Katika sehemu hii ya pili, Harriet Shangarai wa NesiWangu Media anazungumza na mwanaharakati mwenye Albinism Babu Sikare kuhusu maisha yake na shirika lake la 'Afrobino' la kupambana na changamoto inazowaguwasa walemavu wa ngozi katika nchi zinazoendelea.
0 Ubongo wa binadamu unahitaji sukari kwa mda wote ili kuwa na nguvu ya kufanya kazi . Sukari hii yategemewa kutoka kwenye mzunguko wa damu kwani ubongo hauna uwezo wa kuzalisha au kuhifadhi sukari ya kutosha matumizi ya baadaye. Kutokana na hitilafu ya kingosho(dysfunctional pancreas) wagowja wa kisukari huwa na hali ngumu ya kuweka sukari katika vipimo vinavyohitajikana hivyo mara nyingi sukari huwa juu (Hyperglycemia) au chini (Hypoglycemia) na huhitaji tiba. Hivyo basi ni muhimu sana kwa ndugu au rafiki wa karibu kujua machache ili kuwa msaada pale mpendwa wako anapojikuta katika hali ya kuishiwa sukari kwani inahitaji huduma ya haraka kuokoa maisha. DALILI ZA UPUNGIFU WA SUKARI MWILINI (Hypoglycemia) Kipimo cha sukari chini ya 70 mg/dL au 3.9 mmol/L chaweza hatarisha maisha ya mpendwa wako mwenye kisukari. ; Njaa kuumwa kwa kichwa Kutokwa kwa jasho kutikisika kwa mwili...
NDIZI HUSIFIKA KWA UTAJIRI WAKE WA MADINI YA POTASSIUM Potassium ni moja kati ya madini muhimu ya chumvi chumvi mwilini.Ikisaidiana na chumvu chumvi nyingine kama Calcium, Magnesium na Sodium. Potassium ni muhimu sana kwenye usimamiaji wa kiwango sahihi cha maji mwilini, utendaji wa cell na kikubwa zaidi uanzishaji wa mwendo ( conduction of electricity) katika misuli ya mwili yenye mwendo hiari na mwendo usio wa hiari. Hivyo, hupelekea mwamko katika mishipa ya moyo inayohusika na huwa ndio chanzo cha mapigo yanahusika na msukumo wa damu mwilini. ( generates heart bit) Mahitaji ya Potassium kwa mtu mzima ni kati ya milligram zisizopungua 3,500 ml. kwa siku kutoka kwenye lishe. Ili mwili wa binadamu uweze kuendelea na utendaji wake, potassium iliyoko katika mzunguko wa damu yahitaji kuwa kati ya 3.5-5.0mEg/L. Kiwango hiki kikipopunguwa hutupelekea hali ijulikanayo kama; Hypokalemia au Upungufu wa Potassium katika damu. Vile vile kiwang...
Thyroid ni mojawapo ya tezi zilizo mwilini zinazozalisha homoni (hormones) zake ndani ya mwili na kutumika kwenye mfumo wa damu. Miongoni mwa kazi za homoni ya thyroid ni kusimamia utendaji wa shughuli mwilini kama mwendo wa mapigo ya moyo,( heart rate), usagaji wa chakula (digestion) ,mwendo na utendaji wa metaboli (metabolism) na kusimamia matumizi ya calorie mwilini. Ili tezi ya thyroid iweze kufanya kazi yake ya uzalishaji homoni huitaji madini ya Iodine.Madini hayo hupatikana katika vyakula vya mimea vilivyotoka kwenye udongo wenye virutubisho vya iodine ya kutosha, chumvi yenye iodine na vyakula vya baharini. Tezi ya thyroid inapozalisha homoni pungufu na kipimo kinachohitajika husababisha hali ijulikanayo kama “Hypothyrodism”. Tezi hii ikizalisha homoni kupita kipimo kinachohitajika mwilini huitwa “Hyperthyrodism” LEO NINAPENDA KUZUNGUMZA NANYI K...
Comments
Post a Comment