Kutoshiriki na kujitolea katika kuchangia rasilimali kwa ajili ya matumizi yetu sote kwa ujumla ni jipu linaloikuimba jamii yetu. Pengine labda ni tamaduni au binafsi hayajatusibu. Lakini, pale yatakapotukuta sio tu familia, ndugu, jamaa au marafiki bali jamii kwa ujumla huangaika kutafuta namna ya kupata huduma au kukidhi garama za tiba ambazo hazishikiki.
Sio vibaya kwa jamii yako kuwa ya msaada, bali njia hiyo haileti utatuzi endelevu. Tufahamu kwamba tuko katika nchi iliyoendelea na yenye mifumo mbali mbali iliyodhihirika kutoa utatuzi endelevu kwa watu kama sisi na wengine wengi wasio na ndugu,rafiki au jamii inayowajali.
Hivyo basi pale tunapoombwa kushiriki katika jitihada za kukusanya senti za kutusaidia kwa ujumla au HARAMBEE basi tufanye kama tunavyochangia harusi zetu, tukijitokeza kwa wingi, tena kwa vifijo na ngoma, Susan G.Komen hutoa msaada mkubwa tu hata kwa ndugu zetu wahitaji nyumbani Tanzania na yeye hushiriki binafsi na kuona bendera zinazopeperushwa.
IDADI YETU NI KUBWA KULIKO KUNDI AMBALO HUONEKANA MARA KWA MARA KTK PICHA
HONGERA TEAM TANZANIA
NI VYEMA KUSHIRIKI KATIKA PAMBANO DHIDI YA GOJWA LA SARATANI .
NI VYEMA KUSHIRIKI KATIKA PAMBANO DHIDI YA GOJWA LA SARATANI .
KUJIANDIKISHA tuma text ya jina na e-mail yako kwenda
240 -615 - 6042
240- 672 - 1788
tunatanguliza shukurani
See you May 7th, 2016
Comments
Post a Comment