Skip to main content

CHUKUWA TAHADHARI KWA KUPATA CHANJO YA MAFUA MAKALI!




KAMATI YA AFYA  DMV
INATUKUMBUSHIA KUCHUKUWA  TAHADHARI KWA MAFUA MAKALI KWA KUPATA CHANJO YA MAFUA  SASA
Mafua/influenza (Flu) ni ugojwa wa kuambukiza (contagious disease) ambao husambaa hapa marekani wakati wa masika kati ya mwezi wa 5 na mwezi wa 10 .Mafua haya husababishwa na virusi vilivyo katikavya kundi la Influenza
1. Influenza A (H1N1),
2. Influenza A (H3N2)
3. Influenza B.
Maambukizi ya   Ifluenza A & B hupatikana pale unapokuwa karibu na mtu mwenye flu kupitia kukohoa, chafya au kugusana kwa karibu.Yashauriwa kuosha mikono mara kwa mara ili kupunguza maambukizi .Chanjo ya mafua (Flue shot) ni  mchanganyiko wa aina tatu za chanjo(Trivalent vaccine) ambazo hukinga watu dhidi ya virusi vya influenza .
DALILI ZA FLU
  • Homa 100F
  • Mafua,chafya,kukwaruza kwa koo
  • Maumivu ya kichwa,mwili,viungo
  • Uchovu wa mwili
  • Kichefuchefu,kutapika hata kuharisha
FAIDA YA CHANJO
a) Kukinga mwili na ugonjwa wa mafua makali / influenza (“Flu”)
b) Kupunguza Makali au kukinga kuambukiza mafua kwa watu wengine
NANI ALIYE HATARINI ?
  • Watoto (chini ya umri wa miaka mitano)
  • Wazee (miaka 65 na Zaidi)
  • Wagonjwa wenye kinga hafifu za mwili
  • Wanawake Wajawazito
  • Wafanyikazi wa vitengo vya afya
  • Watu wenye kusumbuliwa na magonjwa ya kisukari, asthma, shinikizo la damu, na sarakani.
CHANJO YA MAFUA BURE AU KWA BEI NAFUU HUPATIKANA HAPA.
Weka appointment kupitia: montgomerycomd.gov. Search flu shot location, select: flu clinic appointments 2014.
  • October 20, 2014 from 4 to 8 pm _Montgomery college: Rockville Campus, 9630 Gudesky Dr, Rockville MD 20850.  Giving shots for individuals 6 months of age or older by appointment only. FREE

  • October 31, 2014 from 9 am to 12 noon. Kennedy High school, Richard Montgomery high school and Seneca Valley high school for flu mist clinic by appointment only. Schedule appointments on at: Montgomerycomd.gov. Search flu shot location, select: flu clinic appointments 2014. FREE

  • November 3 and 17, 2014 from 1 pm to 4 pm. Silver Spring health center. 8630 Fenton st. Silver Spring, MD 20910: Schedule appointments on at: montgomerycomd.gov. Search flu shot location, select: flu clinic appointments 2014.FREE
  • November 17, 2014 from 8:30 am to 11:30 am – Germantown Health center.12900 Middlebrook Rd, Germantown MD 20874.
  • Muslim community clinic (MCC). Clinic ipo New Hampshire ave towards north kwenye majengo ya msikiti.
NOTE: Sehemu ambazo huduma sio bure unaombwa uje na health insurance kadi yako na wale wasio na Health Insurance kutakuwa na chaji ya $20 kulingana na MD kipimo cha umaskini ( MD state poverty sliding scale).
                            ILI TUSONGE MBELE, AFYA KWA WANADMV KWANZA !

Ref./Thanks
http://www.cdc.gov/flu/about/disease/symptoms
images

Comments

Popular posts from this blog

HUDUMA YA HARAKA KWA UPUNGUFU WA SUKARI MWILINI (HYPOGLYCEMIA)

0 Ubongo wa binadamu unahitaji sukari kwa mda wote ili kuwa na nguvu ya kufanya kazi . Sukari hii yategemewa kutoka kwenye mzunguko wa damu kwani ubongo hauna uwezo wa kuzalisha au kuhifadhi sukari ya kutosha  matumizi ya  baadaye. Kutokana na hitilafu ya kingosho(dysfunctional pancreas) wagowja wa kisukari huwa na hali ngumu ya kuweka sukari katika vipimo vinavyohitajikana hivyo mara nyingi  sukari huwa juu (Hyperglycemia) au chini  (Hypoglycemia) na huhitaji tiba. Hivyo basi ni muhimu sana kwa ndugu au rafiki wa karibu kujua machache ili kuwa msaada pale mpendwa wako anapojikuta katika hali ya kuishiwa sukari kwani  inahitaji huduma ya haraka kuokoa maisha. DALILI ZA UPUNGIFU WA SUKARI MWILINI (Hypoglycemia) Kipimo cha sukari  chini ya    70 mg/dL au 3.9 mmol/L   chaweza hatarisha maisha ya mpendwa wako  mwenye kisukari. ; Njaa kuumwa kwa kichwa Kutokwa kwa jasho kutikisika kwa mwili Hasira Mwili au ngozi baridi na nyevu K

UPUNGUFU WA POTASSIUM MWILINI, WAWEZA KUWA TISHIO KWA USALAMA WA MOYO !.

NDIZI HUSIFIKA KWA UTAJIRI WAKE WA MADINI YA POTASSIUM Potassium ni moja  kati  ya madini muhimu ya chumvi chumvi mwilini.Ikisaidiana na chumvu chumvi nyingine kama Calcium, Magnesium na Sodium. Potassium ni muhimu sana kwenye usimamiaji wa kiwango sahihi cha maji mwilini, utendaji wa cell na kikubwa zaidi  uanzishaji wa mwendo ( conduction of  electricity) katika  misuli ya mwili yenye mwendo hiari na mwendo usio wa hiari. Hivyo, hupelekea mwamko katika mishipa ya moyo inayohusika na huwa ndio chanzo cha mapigo yanahusika na msukumo wa  damu mwilini. ( generates heart bit) Mahitaji ya Potassium kwa mtu mzima ni kati ya milligram zisizopungua 3,500 ml. kwa siku kutoka kwenye lishe. Ili mwili wa binadamu uweze kuendelea na utendaji wake, potassium iliyoko katika mzunguko wa damu yahitaji kuwa kati ya 3.5-5.0mEg/L. Kiwango hiki kikipopunguwa hutupelekea hali ijulikanayo kama; Hypokalemia au Upungufu wa Potassium katika damu. Vile vile kiwango hiki kinapozidia huitwa H

MATATIZO YA THYROID KWA WANAWAKE .

Thyroid ni mojawapo ya tezi zilizo mwilini zinazozalisha  homoni  (hormones) zake ndani ya mwili  na kutumika  kwenye mfumo wa  damu. Miongoni mwa kazi za homoni ya thyroid ni    kusimamia  utendaji wa shughuli  mwilini kama mwendo wa mapigo ya moyo,( heart rate),  usagaji wa chakula (digestion) ,mwendo na utendaji wa metaboli (metabolism)  na kusimamia matumizi ya calorie mwilini. Ili tezi ya thyroid iweze kufanya kazi yake ya uzalishaji homoni  huitaji madini ya Iodine.Madini  hayo hupatikana katika vyakula vya mimea vilivyotoka  kwenye udongo wenye virutubisho vya iodine ya kutosha, chumvi yenye iodine na vyakula vya baharini. Tezi ya thyroid inapozalisha homoni pungufu na kipimo kinachohitajika  husababisha  hali ijulikanayo kama   “Hypothyrodism”. Tezi hii  ikizalisha  homoni kupita kipimo kinachohitajika mwilini huitwa “Hyperthyrodism” LEO NINAPENDA KUZUNGUMZA NANYI KUHUSU UGONJWA WA HYPOTHYRODISM Hypothyrodism ni ugojwa ambao huwapata  wanawake zaidi kuliko