Skip to main content

JE WAJUA ANEMIA NI TATIZO SUGU KATIKA JAMII.




Ripoti nyingi za wanasayansi zinaonyesha kwamba tatizo la upungufu wa damu mwilini ni tatizo linalosumbuwa zaidi jamii ya watu weusi. Tatizo hili lijulikanalo kwa jina la Anemia, husababishwa na upungufu wa iron au madini ya chuma mwilini yanayohusika katika utengenezaji wa chembechembe nyekundu za damu ( hemoglobin)

Kazi kubwa ya chembechembe hizi mwilini ni kusafirisha  hewa ya Oxygen kutoka  kwenye mapafu kuelekea  kwenye tishu au sehemu mbali mbali za mwilini. Hivyo  upungufu wa chembechembe nyekundu za dam mwilini  hutupelekea uhafifu wa mgao wa oxygen kwenye damu na hivyo kuulazimisha moyo kufanya kazi kwa nguvu zaidi ili kufikisha oxygen katika viungo mbali mbali. Hali hii hupelekea moyo kuongeza kasi ya mapigo japo mgao wa damu bado ni hafifu; hali hii hutuacha na hisia za kuishiwa pumzi na hata kupelekea maumivu ya kifua hasa wakati wa zoezi kama kutembea,kupanda ngazi nk. uchovu wa mwili, maumivu ya kichwa, kizunguzungu, kichefuchefu na mengine mengi.

Kazi ingine ya chembe chembe nyekundu za damu mwilini ni  kusafirisha hewa ya Carbon kutoka mwilini kuelekea kwenye mapafu ambapo hutolewa nje tunapopumua.

BAADHI YA SABABU ZINAZOSABABISHA ANEMIA
  • Hitilafu katika jenetiki (mfano ugojwa wa sickle cell anemia)
  • kupoteza damu nyingi mwilini, 
  • magonjwa ya uboho (bone marrow diseases)
  • Ukosefu wa vyakula vyenye madini ya iron 
  • Utumiaji sugu wa pombe  (Alcoholism)
  • Hitiliafu ya mfumo wa chakula inayozuia kufozwa kwa  virutubisho
Hali hii hujitokeza zadi kwa wanawake kwa ujumla hasa wajaa wazito, watoto,na wasichana kati ya miaka 11 hadi 19 (kundi hili hujulikana kwa uhafifu wa mlo kamilifu japo wanapoteza damu nyingi katika siku za mwezi) Wakifwatiwa na wazee kwani mfumo wa chakula hupunguza umahiri uzeeni na hivyo kuvyonza virutubisho pungufu zaidi ya mahitaji



BAADHI ya DALILI ZA UPUNGUFU WA MADINI YA CHUMA( IRON DEFICIENCY ) ANEMIA KWA WATU WAZIMA



  • Uchovu usioisha (chronic fatique syndrome)
  • Kuhisi kama unatobolewa na visindano kwenye miguu au vidole au ganzi (tingling)
  • Udhaifu mwilini
  • Kuishiwa pumzi katika shughuli ya kawaida kama kutembea ( Shortness of breath)
  • Maumivu ya kifua (hasa wakati wa kutembea au kupanda ngazi )
  • Kuumwa kichwa
  • Kizunguzungu hasa unaposimama ghafla (orthostatic hypotension)
  • Maambukizi ya mara kwa mara
  • Kucha hafifu na zenye kuvunjika mara kwa mara
  • Ubaridi wa mikono, miguu pamoja na kuhisi ganzi
  • Mapigo ya moyo ya haraka haraka na hata yenye hitilafu
  • Hamu ya kula vitu visivyo chakula kama udongo,chaki,mchele au unga mbichi. Hali hii hujulikana kisayansi kwa jina la  “ PICA”  
  •  Ongezeko la weupe wa macho


DALILI ZA ANEMIA KWA WATOTO WADOGO

  • Kupoteza hamu ya chakula
  • Dalili za kuzubaa au kuzorota katika utendaji,kama kutembea,kutambaa au kucheza
  • Mahangaiko na hasira au (irritability)
  • Ongezeko la weupe wa macho au kucha
  • Mapigo ya moyo ya harakaharaka na hata yenye hitilafu
 MAHITAJI YA IRON KWA WATOTO
  • Mtoto mchanga hupata kiwango cha Iron kinachohitajika kutoka kwa maziwa ya mama. Mama hushauriwa kuendelea na Prenatal vitamins ili kukidhi mahitaji haya. Kwa upande wa mtoto anayetumia fomula ,hushauriwa kutumia fomula iliyorutubishwa na iron au (iron fortified formula)
  • Mtoto anapofikia umri wa miezi 4-6 huwa tayari kuanza  uji au ceral laini,Hivyo umri huu hadi mwaka mmoja twashahuriwa kutumia cereal iliyorutubishwa na iron ili kukidhi ongezeko la  majitaji ya mwili pamoja na maziwa ya mama au fomula iliyorutubishwa na iron 
  • Mwaka 1 - 3 (Toddler) 7 mg za iron kwa siku
  • Miaka 4 -8  10 mg za iron kwa siku
  • Miaka 9-13  8 mg za iron kwa siku
  • 13 - 19  ni umri wa kuwa makini sana kwani mahitaji huongezeka kwa watoto wa kike hadi 15 mg. kutokana na upotezaji wa damu wakati wa mwezi. 
  • Yashauriwa kutumia vyakula vya makundi yote kwa kiwango sahihi;  kwani baadhi ya virutubisho kama vitamin C  ni muhimu sana na huwezesha ufyozwaji wa virutubisho vya iron mwilini.
  BAADHI YA VYAKULA VYENYE MADINI YA IRON




MBOGA ZENYE RANGI NZITO YA KIJANI


SAMAKI  ,    MAYAI    NA  MAHARAGE
MAINI
BAADHI YA MBEGU NA NUTS


TAHADHARI
Iron yawezapatikana katika mfumo wa vidonge vya nyongeza( suppliments) 
Chukuwa tahadhari kubwa kwani iron ikizidia mwilini huwa ni sumu (toxic) na hivyo huwezasababisha kifo. Hakikisha umeongea na daktari wako  kabla ya kutimia vidonge  vya iron au dawa kwa ujumla. 
Ni vyema kuzingatia vyakula vyenye virutubisho husika na pale inapolazimika tu, chini ya mwongozo wa daktari ndio kutumia dawa.
NB.Hifadhi vidonge vya iron (na dawa zote ) mbali na upeo wa mazingira ya watoto kwani rangi yake vyekundu uwavutia watoto wakifikiri ni pipi na kuhatarisha maisha.
Shukrani;

Ignatavicius, D.D. & Workman, M.L. (2010). Medical-Surgical Nursing: Patient-Centered Collaborative Care (6th ed.).
 IMAGES;

Comments

Popular posts from this blog

HUDUMA YA HARAKA KWA UPUNGUFU WA SUKARI MWILINI (HYPOGLYCEMIA)

0 Ubongo wa binadamu unahitaji sukari kwa mda wote ili kuwa na nguvu ya kufanya kazi . Sukari hii yategemewa kutoka kwenye mzunguko wa damu kwani ubongo hauna uwezo wa kuzalisha au kuhifadhi sukari ya kutosha  matumizi ya  baadaye. Kutokana na hitilafu ya kingosho(dysfunctional pancreas) wagowja wa kisukari huwa na hali ngumu ya kuweka sukari katika vipimo vinavyohitajikana hivyo mara nyingi  sukari huwa juu (Hyperglycemia) au chini  (Hypoglycemia) na huhitaji tiba. Hivyo basi ni muhimu sana kwa ndugu au rafiki wa karibu kujua machache ili kuwa msaada pale mpendwa wako anapojikuta katika hali ya kuishiwa sukari kwani  inahitaji huduma ya haraka kuokoa maisha. DALILI ZA UPUNGIFU WA SUKARI MWILINI (Hypoglycemia) Kipimo cha sukari  chini ya    70 mg/dL au 3.9 mmol/L   chaweza hatarisha maisha ya mpendwa wako  mwenye kisukari. ; Njaa kuumwa kwa kichwa Kutokwa kwa jasho kutikisika kwa mwili...

UPUNGUFU WA POTASSIUM MWILINI, WAWEZA KUWA TISHIO KWA USALAMA WA MOYO !.

NDIZI HUSIFIKA KWA UTAJIRI WAKE WA MADINI YA POTASSIUM Potassium ni moja  kati  ya madini muhimu ya chumvi chumvi mwilini.Ikisaidiana na chumvu chumvi nyingine kama Calcium, Magnesium na Sodium. Potassium ni muhimu sana kwenye usimamiaji wa kiwango sahihi cha maji mwilini, utendaji wa cell na kikubwa zaidi  uanzishaji wa mwendo ( conduction of  electricity) katika  misuli ya mwili yenye mwendo hiari na mwendo usio wa hiari. Hivyo, hupelekea mwamko katika mishipa ya moyo inayohusika na huwa ndio chanzo cha mapigo yanahusika na msukumo wa  damu mwilini. ( generates heart bit) Mahitaji ya Potassium kwa mtu mzima ni kati ya milligram zisizopungua 3,500 ml. kwa siku kutoka kwenye lishe. Ili mwili wa binadamu uweze kuendelea na utendaji wake, potassium iliyoko katika mzunguko wa damu yahitaji kuwa kati ya 3.5-5.0mEg/L. Kiwango hiki kikipopunguwa hutupelekea hali ijulikanayo kama; Hypokalemia au Upungufu wa Potassium katika damu. Vile vile kiwang...

MATATIZO YA THYROID KWA WANAWAKE .

Thyroid ni mojawapo ya tezi zilizo mwilini zinazozalisha  homoni  (hormones) zake ndani ya mwili  na kutumika  kwenye mfumo wa  damu. Miongoni mwa kazi za homoni ya thyroid ni    kusimamia  utendaji wa shughuli  mwilini kama mwendo wa mapigo ya moyo,( heart rate),  usagaji wa chakula (digestion) ,mwendo na utendaji wa metaboli (metabolism)  na kusimamia matumizi ya calorie mwilini. Ili tezi ya thyroid iweze kufanya kazi yake ya uzalishaji homoni  huitaji madini ya Iodine.Madini  hayo hupatikana katika vyakula vya mimea vilivyotoka  kwenye udongo wenye virutubisho vya iodine ya kutosha, chumvi yenye iodine na vyakula vya baharini. Tezi ya thyroid inapozalisha homoni pungufu na kipimo kinachohitajika  husababisha  hali ijulikanayo kama   “Hypothyrodism”. Tezi hii  ikizalisha  homoni kupita kipimo kinachohitajika mwilini huitwa “Hyperthyrodism” LEO NINAPENDA KUZUNGUMZA NANYI K...