District 20 ni Wilaya inayojumuisha Silver Spring, White Oak na Takoma Park. Wilaya hii hujulikana kwa idadi kubwa ya wahamiaji hasa wale wa jamii ya ki-Afrika. Mchakato wa uchaguzi uliendelea kwa siku tatu mfululizo, ambapo wagombea walipata fursa ya kujieleza,kujibu maswali kutoka kwa jamii na kamati maalumu ambayo ndio yenye usemi wa mwisho na mamlaka katika mchakato huo.
Kamati hiyo hujulikana kama Montgomery County Democratic Central Committee (MCCDC) yenye wajumbe 28 akiwemo Mhe. Jheanelle Wilkins ambaye ndio mshindi wa mchakato huo.
Mhe. Jheanelle Wilkins ni mzaliwa wa Jamaica na muhamiaji aliye na malengo ya kupambana na sheria kali zinazopanga kutenganisha familia za wahamiaji katika utawala mpya ulioko chini ya rais mteuliwa ajulikanaye kama Donald Trump.
Baadhi ya waliogombea nafasi hiyo kutoka barani Africa ni pamoja na Daniel Koroma ambaye ni mzaliwa wa Sierra Leone na mtumishi wa umma katika kata ya Montgomery. Daniel Koroma ambaye alitolewa katika round ya pili amekuwa mfano kwa jamii ya waafrika na ishara kubwa kwa wenyeji kwamba jamii ya wa-Afika ipo hai na ina uwezo mkubwa na mwamko wa kushiriki katika meza inayotengeneza na kuamua sera zinazohusu mipango yote endelevu inayotumia kodi zinazochangwa na kila mmoja aishieye hapa nchini.
Kwa Picha Zaidi
Comments
Post a Comment