Shinikizo la damu hutambulika kama 'Silent Killer' kutokana na ukosefu wa dalili japo maafa yaendelea taratibu.Wengi wenye tatizo hili huwa nalo hata miaka bila dalili na hivyo kutishia usalama wa maisha . Shinikizo la damu hutuweka katika hatari za stroke, heart attack,upofu wa macho pamoja na kudhofisha utendaji wa figo au kuuwa figo ambayo kazi yake kubwa ni kuchuja uchafu mwilini.
CHATI HII YAASHIRIA VIPIMO VYA SHINIKIZO LA DAMU
Ili kugundua tatizo hili ni budi kupima. Ugunduzi na ufumbuzi wa mapema ni wa muhimu na hupunguza madhara yatokanayo na shinikizo la damu.
Baadhi ya dalili chache pale tatizo hili linapozidia ni;
- maumivu ya kichwa,
- kizunguzungu,
- kichefuchefu,
- uhafifu wa kuona,
- kupoteza uwezo wa kutambua
- kuzimia.
VIJISHIPA VIDOGO KATIKA UBONGO VILIVYOPASUKA NA KUVUJA DAMU KUTOKANANA TATIZO LA SHINIKIZO LA DAMU LISILO NA UANGALIZI.
Mishipa ya damu huweza athirika pia kutokana na ongezeko la cholesterol mbaya mwilini(Low density lipoprotein au LDL) na kusababisha mkusanyiko wa mafuta, chembe za damu na uchafu (Plaque) katika ukuta wa mishipa ya damu.Uchafu huu hugandamana na ukuta wa mishipa ya damu na hufanya ukuta huo kuwa mnene na mgumu (Atherosclerosis) .Hii yasababisha njia ya damu kuwa nyembamba na vigumu kwa damu kupenya. Njia hafifu huchangia damu kupenya kwa shida na kuhitaji msukumo mkubwa zaidi na hivyo kuulazimu moyo kuongeza nguvu na kasi. Ongezeko hilo huongeza kishindo cha damu katika mishipa kitu ambacho chawezapasua vijishipa vidogo,kuvujisha damu na kupata majeraha. Kama ilivyokawaida ya mwili kurepea majereha yake,mkusanyiko wa chembe za damu na madini hujikusanya katiaka eneo lililoathirika na kusababisha makovu ambayo hupunguza umahiri wa mishipa(flexibility) na kuifanya migumu. Mkusanyiko huo hutoa mvuto zaidi kwa cholesterol mbaya (LDL) kugandamana pamoja na mabaki ya calcium katika majeraha yaliyoyaacha makovu na hivyo kwa pamoja kugumisha na kuongeza unene wa ukuta wa mishipa.Mishipa ambayo ni migumu daima hufanya pressure ya damu kuwa juu kwani haina umahiri wa kutanuka na kujirudi pale msukumo wa damu unapoongezeka na kupungua kama inavyotakiwa.
Picha hizi zaashiria mishipa iliyogandamana kwa mkusanyiko (plaque) cholesterol mbaya na uchafu wa chembe nyingine mwilini,migumu na yenye nafasi ndogo kwa damu kupenya. (Atheroslcerosis).
Tatizo la uchafu(plaque) unaogandamana na ukuta wa mishipa ya damu ni uwezo wake wa kumegeka wakati wowote na kusafiri katika mishipa ya damu.Uchafu huu huwa ni kizuizi kwani waweza kukwama kwenye njia inayosafirisha damu katika sehemu mbali mbali za mwili.Hatari zaidi ni pale uchafu huu unapokwama kwenye mshipa unaoshuhulika na usafirishaji wa damu kwenye ubongo. Hapo ndipo mgao wa damu inayokwenda kwenye ubongo wapungua au kukatika na kusababisha ukosefu wa damu,oxygen na virutubisho katika ubongo na kutuweka katikahatari za stroke(Ischemic Stroke ).
Maafa ya mishipa iliyo na uchafu sehemu za moyo hutoa maumivu makali sehemu ya moyo pale mgao wa damu unapokuwa hafifu (Angina) na Heart Attack pale mgao wa damu unapokosekana kabisa.Kwani mishaipa ya moyo huitaji damu yenye kugawa oxygen na virutubisho muda wote ili kuweza fanya kazi yake vizuri.
Kwa upande wa mishipa inayosafirisha damu sehemu za miguu, ikiwa na kizuizi au (plaque)maumivu huwa makali baada ya kutembea kwa mda mfupi kwani mishipa inashidwa kupitisha damu ya kutosha yenye oxygen inayotosha kwa matumizi yaliyoongezeka wakati wa zoezi. Na mara nyingi mgojwa hujihisi nafuu pale anapopumzika au kuacha matembezi.Pia hushauriwa kuninginiza miguu pembeni ya kitanda(dangle the feet) ili kuruhusu urahisi wa msukumo wa damu yenye oxygen. (Peripheral Artery Disease)
SHINIKIZO LA DAMU LAWEZA SABABISHWA NA YAFUTAYO;
- Umri
- Ongezeko la cholesterol mbaya mwilini
- Diet ya vyakula vya mafuta,nyama nyekundu,chumvi au vyakula hafifu (processed foods na sukari nyingi)
- Hasili ya rangi takwimu zaonyesha weusi ni wengi kuliko wazungu
- Historia ya shinikizo la damu kifamilia
- Aina tofauti za dawa
- Kisukari
- Gout
- Magojwa ya figo
- Uvutaji wa sigara au tobacco.
- Ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi au Potassium kidogo.
- Ukosefu wa mazoezi ya mwili .
- Unene wa mwili.
- Utumiaji wa pombe kupita kiasi (>2/siku kwa mme au >1/siku kwa mke)
KINGA AU TIBA
Wengi tunakubali kwamba kinga ni bora kuliko tiba kwani mti haunyauki siku moja, huwanza na tawi hatimaye mti huporomoka. Mbali na dawa za shinikizo la damu, hatuna budi kubadili mfumo wa maisha kama;
- kupunguza chumvi, mafuta,sukari au processed foods.
- Acha uvutaji wa sigara,
- Punguza pombe
- Punguza uzito wa mwili.
- Fanya mazoezi ya mwili walau mara 4 hadi 5 kwa wiki
- Ongeza mboga,matunda na vyakula asilia (ambavyo havijakobolewa na sio vya makopo)
- Pika mara kwa mara kuliko kula migahawani
- Punguza nyama choma,nyekundu na za mafuta
Wataalamu wanashauri kupima pressure mara kwa mara ili kugundua mapema pale unapokuwa na mabadiliko na kufanyia marekebisho.
Shukrani;
http://www.cdc.gov/bloodpressure/
http://www.cdc.gov/stroke/types_of_stroke.htm
http://www.nhlbi.nih.gov/health/health-topics/topics/atherosclerosis
http://watchlearnlive.heart.org/CVML_Player.php?moduleSelect=hemstrh
Comments
Post a Comment