Skip to main content

SHINIKIZO LA DAMU






Shinikizo la damu hujullikana kama 'Silent Killer' kwani ni wengi wenye tatizo hili na huishi nalo hata miaka paasipo kulitambua. Shinikizo la damu hutuweka katika hatari za kiharusi (stroke), mshituko na hata kushidwa kwa moyo (heart attack and/or heart failure), upofu wa macho, pamoja na kushindwa kwa figo ambayo kazi yake kubwa ni kuchuja uchafu mwilini.








 
Ili kugundua tatizo la shinikizo la damu mapema, ni budi kupata kipimo na kujenga tabia ya kujichunguza mara kwa mara . Uchunguzi na ufumbuzi wa mapema husaidia kupunguza madhara yatokanayo na shinikizo la damu.

Baadhi ya dalili chache pale tatizo hili linapozidia ni pamoja na;
  • maumivu ya kichwa, 
  • kizunguzungu,
  • kichefuchefu,
  • uhafifu wa kuona,
  • kupoteza uwezo wa kutambua na hata kuzimia. 
Shinikizo la damu uhashiria kishindo au kipondo cha mzunguko wa damu katika kuta za mishipa mwilini. Kipondo hicho kinapokuwa kikubwa kwa muda mrefu, hupeelekea kudhoofika kwa mishipa ya damu na hivyo kuifanya iwe hafifu. Uhafifu wa mishipa ya damu hasa katika ubongo ni hatari kwa usalama, mishipa hafifu ni rahisi kupasuka na kusababisha kuvuja kwa damu; hali mbayo hujulikana kama kiharusi au hemorrhagic stroke).


VIJISHIPA VIDOGO KATIKA UBONGO VILIVYOPASUKA NA KUVUJA DAMU.
TATIZO LITOKALO NA SHINIKIZO LA DAMU LILIKOSA UANGALIZI .

hemorrhagic stroke




                                        


Vile vile, Mishipa ya damu huweza athirika kutokana na ongezeko la cholesterol mbaya mwilini (Low density lipoprotein au LDL) na kusababisha mkusanyiko wa uchafu ujulikanao kama Plaque; mkusanyiko wa mafuta, chembe za damu na uchafu katika kuta za mishipa ya damu. Uchafu huu wenye mnato mzito, hugandamana na kuta za mishipa ya damu na kufanya kuta hizo kuwa nono, na ngumu hali ijulikanayo kama Atherosclerosis. Jambo hili husababisha njia ya damu kupunguza umahiri kwa kuwa nyembamba kinyume na maumbile, kupenyeka kwa shida, ngumu na isiyotanuka na kunywea kama kawaida ili kukabiliana na kipondo cha mzunguko wa damu, kuziba kabisa na kutoruhusu damu kupenya, hali ijulikanayo kama Ischemic Stroke

Njia hafifu ya mishipa ya damu, hupelekea damu kupenya kwa shida na hivyo kuhitaji msukumo mkubwa na wenye nguvu zaidi, hali hii hulazimu moyo kuongeza nguvu ya utendaji na kasi ili kutimiza jukumu la msukumo na mzunguko wa damu

Ongezeko hilo la utendaji wa moyo likiendelea kwa muda mrefu, hudhoofisha misuli ya moyo, kuifanya itanuke, ilegee na kupunguza umahiri wake. Hali hii yaweza pelekea msukumo hafifu wa damu, kushindwa kwa moyo au heart failure.

Vile vile ongezeke la kipondo cha mzunguko wa damu katika mishipa laweza sababisha vijishipa vidogo dogo kupasuka na kuchuruzika damu na kuleta majeraha. Kama ilivyokuwa kawaida kwa mwili kukarabati majereha yake, kwa haraka sana chembe za damu na madini hujikusanya katika eneo lililoathirika na kutoa mvuto zaidi kwa cholesterol mbaya (LDL) kugandamana pamoja namabaki ya calcium katika jeraha na kusababisha uwepo wa kovu. Kovu katika mshipa wa damu hupunguza umahiri wa mishipa(flexibility) kuifanya migumu na isiyopenyeka kwa urahisi na kudhoofisha usafirishaji wa damu.


Picha hizi zaashiria mishipa iliyogandamana kwa mkusanyiko (plaque) cholesterol mbaya na uchafu wa chembe nyingine mwilini,migumu na yenye nafasi ndogo kwa damu kupenya. (Atheroslcerosis).






Plaque;
Tatizo la uchafu (plaque) unaogandamana na ukuta wa mishipa ya damu ni uwezo wake wa kumegeka kwa ghafla au wakati wowote na kusafiri katika mishipa ya damu. Uchafu huu huwa ni kizuizi kwani waweza kukwama kwenye njia inayosafirisha damu sehemu mbali mbali mwilini.

Hatari zaidi ni pale uchafu huu unapokwama kwenye mshipa usafirisha damu kwenye ubongo kwani hupunguza mgao wa damu inayokwenda kwenye ubongo au kuikatiza kwa ghafla na kusababisha ukosefu wa damu safi ya oxygen, na virutubisho katika ubongo. Hali hii na kutuweka katikahatari za stroke (Ischemic Stroke ).

Maafa ya mishipa iliyo na uchafu sehemu za moyo hutoa maumivu makali sehemu ya moyo pale mgao wa damu unapokuwa hafifu (Angina) na shambulizi la moyo au Heart Attack pale mgao wa damu unapokosekana kabisa. Kwani mishipa ya moyo inihitaji damu yenye kugawa oxygen na virutubisho muda wote ili kuweza fanya kazi yake vizuri.

Kwa upande wa mishipa inayosafirisha damu sehemu za miguu, ikiwa na kizuizi au (plaque) maumivu ya miguu huwa makali baada ya kutembea kwa mda mfupi. Hali hii hujitokeza pale mishipa inaposhidwa kupitisha damu yenye oxygen ya kutosha inayoendana na ongezeko la uhitaji wa damu safi ya oxygen, kutokana na zoezi. Na mara nyingi mgojwa hujihisi nafuu pale anapopumzika au kuacha matembezi. Pia hushauriwa kuninginiza miguu pembeni ya kitanda (dangle the feet) ili kurahisisha upenyaji wa damu yenye oxygen. Hali hii hujulikana kama (Peripheral Artery Disease)
 


SHINIKIZO LA DAMU LAWEZA SABABISHWA NA YAFUTAYO;

  • Umri
  • Ongezeko la cholesterol mbaya mwilini
  • Diet ya vyakula vya mafuta,nyama nyekundu,chumvi au vyakula hafifu (processed foods na  sukari nyingi)
  • Hasili ya rangi takwimu zaonyesha weusi ni wengi kuliko wazungu
  • Historia ya shinikizo la damu kifamilia
  • Aina tofauti za dawa
  • Kisukari
  • Gout 
  • Magojwa ya figo
  • Uvutaji wa sigara au tobacco.
  • Ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi au Potassium kidogo.
  • Ukosefu wa mazoezi ya mwili .
  • Unene wa mwili.
  • Utumiaji wa pombe kupita kiasi (>2/siku, kwa mme au  >1/siku kwa mke)


KINGA AU TIBA

Wengi tunakubali kwamba kinga ni bora kuliko tiba kwani mti haunyauki siku moja, huwanza na tawi hatimaye mti huporomoka. Mbali na dawa za  shinikizo la damu, hatuna budi kubadili  mfumo  wa maisha kama;
  • kupunguza chumvi, mafuta,sukari au processed foods.
  • Acha uvutaji wa sigara,
  • Punguza pombe 
  • Punguza uzito wa mwili.
  • Fanya  mazoezi ya mwili walau mara 4 kwa wiki
  • Ongeza mboga,matunda  na vyakula asilia (ambavyo havijakobolewa na sio vya makopo)
  • Epuka nyama nyekundu
Wataalamu wanashauri kupima pressure mara kwa mara ili kugundua mapema pale unapokuwa na mabadiliko na kufainyia marekebisho.


Shukrani;
www.naturalhealthadvisory.com 
http://www.cdc.gov/bloodpressure/
http://www.cdc.gov/stroke/types_of_stroke.htm
http://www.nhlbi.nih.gov/health/health-topics/topics/atherosclerosis
http://watchlearnlive.heart.org/CVML_Player.php?moduleSelect=hemstrh




   

Comments

Popular posts from this blog

HUDUMA YA HARAKA KWA UPUNGUFU WA SUKARI MWILINI (HYPOGLYCEMIA)

0 Ubongo wa binadamu unahitaji sukari kwa mda wote ili kuwa na nguvu ya kufanya kazi . Sukari hii yategemewa kutoka kwenye mzunguko wa damu kwani ubongo hauna uwezo wa kuzalisha au kuhifadhi sukari ya kutosha  matumizi ya  baadaye. Kutokana na hitilafu ya kingosho(dysfunctional pancreas) wagowja wa kisukari huwa na hali ngumu ya kuweka sukari katika vipimo vinavyohitajikana hivyo mara nyingi  sukari huwa juu (Hyperglycemia) au chini  (Hypoglycemia) na huhitaji tiba. Hivyo basi ni muhimu sana kwa ndugu au rafiki wa karibu kujua machache ili kuwa msaada pale mpendwa wako anapojikuta katika hali ya kuishiwa sukari kwani  inahitaji huduma ya haraka kuokoa maisha. DALILI ZA UPUNGIFU WA SUKARI MWILINI (Hypoglycemia) Kipimo cha sukari  chini ya    70 mg/dL au 3.9 mmol/L   chaweza hatarisha maisha ya mpendwa wako  mwenye kisukari. ; Njaa kuumwa kwa kichwa Kutokwa kwa jasho kutikisika kwa mwili Hasira Mwili au ngozi baridi na nyevu K

UPUNGUFU WA POTASSIUM MWILINI, WAWEZA KUWA TISHIO KWA USALAMA WA MOYO !.

NDIZI HUSIFIKA KWA UTAJIRI WAKE WA MADINI YA POTASSIUM Potassium ni moja  kati  ya madini muhimu ya chumvi chumvi mwilini.Ikisaidiana na chumvu chumvi nyingine kama Calcium, Magnesium na Sodium. Potassium ni muhimu sana kwenye usimamiaji wa kiwango sahihi cha maji mwilini, utendaji wa cell na kikubwa zaidi  uanzishaji wa mwendo ( conduction of  electricity) katika  misuli ya mwili yenye mwendo hiari na mwendo usio wa hiari. Hivyo, hupelekea mwamko katika mishipa ya moyo inayohusika na huwa ndio chanzo cha mapigo yanahusika na msukumo wa  damu mwilini. ( generates heart bit) Mahitaji ya Potassium kwa mtu mzima ni kati ya milligram zisizopungua 3,500 ml. kwa siku kutoka kwenye lishe. Ili mwili wa binadamu uweze kuendelea na utendaji wake, potassium iliyoko katika mzunguko wa damu yahitaji kuwa kati ya 3.5-5.0mEg/L. Kiwango hiki kikipopunguwa hutupelekea hali ijulikanayo kama; Hypokalemia au Upungufu wa Potassium katika damu. Vile vile kiwango hiki kinapozidia huitwa H

MATATIZO YA THYROID KWA WANAWAKE .

Thyroid ni mojawapo ya tezi zilizo mwilini zinazozalisha  homoni  (hormones) zake ndani ya mwili  na kutumika  kwenye mfumo wa  damu. Miongoni mwa kazi za homoni ya thyroid ni    kusimamia  utendaji wa shughuli  mwilini kama mwendo wa mapigo ya moyo,( heart rate),  usagaji wa chakula (digestion) ,mwendo na utendaji wa metaboli (metabolism)  na kusimamia matumizi ya calorie mwilini. Ili tezi ya thyroid iweze kufanya kazi yake ya uzalishaji homoni  huitaji madini ya Iodine.Madini  hayo hupatikana katika vyakula vya mimea vilivyotoka  kwenye udongo wenye virutubisho vya iodine ya kutosha, chumvi yenye iodine na vyakula vya baharini. Tezi ya thyroid inapozalisha homoni pungufu na kipimo kinachohitajika  husababisha  hali ijulikanayo kama   “Hypothyrodism”. Tezi hii  ikizalisha  homoni kupita kipimo kinachohitajika mwilini huitwa “Hyperthyrodism” LEO NINAPENDA KUZUNGUMZA NANYI KUHUSU UGONJWA WA HYPOTHYRODISM Hypothyrodism ni ugojwa ambao huwapata  wanawake zaidi kuliko