KUPATA HUDUMA HII ENEO LA DMV KWA ASIYE NA BIMA YA AFYA CALL 240 672 1788
Tezi Dume, ni tezi yenye umbile la donati iliyoko chini ya kibofu cha mkojo.Tezi hii huzungukwa na mirija ya mkojo na uhusika na urutubishaji wa mbegu za kiume (semen). Mabadiliko ya kimaumbile katika tezi ya prostate kama uvimbe,ongezeko la ukubwa au kushamiri kwa saratani, hupelekea hitilafu katika mfumo wa mkojo kwa kufinya mrija wa mkojo na hivyo mkojo kupita kwa shida,hukwama au kuacha mabaki.Hali hii humpelekea mgojwa uhitaji wa kutumia bafu mara kwa mara na hata kushindwa kuzia mkojo kuchuruzika. (Maumbile yote mwilini, yamekadiriwa kulingana na nafasi iliyoko, hivyo umbile linapoongezeka ukubwa, huleta hitilafu kwa mfumo mwingine).Saratani ya Prostate yaweza sambaa katika mifupa na tishu za jirani na hata kubana mishipa ya mgongo na kuleta maumivu sehemu za mgongo,hip na pelvic.Yashauriwa kufanya uchunguzi wa afya ya tezi dume kuanzia “miaka 45 kwa wale walio na historia ya saratani ya tezi dume katika familia, na kwa watu wa jamii ya Kiafrika”. Kwa ujumla uchunguzi wa tezi dume hushauriwa kwa wanaume wote kuanzia umri wa miaka 50. Kwa umri wa miaka 40, ni vyema kuzungumza na daktari wako ili kuongeza ufahamu na kuripoti mabadiliko yeyote.
BAADHI YA MATATIZO YA TEZI YA PROSTATE
Prostate Cancer ( Saratani ya tezi ya Prostate ) Saratani ya prostate ni saratani inayowashambulia wanaume hasa kuanzia umri wa miaka 50 na kuendelea.Saratani hii huweza kutibika kwa mionzi (radiation), upasuaji, chemotherapy au hormonal therapy.
BAADHI YA VIPIMO VYA SARATANI YA TEZI YA PROSTATE
Digital Rectal Exam ni testi ambayo hufanyika ili kugundua mabadiliko ya ukubwa au hitilafu inayoleta mabadiliko katika maumbile ya tezi ya prostate
Mara nyingi Prostate cancer haina dalili pale inapoanza lakini baadaye dalili zifuatazo huweza kujitokeza.
Dalili nyingine ;
Shukrani,
|
Dalili za ongezeko la ukubwa wa tezi ya prostate;
- Maambukizi ya mfumo wa mkojo mara kwa mara ( Urinary Tract Infection au UTI) Mabaki ya mkojo kwenye kibofu au mkojo uliosimama kwa muda mrefu ni chanzo cha maambukizi ya mfumo wa mkojo
- Mawe katika njia ya mkojo
- Mkojo wenye matone ya damu
- Kukojoa mara kwa mara(mabaki ya mkojo katika kibofu hupelekea mtu kuhisi anahitaji kukojoa mara kwa mara japo mkojo unaopatikana ni kidogo sana
- Mkojo unaosita
- Mkojo unaoshindikana kuzuia wa haraka na ghafla
- Kuvuja kwa mkojo kidogo kidogo
- Mkojo unaokatika katika
- Mkojo wa mara kwa mara usiku( Nocturia)
- Mkojo unaokulazimu kujikakamua
BAADHI YA VIPIMO VYA SARATANI YA TEZI YA PROSTATE
- Prostate Specific Antigen (PSA); Kipimo hiki huchunguza kiwango cha antigen za prostate kwenye damu ambacho kwa mtu wa kawaida, huwa kati ya 4 mg/ml. au pungufu. Testi hii huhitaji ushauri wa daktari
Prostate Specific Antigen (PSA); Kipimo hiki huchunguza kiwango cha antigen za prostate kwenye damu ambacho kwa mtu wa kawaida, huwa kati ya 4 mg/ml. au pungufu. Testi hii huhitaji ushauri wa daktari
Digital Rectal Exam ni testi ambayo hufanyika ili kugundua mabadiliko ya ukubwa au hitilafu inayoleta mabadiliko katika maumbile ya tezi ya prostate
Mara nyingi Prostate cancer haina dalili pale inapoanza lakini baadaye dalili zifuatazo huweza kujitokeza.
- Damu kwenye mkojo
- Ongezeko la ukubwa wa tezi ya prostate
- Kupungua uzito wa mwili
- Uchovu
- Anemia (Upungufu wa chembe chembe nyekundu za damu)
- Mkojo wa mara kwa mara usiku
- Kuvuja kwa mkojo kidogo kidogo
- Maumivu wakati wa kukojoa
Dalili nyingine ;
- Maumivu wakati wa kukojoa
- Kuhisi uhitaji wa kukojoa kwa ghafla
- Damu kwenye mbegu za kiume (bloody semen)
- Ugumu wa kufanya tendo la ndoa au kupungukiwa na nguvu katika uwezo huo
- Maumivu katika utoaji wa mbegu za kiume
- Uvimbe katika sehemu ya miguu au hip na sehemu za uume au pelvic
- Kuhisi ganzi na maumivu ya mgongo, hip au miguu
- Maumivu ya mifupa ya mda mrefu na yasiyo na nafuu
Shukrani,
Anatomy and Physiology: From Science to Life / Edition 1by Gail Jenkins, Christopher Kemnitz, Gerard J. Tortora, Gerard J. Tortora, Christopher Kemnit;:http://www.cancer.gov/cancertopics/pdq/treatment/prostate/PatientNational Kidney and Urologic Diseases Information Clearinghouse web site: “What I Need to Know About Prostate Problems.”http://web.archive.org/web/20020601194638/http://www.niddk.nih.gov/health/urolog/pubs/prospro/prospro.htm#1
Prostate Cancer Foundation web site: “About the Prostate.”http://www.prostatecancerfoundation.org/site/c.itIWK2OSG/b.68230/k.DAE7/What_Is_the_Prostate.htmNetter, F. Atlas of Human Anatomy, 3rd edition, Saunders, 2002.
Young, B. Wheater’s Functional Histology, 4th edition, Churchill Livingstone, 2000.American Cancer Society web site: “Overview: Prostate Cancer.”http://www.cancer.org/docroot/CRI/content/CRI_2_2_1X_How_many_men_get_prostate_cancer_36.asp?sitearea(University of Texas MD.Anderson Cancer Center) Images

Comments
Post a Comment