mzunguko wa damu kwani ubongo hauna uwezo wa kuzalisha au kuhifadhi sukari ya kutosha  matumizi ya  baadaye. Kutokana na hitilafu ya kingosho(dysfunctional pancreas) wagowja wa kisukari huwa na hali ngumu ya kuweka sukari katika vipimo vinavyohitajikana hivyo mara nyingi  sukari huwa juu (Hyperglycemia) au chini  (Hypoglycemia) na huhitaji tiba. Hivyo basi ni muhimu sana kwa ndugu au rafiki wa karibu kujua machache ili kuwa msaada pale mpendwa wako anapojikuta katika hali ya kuishiwa sukari kwani  inahitaji huduma ya haraka kuokoa maisha. DALILI ZA UPUNGIFU WA SUKARI MWILINI (Hypoglycemia) Kipimo cha sukari  chini ya    70 mg/dL au 3.9 mmol/L   chaweza hatarisha maisha ya mpendwa wako  mwenye kisukari. ; Njaa kuumwa kwa kichwa Kutokwa kwa jasho kutikisika kwa mwili Hasira Mwili au ngozi baridi na nyevu K

    UPUNGUFU WA POTASSIUM MWILINI, WAWEZA KUWA TISHIO KWA USALAMA WA MOYO !.

    NDIZI HUSIFIKA KWA UTAJIRI WAKE WA MADINI YA POTASSIUM Potassium ni moja  kati  ya madini muhimu ya chumvi chumvi mwilini.Ikisaidiana na chumvu chumvi nyingine kama Calcium, Magnesium na Sodium. Potassium ni muhimu sana kwenye usimamiaji wa kiwango sahihi cha maji mwilini, utendaji wa cell na kikubwa zaidi  uanzishaji wa mwendo ( conduction of  electricity) katika  misuli ya mwili yenye mwendo hiari na mwendo usio wa hiari. Hivyo, hupelekea mwamko katika mishipa ya moyo inayohusika na huwa ndio chanzo cha mapigo yanahusika na msukumo wa  damu mwilini. ( generates heart bit) Mahitaji ya Potassium kwa mtu mzima ni kati ya milligram zisizopungua 3,500 ml. kwa siku kutoka kwenye lishe. Ili mwili wa binadamu uweze kuendelea na utendaji wake, potassium iliyoko katika mzunguko wa damu yahitaji kuwa kati ya 3.5-5.0mEg/L. Kiwango hiki kikipopunguwa hutupelekea hali ijulikanayo kama; Hypokalemia au Upungufu wa Potassium katika damu. Vile vile kiwango hiki kinapozidia huitwa H

    MATATIZO YA THYROID KWA WANAWAKE .

    Thyroid ni mojawapo ya tezi zilizo mwilini zinazozalisha  homoni  (hormones) zake ndani ya mwili  na kutumika  kwenye mfumo wa  damu. Miongoni mwa kazi za homoni ya thyroid ni    kusimamia  utendaji wa shughuli  mwilini kama mwendo wa mapigo ya moyo,( heart rate),  usagaji wa chakula (digestion) ,mwendo na utendaji wa metaboli (metabolism)  na kusimamia matumizi ya calorie mwilini. Ili tezi ya thyroid iweze kufanya kazi yake ya uzalishaji homoni  huitaji madini ya Iodine.Madini  hayo hupatikana katika vyakula vya mimea vilivyotoka  kwenye udongo wenye virutubisho vya iodine ya kutosha, chumvi yenye iodine na vyakula vya baharini. Tezi ya thyroid inapozalisha homoni pungufu na kipimo kinachohitajika  husababisha  hali ijulikanayo kama   “Hypothyrodism”. Tezi hii  ikizalisha  homoni kupita kipimo kinachohitajika mwilini huitwa “Hyperthyrodism” LEO NINAPENDA KUZUNGUMZA NANYI KUHUSU UGONJWA WA HYPOTHYRODISM Hypothyrodism ni ugojwa ambao huwapata  wanawake zaidi kuliko