Skip to main content

FIMBO YA KISASA YA KUTEMBELEA


Fimbo ya kutembelea yaweza tumika na wazee au mtu wa umri wowote mwenye uhitaji  wa kuimarisha msingi kabla ya kupiga hatua ili kupunguza  atari za kuanguka. Vilevile, fimbo husaidia  kupunguza uzito unaotua katika viungo vya mwili kama magoti ,mgongo na hips. Uzito wa mwili huongeza mwelemeo na maumivu hasa kwa watu wenye arthritis, maumivu ya mgongo na maumivu mengine ya viungo.


Fimbo hii huweza kukunjika na kukaa ndani ya mkoba

Fimbo ya kutembelea hutakiwa kuwa na urefu wa kutosha ili kuepuka kuinama na kuumiza mgongo.
Urefu  sahihi ni ule unaofika eneo la kiuno kwa mtu anayeitumia


Watu wenye tatizo la usawa (balance ) huitaji mwangaza wa kutosha ili kupunguza atari za kuanguka.


Fimbo hii ina taa yenye mwangaza wa kutosha kuona unapokwenda

Waweza pata fimbo ya kutembelea katika duka lolote la vifaa vya afya. 
Fimbo yenye taa huondoa kadhia za kubebana na tochi. Ni vyema mkono uwe huru kusaidia mtu ambaye tayari ana udhaifu endapo utahitajika mara .  

MATUMIZI SAHIHI YA FIMBO YA KUTEMBELEA

  • Fimbo ya kutembelea uhitaji kukaa upande wa mwili ulio imara na sio upande ulio dhaifu( wako wengi wenye kufanya kosa la kuiweka fimbo upande dhaifu)

  • Baada ya kuweka fimbo  upande imara, sogeza fimbo na  mguu dhaifu kwanza kisha sogeza mguu imara. Hivyo fimbo na mguu dhaifu huambatana kama asemavyo mtaalam wa mazoezi ya kimwili ‘Brian Benjamin’ ili kugawanya uzito wa mwili kati ya upande wa mguu imara na upande dhaifu unaosaidiwa na fimbo ya kutembelea.

  • Weka fimbo umbali wa 2'inch mbele au pembeni mwako na sio mbali nawe.
  • Fimbo yenye urefu sahihi ni fimbo yenye kufika eneo la kiuno

  • PANDA NGAZI; Wakati wa kupanda ngazi panda na mguu imara kwanza, ukifutia mguu wenye udhaifu pamoja na fimbo

  • SHUKA NGAZI; Shusha kwanza mguu dhaifu, ukifuatiwa na fimbo, kisha  weka mguu wenye nguvu ( kumbuka;juu nenda na mguu imara, chini shuka na mguu mbovu)
  • Hakikisha umeondoa vizuizi vinavyowezachangia atari za kuanguka kama mkeka, nyaya za umeme, maji maji na furniture zilizo kwenye njia.

Shukrani;
seniorhealth365.com

Comments

Popular posts from this blog

HUDUMA YA HARAKA KWA UPUNGUFU WA SUKARI MWILINI (HYPOGLYCEMIA)

0 Ubongo wa binadamu unahitaji sukari kwa mda wote ili kuwa na nguvu ya kufanya kazi . Sukari hii yategemewa kutoka kwenye mzunguko wa damu kwani ubongo hauna uwezo wa kuzalisha au kuhifadhi sukari ya kutosha  matumizi ya  baadaye. Kutokana na hitilafu ya kingosho(dysfunctional pancreas) wagowja wa kisukari huwa na hali ngumu ya kuweka sukari katika vipimo vinavyohitajikana hivyo mara nyingi  sukari huwa juu (Hyperglycemia) au chini  (Hypoglycemia) na huhitaji tiba. Hivyo basi ni muhimu sana kwa ndugu au rafiki wa karibu kujua machache ili kuwa msaada pale mpendwa wako anapojikuta katika hali ya kuishiwa sukari kwani  inahitaji huduma ya haraka kuokoa maisha. DALILI ZA UPUNGIFU WA SUKARI MWILINI (Hypoglycemia) Kipimo cha sukari  chini ya    70 mg/dL au 3.9 mmol/L   chaweza hatarisha maisha ya mpendwa wako  mwenye kisukari. ; Njaa kuumwa kwa kichwa Kutokwa kwa jasho kutikisika kwa mwili Hasira Mwili au ngozi baridi na nyevu K

UPUNGUFU WA POTASSIUM MWILINI, WAWEZA KUWA TISHIO KWA USALAMA WA MOYO !.

NDIZI HUSIFIKA KWA UTAJIRI WAKE WA MADINI YA POTASSIUM Potassium ni moja  kati  ya madini muhimu ya chumvi chumvi mwilini.Ikisaidiana na chumvu chumvi nyingine kama Calcium, Magnesium na Sodium. Potassium ni muhimu sana kwenye usimamiaji wa kiwango sahihi cha maji mwilini, utendaji wa cell na kikubwa zaidi  uanzishaji wa mwendo ( conduction of  electricity) katika  misuli ya mwili yenye mwendo hiari na mwendo usio wa hiari. Hivyo, hupelekea mwamko katika mishipa ya moyo inayohusika na huwa ndio chanzo cha mapigo yanahusika na msukumo wa  damu mwilini. ( generates heart bit) Mahitaji ya Potassium kwa mtu mzima ni kati ya milligram zisizopungua 3,500 ml. kwa siku kutoka kwenye lishe. Ili mwili wa binadamu uweze kuendelea na utendaji wake, potassium iliyoko katika mzunguko wa damu yahitaji kuwa kati ya 3.5-5.0mEg/L. Kiwango hiki kikipopunguwa hutupelekea hali ijulikanayo kama; Hypokalemia au Upungufu wa Potassium katika damu. Vile vile kiwango hiki kinapozidia huitwa H

MATATIZO YA THYROID KWA WANAWAKE .

Thyroid ni mojawapo ya tezi zilizo mwilini zinazozalisha  homoni  (hormones) zake ndani ya mwili  na kutumika  kwenye mfumo wa  damu. Miongoni mwa kazi za homoni ya thyroid ni    kusimamia  utendaji wa shughuli  mwilini kama mwendo wa mapigo ya moyo,( heart rate),  usagaji wa chakula (digestion) ,mwendo na utendaji wa metaboli (metabolism)  na kusimamia matumizi ya calorie mwilini. Ili tezi ya thyroid iweze kufanya kazi yake ya uzalishaji homoni  huitaji madini ya Iodine.Madini  hayo hupatikana katika vyakula vya mimea vilivyotoka  kwenye udongo wenye virutubisho vya iodine ya kutosha, chumvi yenye iodine na vyakula vya baharini. Tezi ya thyroid inapozalisha homoni pungufu na kipimo kinachohitajika  husababisha  hali ijulikanayo kama   “Hypothyrodism”. Tezi hii  ikizalisha  homoni kupita kipimo kinachohitajika mwilini huitwa “Hyperthyrodism” LEO NINAPENDA KUZUNGUMZA NANYI KUHUSU UGONJWA WA HYPOTHYRODISM Hypothyrodism ni ugojwa ambao huwapata  wanawake zaidi kuliko