Fimbo ya kutembelea yaweza tumika na wazee au mtu wa umri wowote mwenye uhitaji wa kuimarisha msingi kabla ya kupiga hatua ili kupunguza atari za kuanguka. Vilevile, fimbo husaidia kupunguza uzito unaotua katika viungo vya mwili kama magoti ,mgongo na hips. Uzito wa mwili huongeza mwelemeo na maumivu hasa kwa watu wenye arthritis, maumivu ya mgongo na maumivu mengine ya viungo.
Fimbo hii huweza kukunjika na kukaa ndani ya mkoba
Fimbo ya kutembelea hutakiwa kuwa na urefu wa kutosha ili kuepuka kuinama na kuumiza mgongo.
Urefu sahihi ni ule unaofika eneo la kiuno kwa mtu anayeitumia
Urefu sahihi ni ule unaofika eneo la kiuno kwa mtu anayeitumia
Watu wenye tatizo la usawa (balance ) huitaji mwangaza wa kutosha ili kupunguza atari za kuanguka.
Fimbo hii ina taa yenye mwangaza wa kutosha kuona unapokwenda
Waweza pata fimbo ya kutembelea katika duka lolote la vifaa vya afya.
Fimbo yenye taa huondoa kadhia za kubebana na tochi. Ni vyema mkono uwe huru kusaidia mtu ambaye tayari ana udhaifu endapo utahitajika mara .
MATUMIZI SAHIHI YA FIMBO YA KUTEMBELEA
- Fimbo ya kutembelea uhitaji kukaa upande wa mwili ulio imara na sio upande ulio dhaifu( wako wengi wenye kufanya kosa la kuiweka fimbo upande dhaifu)
- Baada ya kuweka fimbo upande imara, sogeza fimbo na mguu dhaifu kwanza kisha sogeza mguu imara. Hivyo fimbo na mguu dhaifu huambatana kama asemavyo mtaalam wa mazoezi ya kimwili ‘Brian Benjamin’ ili kugawanya uzito wa mwili kati ya upande wa mguu imara na upande dhaifu unaosaidiwa na fimbo ya kutembelea.
- Weka fimbo umbali wa 2'inch mbele au pembeni mwako na sio mbali nawe.
- Fimbo yenye urefu sahihi ni fimbo yenye kufika eneo la kiuno
- PANDA NGAZI; Wakati wa kupanda ngazi panda na mguu imara kwanza, ukifutia mguu wenye udhaifu pamoja na fimbo
- SHUKA NGAZI; Shusha kwanza mguu dhaifu, ukifuatiwa na fimbo, kisha weka mguu wenye nguvu ( kumbuka;juu nenda na mguu imara, chini shuka na mguu mbovu)
- Hakikisha umeondoa vizuizi vinavyowezachangia atari za kuanguka kama mkeka, nyaya za umeme, maji maji na furniture zilizo kwenye njia.
seniorhealth365.com
Comments
Post a Comment