Maziwa ya mama husifika kwa virutubisho vya hali ya juu na vyenye uwezo wa kukidhi mahitaji ya mtoto mchanga. Baadhi ya virutubisho hivyo ni pamoja na protini,wanga,mafuta na madini ambayo ni muhimu katika ukuwaji wa mtoto mchanga na uimarishaji wa mfumo wa ufahamu(Felden & Eidenkman, 2003). Vile vile, maziwa ya mama humpatia mototo kinga asilia yenye kumwezesha kupambana na baadhi ya magojwa na maambukizi yakiwemo;
- Maambukizi ya sikio na mafua ya mara kwa mara
- Magojwa ya mfumo wa chakula yanayopelekea kuharisha, pamoja na magojwa sugu kama crohn’s, celiac na necrotizing enterocolitis (Bhandari et al., 2003,..Morrow er al., 2004)
- Magojwa ya atopic kama eczema na asthma ambayo asilimia kubwa husababishwa na matatizo ya mzio (allergies)
- Hupunguza hatari za unene wa utotoni
- Hupunguza hatari za kifo cha ghafla kwa watoto wachanga SIDS (Sudden Infant Death Syndrome)
Baadhi ya faida kwa mama anayenyonyesha ni pamoja na kujenga mahusiano ya karibu ya awali kati ya mama na mtoto. Mama anayenyoshesha husemakana kupunguza hatari za magojwa ya saratani ya matiti na saratani ya ovari (Riman,..Persson.2004). Vile vile, tendo la kunyonyesha hupelekea mwamko wa ongezeko la uzalishaji wa homini ya oxytocini mwilini. Oxytoxini ni homoni inayohusika na kupelekea mwamko wa uchungu wa uzazi na uandaaji wa mazingira ya kukabiliana na zoezi la uzazi. Pale zoezi hilo linapokamilika oxytoxini husaidia kufinya au kubana misuli ya tumbo la uzazi na hivyo kupunguza hatari za mama kupoteza damu nyingi na kurudisha tumbo la uzazi katika hali yake ya awali. (Lawrence,..2005)
Shirika linalojihusisha na malezi bora kwa watoto wachanga "American Academy of Pediatrics" (AAP) lasisitiza unyonyeshaji wa watoto wachanga kwa kipindi kisichopungua miezi sita. Mtoto akishatimia umri wa miezi sita, AAP yashauri mtoto kupatiwa vyakula vigumu pamoja na maziwa ya mama ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya mwili. Mtoto anayeachishwa ziwa la mama chini ya umri wa miezi 12 hushauriwa kutumia fomula zilizo na virutubisho vya madini ya chuma na sio maziwa ya ng'ombe (Gartner et al. 2005)
Shukrani:
Maternity & women's health care, edition 9, Deitra Leonard Lowdermilk, Shannon E. Perry Karen Piotrowski - Deitra Lowdermilk - Mosby Elsevier - 2007
Picha:http://www.onehealthylife.org
The African American Health Program is funded by the Montgomery County Department of Health and Human Services and administered by McFarland & Associates, Inc
Comments
Post a Comment