NO LONGER A TABOO!.
Magojwa ya kiakili husumbuwa wengi katika jamii na hufumbiwa macho kutokana na stigma itokanayo na imani potofu na tamaduni zinazopotosha na hivyo kuwa kikwazo cha jamii kutafuta ushauri wa kitaalamu. Jambo hili limepelekea uhafifu wa huduma na ukosefu wa ushirikiano katika kuleta mwangaza.
Nia na madhumuni ya campaign ya Mental Health Awareness, ni kuleta mwangaza katika jamii kuhusu magojwa ya kiakili, kuelimisha na kupata ufumbuzi wa kitaalamu pamoja na huduma zitazoweza kupatikana hasa kwa jamii ya wahamiaji.
Campaign hii inayoongozwa na Montgomery County African Affairs Advisory Group, ikishirikiana na mashirika mbalimbali, wataalam wa magojwa ya akili na jamii ya wa-Afrika, imekusudia kuvunja ukimya katika magojwa ya kiakili na kumulika vijana ambao hali yao ni tete na bila msaada hujikuta katika mazingira magumu. Wengi huishia kutumia vileo, kuingia kwenye hanasa zenye kuhatarisha maisha yao na hata kutoa maisha yao pale wanapokosa fafanuzi au msaada.
Vile vile campaign hii itamulika wazee na jamii yote kwa ujumla, kwani hakuna asiyeguswa na changamoto za maisha zitokanazo na mazingira, zikifwatiwa na genetics na mambo mengine mbali mbali anayopitia mwanadamu.
Viongozi wa dini walitoa mwangaza waki-imani na kusii waumini wao kufuata taratibu
za-kitaalamu ambazo ni moja ya baraka na miujiza aliyoweka Mwenenyezi Mungu. Viongozi hao wa dini waliendelea kusema, sala ni jambo la muhimu, lakini hawatoshauri waumini kuacha dawa pale wanaposhiriki sala au maombi maalum ya mfungo.
WATAALAM WA MAGOJWA YA AKILI WAKIFAFANUA KWA UNDANI KUHUSU MAZINGIRA AMBAYO YAWEZA KUDHOOFISHA AFYA YA KIAKILI, PAMOJA NA MAUMBILE YA GENITICS YANAOPELEKEA BAADHI YA WATU KUWA KATIKA ATARI ZAIDI YA KUKUMBWA NA MAGOJWA HAYA.
MAELEZO YA UNDANI KUHUSU KUHUSU AFYA YA KIAKILI KWA VIJANA
Comments
Post a Comment