Mwanaume hutambulika kama shujaa katika uso wa jamii. Hutegemewa kuonyesha ujasiri wakati wote na hata kuficha hisia za ndani ili asiwe pungufu katika jamii inayomzunguka.Ripoti ya utafiti uliofanywa na taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Kiakili nchini Marekani 'NIMH', imedhihirisha kuwa wanaume wengi huficha hisia zao za ndani kitu ambacho ni tofauti kubwa na wanawake. Utafiti huo ulioanza 2003, umesema kuwa zaidi ya wanaume millioni sita hupata hisia sugu za huzuni au Depression kila mwaka.
Depression ni hali ya hisia sugu za huzuni wenye uwezo wa kudhoofisha afya ya kisaikolojia unaombatana na dalili zifuatazo ;
- Msongo wa mawazo
- Kukata tamaa au kupoteza matumaini
- Ugumu wa kushiriki shughuli za kila siku kama usafi wa mwili,mavazi na mazingira,
- Ukosefu wa usingizi
- Hasira za ghafla
- Kutoshiriki mazungumzo au eneo lenye watu
- Kupoteza ladha ya chakula au ongezeko la mlo
- Hasira
- Ugumu wa kushiriki tendo la ndoa
- Ugumu wa kupata usingizi
- Maumivu ya mara kwa mara ya kichwa au mgongo
- Ongezeko la matendo yenye kuhatarisha usalama kama; pombe, wapenzi wa kubadili ghafla na bila uangalifu
- Uwendeshaji gari wa fujo na usiokuwa wa makini tofauti na kawaida
- Hata kukata tamaa ya kuishi
NINI KINASABABISHA HISIA SUGU ZA HUZUNI/DEPRESSION
Shukrani;
http://www.apa.org/research/action/men.aspx
- Ugumu wa maisha
- Kutofikia malengo ya maisha
- Kupoteza kazi
- Kupoteza mwenza
- Ukosefu wa nyanja za kukabilina na changamoto au mabadiliko
- Magojwa
- Kifo
- Baadhi ya dawa
- Kuvunjika kwa ndoa
- Ukosefu wa usingizi mwororo
- Utumiaji wa pombe
- Ukosefu wa kikundi tegemezi (support system)
- Historia ya kifamilia (predisposed factors)
BAADHI YA NJIA ZA KUPUNGUZA DEPRESSION
- Mazoezi ya mwili
- Mlo wenye virutubisho
- Uwepo wa marafiki au jamii yenye kutegemeana
- Kuzungumza kuhusu hisia za ndani na uwepo wa mwenye kuzijali
- Kubadili mazingira
- Dawa hupatikana kwa daktari kwa hali iliyo sugu na hasa yenye kutishia usalama
Mgojwa wa Depression huhitaji uwangalizi wa karibu na msaada
kutoka kwa familia. Chunguza kama kuna mipango ya kujidhuru na
pata msaada wa kitaalum mapema.
Shukrani;
http://www.apa.org/research/action/men.aspx
http://www.helpguide.org/mental/treatment_strategies_depression.htm
Image;stock-photo/worried_businessman.html
Comments
Post a Comment