Skip to main content

NI NINI HASA FAIDA YA MAZIWA YA MAMA?

Maziwa ya mama husifika kwa  virutubisho vya hali ya juu na vyenye uwezo wa kukidhi mahitaji ya mtoto mchanga. Baadhi ya virutubisho hivyo ni pamoja na protini,wanga,mafuta na madini ambayo ni muhimu katika ukuwaji wa mtoto mchanga na uimarishaji wa mfumo wa ufahamu(Felden & Eidenkman, 2003). Vile vile, maziwa ya mama humpatia mototo kinga asilia yenye kumwezesha kupambana na baadhi ya magojwa na maambukizi yakiwemo;
  • Maambukizi ya sikio na mafua ya mara kwa mara
  • Magojwa ya mfumo wa chakula yanayopelekea kuharisha, pamoja na magojwa sugu kama crohn’s, celiac na necrotizing  enterocolitis (Bhandari et al., 2003,..Morrow er al., 2004)
  • Magojwa ya atopic kama eczema na asthma ambayo asilimia kubwa husababishwa na matatizo ya mzio (allergies)
  • Hupunguza hatari za unene wa utotoni
  • Hupunguza hatari za kifo cha ghafla kwa watoto wachanga SIDS (Sudden Infant Death Syndrome)


Baadhi ya faida kwa mama anayenyonyesha ni pamoja na kujenga mahusiano ya karibu ya awali kati ya mama na mtoto. Mama anayenyoshesha husemakana kupunguza hatari za magojwa ya saratani ya matiti na saratani ya ovari (Riman,..Persson.2004). Vile vile, tendo la kunyonyesha hupelekea  mwamko wa ongezeko la uzalishaji wa  homini ya oxytocini mwilini. Oxytoxini ni homoni inayohusika na kupelekea mwamko wa uchungu wa uzazi na uandaaji wa mazingira ya kukabiliana na zoezi la uzazi. Pale zoezi hilo linapokamilika oxytoxini husaidia kufinya au kubana misuli ya tumbo la uzazi na hivyo kupunguza hatari za mama kupoteza damu nyingi na kurudisha tumbo la uzazi katika hali yake ya awali. (Lawrence,..2005)

Shirika linalojihusisha na malezi bora kwa watoto wachanga "American Academy of Pediatrics" (AAP)  lasisitiza  unyonyeshaji wa watoto wachanga  kwa kipindi kisichopungua miezi sita. Mtoto akishatimia umri wa miezi sita, AAP yashauri mtoto kupatiwa vyakula vigumu pamoja na maziwa ya mama ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya mwili. Mtoto anayeachishwa ziwa la mama chini ya umri wa miezi 12 hushauriwa kutumia fomula zilizo na virutubisho vya madini ya chuma na sio maziwa ya ng'ombe (Gartner et al. 2005)

Shukrani:
Maternity & women's health care, edition 9, Deitra Leonard Lowdermilk, Shannon E. Perry Karen Piotrowski - Deitra Lowdermilk - Mosby Elsevier - 2007
Picha:http://www.onehealthylife.org


The African American Health Program is funded by the Montgomery County Department of Health and Human Services and administered by McFarland & Associates, Inc


Comments

Popular posts from this blog

HUDUMA YA HARAKA KWA UPUNGUFU WA SUKARI MWILINI (HYPOGLYCEMIA)

0 Ubongo wa binadamu unahitaji sukari kwa mda wote ili kuwa na nguvu ya kufanya kazi . Sukari hii yategemewa kutoka kwenye mzunguko wa damu kwani ubongo hauna uwezo wa kuzalisha au kuhifadhi sukari ya kutosha  matumizi ya  baadaye. Kutokana na hitilafu ya kingosho(dysfunctional pancreas) wagowja wa kisukari huwa na hali ngumu ya kuweka sukari katika vipimo vinavyohitajikana hivyo mara nyingi  sukari huwa juu (Hyperglycemia) au chini  (Hypoglycemia) na huhitaji tiba. Hivyo basi ni muhimu sana kwa ndugu au rafiki wa karibu kujua machache ili kuwa msaada pale mpendwa wako anapojikuta katika hali ya kuishiwa sukari kwani  inahitaji huduma ya haraka kuokoa maisha. DALILI ZA UPUNGIFU WA SUKARI MWILINI (Hypoglycemia) Kipimo cha sukari  chini ya    70 mg/dL au 3.9 mmol/L   chaweza hatarisha maisha ya mpendwa wako  mwenye kisukari. ; Njaa kuumwa kwa kichwa Kutokwa kwa jasho kutikisika kwa mwili...

UPUNGUFU WA POTASSIUM MWILINI, WAWEZA KUWA TISHIO KWA USALAMA WA MOYO !.

NDIZI HUSIFIKA KWA UTAJIRI WAKE WA MADINI YA POTASSIUM Potassium ni moja  kati  ya madini muhimu ya chumvi chumvi mwilini.Ikisaidiana na chumvu chumvi nyingine kama Calcium, Magnesium na Sodium. Potassium ni muhimu sana kwenye usimamiaji wa kiwango sahihi cha maji mwilini, utendaji wa cell na kikubwa zaidi  uanzishaji wa mwendo ( conduction of  electricity) katika  misuli ya mwili yenye mwendo hiari na mwendo usio wa hiari. Hivyo, hupelekea mwamko katika mishipa ya moyo inayohusika na huwa ndio chanzo cha mapigo yanahusika na msukumo wa  damu mwilini. ( generates heart bit) Mahitaji ya Potassium kwa mtu mzima ni kati ya milligram zisizopungua 3,500 ml. kwa siku kutoka kwenye lishe. Ili mwili wa binadamu uweze kuendelea na utendaji wake, potassium iliyoko katika mzunguko wa damu yahitaji kuwa kati ya 3.5-5.0mEg/L. Kiwango hiki kikipopunguwa hutupelekea hali ijulikanayo kama; Hypokalemia au Upungufu wa Potassium katika damu. Vile vile kiwang...

.KUKABWA NA JINAMIZI A.K.A "SLEEP APNEA"

Je unahisi dalili zifuatazo? Kukoroma  kwa sauti kubwa hata kusumbua  mwenzio Uchovu unapoamka japo umelala usiku kucha  Maumivu ya kichwa unapoamka Mdomo au koo kuwa kavu unapoamka  Kusimamisha pumzi usingizini Kuzinduka mara kwa mara usingizini ukitafuta pumzi, kukabwa au kukohoa.? Usingizi wa mara kwa mara unaoingiliana na kazi,masomo,usalama barabarini. Ugumu wa kukaa macho kwa mda wakati wa vikao, kujisomea au kutazama TV Dalili kubwa ya Sleep Apnea ni kukoroma kwa sauti ya kuzidia na hata kukera mwezio Pict.Courtesy  of http://always-healthy.com/sleep-apnea  Harvard School of Medicine  yatoa ufafanuzi zaidi kuhusu ‘Kukabwa na Jinamizi’ a.k.a 'Obstructive Sleep Apnea'  (Ukosefu wa pumzi Usingizini) Video courtesy of Harvard School of Medicine UFAFANUZI NA ATHARI ZA UKOSEFU WA PUMZI USINGIZINI Binadamu yeyote anaposinzia mwili hulegea na viungo hupumzika.Ulegevu...