Mwanadiaspora Mtanzania na Mkurugenzi wa JENGA TANZANIA FOUNDATION Bw. Nasoro Ally akitambulisha rasmi Home Malaria Kit katika mkutano wa Africa Diaspora Market Place (ADMP III) uliofanyika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani tarehe 10/27/2014.
Akizungumza katika mkutano huo, Bw.. Nasoro Ally alieleza kuwa bado Malaria ni tishio kubwa la uhai kwa Sub-Sahara Africa na ni chanzo cha vifo vya watoto wadogo hasa chini ya umri wa miaka 5 .
Kipimo hicho chenye uwezo wa kugundua vijidudu vya Malaria mwilini kati ya dakika 5 hadi 10 kimekubalika na shirika la World Health Organization (WHO) kama kipimo sahihi na cha haraka kwa upimaji wa Malaria nyumbani. Bw. Nassoro aliongeza kusema, kipimo hicho kitatolewa bure nchini Tanzania kwa familia zisizojiweza na kuhakikisha kinafika sehemu mbali mbali za ndani hasa mikoani na vijijini ili kurahisisha upatikanaji wa huduma sahihi za afya na kufupisha safari ndefu na zenye milolongo.

Mkurugenzi wa JENGA TANZANIA foundation Bw. Nasoro Ally na Mwanasayansi msaidizi wa JENGA TANZANIA, Da. Asha Nyanganyi wakitambulisha rasmi kipimio cha nyumbani cha Malaria kwa Mhe. Balozi Liberatous Mumulala na wawakilishi wa USAID waliohudhuria mkutano huo.
VIDEO YENYE MAELEZO KUHUSU KIPIMO CHA NYUMBANI CHA MALARIA
Kipimo cha Nyumbani cha Malaria Chenye Uwezo wa Kugundua Vijidudu vya Malaria Vikiwemo Plasmodium Falciparim (PF) Vivax(PV) Ovale (Po) na Malariae(Pm) antigen kati ya dakika 5 hadi 10 .

Mhe.Balozi Leberata Mulamula akipata kipimo cha Malaria Mara moja kutoka kwa Mwanasayansi msaidizi wa JENGA Da,Asha Nyanganyi

Kipimo cha Nyumbani cha Malaria Chenye Uwezo wa Kugundua Vijidudu vya Malaria Vikiwemo Plasmodium Falciparim (PF) Vivax(PV) Ovale (Po) na Malariae(Pm) antigen
|
Mhe.Balozi Leberata Mulamula akipata kipimo cha Malaria Mara moja kutoka kwa Mwanasayansi msaidizi wa JENGA Da,Asha Nyanganyi

Baadhi ya watu wachache walioshiriki katika kipimo hicho.
Shukrani; Images
Sunday Shomari
Jenga Tanzania Foundation
Story;
NesiWangublogspot.com
Story;
NesiWangublogspot.com
Comments
Post a Comment