Skip to main content

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI ( CERVICAL CANCER ).


Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ambayo hutokana na mabadiliko ya mfumo wa chembechembe au cells zilizoko  katika shingo ya kizazi.Mabadiliko haya hupelekea chembe chembe hizo kushamiri na kuzaliana kwa kasi kinyume na mpangilio wa maumbile.

Saratani ya Shingo ya kizazi yasemekana kuwa ni saratani inayoongoza kwa kusababisha vifo vya  wanawake katika nchi zinazoendelea. Repoti ya 2012 ya shirika la afya duniani 'WHO' imesema kati ya matukio 75,000 ya waathirika wa saratani ya kizazi barani Afrika, 50,000 walifariki dunia.Namba za matukio haya zinawakilisha waathirika waliopata fursa ya utafiti jabo


NINI KINACHOSABISHA SARATANI YA SHINGO YA UZAZI ?

Ripoti za utafiti wa kisayansi zimeafiki kuwa asilimia 99%  ya saratani za shingo ya kizazi hutokana na maambukizi ya virusi vya 'Human Papillomavirus' au HPV vilivyoko katika jamii ya papilloma. Baadhi ya virusi hivi vyenye aina zaidi ya mia moja huambukizwa kwa njia ya  kujamiana.






BAADHI YA MAMBO YANAYOONGEZA  HATARI  ZA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI?

  • Kushiriki tendo ndoa katika  umri mdogo au chini ya miaka 18
  • Kuwa na wenzi tofauti au mwenzi aliye na wapenzi tofauti
  • Utumiaji wa sigara kwani hupunguza nguvu ya kinga mwilini(impairs immune system)
  • Watu wenye kinga hafifu ya mwili au magojwa kama Ukimwi
  • Uzazi wa mara kwa mara


BAADHI YA DALILI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

  • Kutokwa na majimaji au uchafu wenye harufu kali ukeni.
  • Kutokwa na damu ukeni mbali na siku za mwezi au baada ya tendo la ndoa
  • Maumivu makali ya sehemu ya chini ya tumbo ( pelvic area)
  • Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana.
  • Kupungua kwa uzito wa mwili bila kukusudia
  • Mkojo wenye matone ya damu


JE SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI HUTIBIKA ?
Saratani ya shingo ya kizazi yaweza kutibika iwapo itagundulika mapema.

PAP TEST (PAPANICOLAOUS TEST);

Pap-Smear ni test ambayo hutumika  kuchunguza  mabadiliko ya chembe zilizoko katika mlango wa kizazi   ili kugundua mabadiliko yanayotokea katika chembe hizo na hivyo kuwahi kuyakabili mapema.




UMRI WA KUPATA PAP TEST
Test hii hushauriwa kwa wanamke wa umri wa miaka 21 hadi 65  na chini ya umri wa miaka 21 endapo umeingia katika tendo la ndoa kwa kipindi cha kisichopungua miaka 3.


KUPUNGUZA HATARI ZA
SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI?

  • Pap tests.  Waweza kupata Pap test mara 1 kwa mwaka au mara 1 kwa miaka 2- 3,hii itategemea ushauri wa daktari,umri,hali yako ya afya kwa ujumla, na majibu uliyoyapata katika testi zilizotangulia na mfumo wako wa maisha.

  • Pata HPV vaccine (hii yashauriwa kati ya umri wa miaka 12 hadi 26 chini ya mwongozo wa daktari)

    • Kuwa na mpenzi mmoja. Mahusiano ya kimwili na mtu mmoja hupunguza hatari za maambukizi ya magojwa ya zinaa.

    • Tumia kinga (condoms). Hii husaidia kupunguza maambukizi ya magojwa ya  zinaa  


    Shukrani/Thanks;

    Ignatavicius, D.D. & Workman, M.L. (2010). Medical-Surgical Nursing: Patient-Centered Collaborative Care (6th ed.).
    (WHO/ICO HPV Information Centre 2010)
    https://www.imaworldhealth.org/archive/cervical
    (WHO/ICO HPV Information Centre 2010)

    Comments

    Popular posts from this blog

    HUDUMA YA HARAKA KWA UPUNGUFU WA SUKARI MWILINI (HYPOGLYCEMIA)

    0 Ubongo wa binadamu unahitaji sukari kwa mda wote ili kuwa na nguvu ya kufanya kazi . Sukari hii yategemewa kutoka kwenye mzunguko wa damu kwani ubongo hauna uwezo wa kuzalisha au kuhifadhi sukari ya kutosha  matumizi ya  baadaye. Kutokana na hitilafu ya kingosho(dysfunctional pancreas) wagowja wa kisukari huwa na hali ngumu ya kuweka sukari katika vipimo vinavyohitajikana hivyo mara nyingi  sukari huwa juu (Hyperglycemia) au chini  (Hypoglycemia) na huhitaji tiba. Hivyo basi ni muhimu sana kwa ndugu au rafiki wa karibu kujua machache ili kuwa msaada pale mpendwa wako anapojikuta katika hali ya kuishiwa sukari kwani  inahitaji huduma ya haraka kuokoa maisha. DALILI ZA UPUNGIFU WA SUKARI MWILINI (Hypoglycemia) Kipimo cha sukari  chini ya    70 mg/dL au 3.9 mmol/L   chaweza hatarisha maisha ya mpendwa wako  mwenye kisukari. ; Njaa kuumwa kwa kichwa Kutokwa kwa jasho kutikisika kwa mwili...

    UPUNGUFU WA POTASSIUM MWILINI, WAWEZA KUWA TISHIO KWA USALAMA WA MOYO !.

    NDIZI HUSIFIKA KWA UTAJIRI WAKE WA MADINI YA POTASSIUM Potassium ni moja  kati  ya madini muhimu ya chumvi chumvi mwilini.Ikisaidiana na chumvu chumvi nyingine kama Calcium, Magnesium na Sodium. Potassium ni muhimu sana kwenye usimamiaji wa kiwango sahihi cha maji mwilini, utendaji wa cell na kikubwa zaidi  uanzishaji wa mwendo ( conduction of  electricity) katika  misuli ya mwili yenye mwendo hiari na mwendo usio wa hiari. Hivyo, hupelekea mwamko katika mishipa ya moyo inayohusika na huwa ndio chanzo cha mapigo yanahusika na msukumo wa  damu mwilini. ( generates heart bit) Mahitaji ya Potassium kwa mtu mzima ni kati ya milligram zisizopungua 3,500 ml. kwa siku kutoka kwenye lishe. Ili mwili wa binadamu uweze kuendelea na utendaji wake, potassium iliyoko katika mzunguko wa damu yahitaji kuwa kati ya 3.5-5.0mEg/L. Kiwango hiki kikipopunguwa hutupelekea hali ijulikanayo kama; Hypokalemia au Upungufu wa Potassium katika damu. Vile vile kiwang...

    MATATIZO YA THYROID KWA WANAWAKE .

    Thyroid ni mojawapo ya tezi zilizo mwilini zinazozalisha  homoni  (hormones) zake ndani ya mwili  na kutumika  kwenye mfumo wa  damu. Miongoni mwa kazi za homoni ya thyroid ni    kusimamia  utendaji wa shughuli  mwilini kama mwendo wa mapigo ya moyo,( heart rate),  usagaji wa chakula (digestion) ,mwendo na utendaji wa metaboli (metabolism)  na kusimamia matumizi ya calorie mwilini. Ili tezi ya thyroid iweze kufanya kazi yake ya uzalishaji homoni  huitaji madini ya Iodine.Madini  hayo hupatikana katika vyakula vya mimea vilivyotoka  kwenye udongo wenye virutubisho vya iodine ya kutosha, chumvi yenye iodine na vyakula vya baharini. Tezi ya thyroid inapozalisha homoni pungufu na kipimo kinachohitajika  husababisha  hali ijulikanayo kama   “Hypothyrodism”. Tezi hii  ikizalisha  homoni kupita kipimo kinachohitajika mwilini huitwa “Hyperthyrodism” LEO NINAPENDA KUZUNGUMZA NANYI K...