Skip to main content

JE YAWEZEKANA KWA MWANAUME KUPATA DEPRESSION ?




Mwanaume hutambulika kama shujaa katika uso wa jamii. Hutegemewa kuonyesha ujasiri wakati wote na hata kuficha hisia za ndani ili asiwe pungufu katika jamii inayomzunguka.Ripoti ya utafiti uliofanywa na taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Kiakili nchini Marekani 'NIMH', imedhihirisha kuwa wanaume wengi huficha hisia zao za ndani kitu ambacho ni tofauti kubwa  na wanawake. Utafiti huo ulioanza 2003, umesema kuwa zaidi ya wanaume millioni sita hupata hisia sugu za huzuni au Depression kila mwaka.

Depression ni hali ya hisia  sugu za huzuni wenye uwezo wa kudhoofisha afya ya kisaikolojia unaombatana na dalili zifuatazo ;
  1. Msongo wa mawazo
  2. Kukata tamaa au kupoteza matumaini  
  3. Ugumu wa kushiriki shughuli za kila siku kama usafi wa mwili,mavazi na mazingira, 
  4. Ukosefu wa usingizi
  5. Hasira za ghafla
  6. Kutoshiriki mazungumzo au eneo lenye watu
  7. Kupoteza ladha ya chakula au  ongezeko la mlo 
BAADHI YA DALILI ZA DEPRESSION KWA WANAUME
  • Hasira
  • Ugumu wa kushiriki tendo la ndoa
  • Ugumu wa kupata usingizi
  • Maumivu ya mara kwa mara ya kichwa au mgongo
  • Ongezeko la matendo yenye kuhatarisha usalama kama; pombe, wapenzi  wa kubadili ghafla na bila uangalifu  
  • Uwendeshaji gari wa fujo na usiokuwa wa makini tofauti na kawaida
  • Hata kukata tamaa ya kuishi 
NINI KINASABABISHA HISIA SUGU ZA HUZUNI/DEPRESSION
  • Ugumu wa maisha 
  • Kutofikia malengo ya maisha
  • Kupoteza kazi
  • Kupoteza mwenza
  • Ukosefu  wa nyanja za kukabilina na changamoto au mabadiliko  
  • Magojwa
  • Kifo
  • Baadhi ya dawa
  • Kuvunjika kwa ndoa
  • Ukosefu wa usingizi mwororo
  • Utumiaji wa pombe
  • Ukosefu wa kikundi tegemezi (support system)
  • Historia ya kifamilia (predisposed factors)
BAADHI YA NJIA ZA KUPUNGUZA DEPRESSION
  • Mazoezi ya mwili
  • Mlo wenye virutubisho
  • Uwepo wa marafiki au jamii yenye kutegemeana
  • Kuzungumza kuhusu hisia za ndani na uwepo wa mwenye kuzijali
  • Kubadili mazingira
  • Dawa hupatikana kwa daktari kwa hali iliyo sugu na hasa yenye kutishia usalama 
Mgojwa wa Depression huhitaji uwangalizi wa karibu na msaada 

kutoka kwa familia. Chunguza kama kuna mipango ya kujidhuru na 

pata msaada wa kitaalum mapema.


Shukrani;

http://www.apa.org/research/action/men.aspx

http://www.helpguide.org/mental/treatment_strategies_depression.htm

Image;stock-photo/worried_businessman.html






Comments

Popular posts from this blog

HUDUMA YA HARAKA KWA UPUNGUFU WA SUKARI MWILINI (HYPOGLYCEMIA)

0 Ubongo wa binadamu unahitaji sukari kwa mda wote ili kuwa na nguvu ya kufanya kazi . Sukari hii yategemewa kutoka kwenye mzunguko wa damu kwani ubongo hauna uwezo wa kuzalisha au kuhifadhi sukari ya kutosha  matumizi ya  baadaye. Kutokana na hitilafu ya kingosho(dysfunctional pancreas) wagowja wa kisukari huwa na hali ngumu ya kuweka sukari katika vipimo vinavyohitajikana hivyo mara nyingi  sukari huwa juu (Hyperglycemia) au chini  (Hypoglycemia) na huhitaji tiba. Hivyo basi ni muhimu sana kwa ndugu au rafiki wa karibu kujua machache ili kuwa msaada pale mpendwa wako anapojikuta katika hali ya kuishiwa sukari kwani  inahitaji huduma ya haraka kuokoa maisha. DALILI ZA UPUNGIFU WA SUKARI MWILINI (Hypoglycemia) Kipimo cha sukari  chini ya    70 mg/dL au 3.9 mmol/L   chaweza hatarisha maisha ya mpendwa wako  mwenye kisukari. ; Njaa kuumwa kwa kichwa Kutokwa kwa jasho kutikisika kwa mwili Hasira Mwili au ngozi baridi na nyevu K

UPUNGUFU WA POTASSIUM MWILINI, WAWEZA KUWA TISHIO KWA USALAMA WA MOYO !.

NDIZI HUSIFIKA KWA UTAJIRI WAKE WA MADINI YA POTASSIUM Potassium ni moja  kati  ya madini muhimu ya chumvi chumvi mwilini.Ikisaidiana na chumvu chumvi nyingine kama Calcium, Magnesium na Sodium. Potassium ni muhimu sana kwenye usimamiaji wa kiwango sahihi cha maji mwilini, utendaji wa cell na kikubwa zaidi  uanzishaji wa mwendo ( conduction of  electricity) katika  misuli ya mwili yenye mwendo hiari na mwendo usio wa hiari. Hivyo, hupelekea mwamko katika mishipa ya moyo inayohusika na huwa ndio chanzo cha mapigo yanahusika na msukumo wa  damu mwilini. ( generates heart bit) Mahitaji ya Potassium kwa mtu mzima ni kati ya milligram zisizopungua 3,500 ml. kwa siku kutoka kwenye lishe. Ili mwili wa binadamu uweze kuendelea na utendaji wake, potassium iliyoko katika mzunguko wa damu yahitaji kuwa kati ya 3.5-5.0mEg/L. Kiwango hiki kikipopunguwa hutupelekea hali ijulikanayo kama; Hypokalemia au Upungufu wa Potassium katika damu. Vile vile kiwango hiki kinapozidia huitwa H

MATATIZO YA THYROID KWA WANAWAKE .

Thyroid ni mojawapo ya tezi zilizo mwilini zinazozalisha  homoni  (hormones) zake ndani ya mwili  na kutumika  kwenye mfumo wa  damu. Miongoni mwa kazi za homoni ya thyroid ni    kusimamia  utendaji wa shughuli  mwilini kama mwendo wa mapigo ya moyo,( heart rate),  usagaji wa chakula (digestion) ,mwendo na utendaji wa metaboli (metabolism)  na kusimamia matumizi ya calorie mwilini. Ili tezi ya thyroid iweze kufanya kazi yake ya uzalishaji homoni  huitaji madini ya Iodine.Madini  hayo hupatikana katika vyakula vya mimea vilivyotoka  kwenye udongo wenye virutubisho vya iodine ya kutosha, chumvi yenye iodine na vyakula vya baharini. Tezi ya thyroid inapozalisha homoni pungufu na kipimo kinachohitajika  husababisha  hali ijulikanayo kama   “Hypothyrodism”. Tezi hii  ikizalisha  homoni kupita kipimo kinachohitajika mwilini huitwa “Hyperthyrodism” LEO NINAPENDA KUZUNGUMZA NANYI KUHUSU UGONJWA WA HYPOTHYRODISM Hypothyrodism ni ugojwa ambao huwapata  wanawake zaidi kuliko