Uchunguzi unaotuwezesha kutambuwa umbile la kawaida la titi na hivyo kutupelekea kutambua mabadiliko endapo yatatokea.Ushauri wa Jamii ya Utafiti wa saratani ya matiti nchini Marekani washauri wanawake kufanya uchunguzi binafsi wa matiti kuanzia umri wa miaka 20. Uchunguzi wa litaalamu wa Mammogram mara moja mwaka washauriwa kwa Wanawake kuanzia umri wa miaka 40.
Si ajabu kwa matiti mawili kutofautiana kimaumbile, tofauti tunayozungumzia hapa ni ile yenye kuleta mabadiliko upande mmoja, bila mabadiliko hayo kuonekana upande wa pili. Yashauriwa kufanya Uchunguzi Binafsi wa Matiti kila mwezi kati ya siku 3 hadi 5 baada ya kumaliza siku mwezi.
RIPOTI DALILI ZIFUATAZO KWA DAKTARI
- Titi lenye wekundu, mpauko au mchubuko
- Uororo usiowiana
- Ngozi iliyokunjamana
- Ngozi yenye unyeleo (pores) kama ganda la chungwa
- Kudidimia kwa chuchu
- Maumivu
- Vipele
- Muwasho
- Ongezeko la unene wa ngozi ya titi au kwapa
- Uvimbe katika titi au chini ya kwapa
- Mabadiliko katika chuchu yakiwemo mwelekeo; Kawaida chuchu ya kushoto huelekea kushoto na chuchu ya kulia huelekea kulia.
HATUA ZA UCHUNGUZI BINAFSI WA MATITI;
1.Simama wima mbele ya kioo na kisha tizama na chunguza muonekano wa umbile la titi na ripoti mabadiliko yafuatayo kwa daktari;
(2)Mikono kiunoni (hakikisha mabega yamenyooka) rudia hatua za mwanzo na jeuka taratibu upande hadi upande ili kukagua sehemu za ukingoni mwa titi
( 3) Mikono juu ya kichwa endelea kuchunguza, kisha mkono Mmoja baada ya mwingine, Tumia viganja vya vidole vitatu vya kati, papasa kwa kishindo cha kadri mzingo wote wa titi bila kusahau eneo la kwapa na kifua.
Tumia njia zifuatazo a)Mduara au Mzunguko b) Juu/Chini
4. Lala chali na weka mto chini ya bega. Kwa uchunguzi wa titi la kushoto, weka mto chini ya bega la kushoto na tumia mkono wa kulia. Vilevile kwa titi la kulia weka mto chini ya bega la kulia na tumia mkono wa kushoto) Hii husaidia tishu za titi kusambaa na kurahisisha uchuguzi.Fuata maelezo yaliyotangulia katika kipengele cha tatu.
5. Bonyeza chuchu ili kuona kama inatoa majimaji ya aina yeyote;yawezakuwa maji meupe, maziwa, usaa au damu (Kipengele hiki ni kwa wale wasio wajaa wazito au wanye nyonyesha).
Saratani ya Matiti yaweza kutibika endapo imegundulika mapema.
Kwa wale wasio na bima ya afya na wanahitaji Mammogram au huduma ya juu ya utafiti wa saratani ya matiti, tuma text kupitia 240 672-1788 au tembelea African Women Cancer Awareness Association (AWCAA); www.awcaa.org
Breast cancer.org
wcfcourier.com
wcfcourier.com
Many More....Thanks for the effort
Many more;
Comments
Post a Comment