Maisha ya leo sio ya jembe na panga lakini jasho lake ni kali.Wengi tuna kazi nyingi na muda ni kidogo.Japo stress kidogo yaweza kuimarisha utendaji wetu,stress ikizidia au ya muda mrefu huwa ni hatari kwa usalama.
Msongo na mfadhaiko wa kiakili (Stress) tunaohisi, ni jibu au tokeo la mwili uliotahadhariwa kuwa hali inayoendelea imefika kiwango kinachozidi na kuelemea na hivyo mwili wapewa tahadhari kujiandaa kukabiliana na hali yeyote itakayojitokeza (defence mechanism). Hali hii hupelekea maumbile ya mwili kujiandaa kwa kuzalisha hormones ziitwazo; adrenaline, cortisol na norepinephrine ambazo kwa haraka hupandisha shinikizo la damu ( blood pressure), mapigo ya moyo, pumzi na kuongeza sukari mwilini ili misuli ipate nguvu ya kukabiliana na shambulizi linalohisiwa. Iwe ni kupigana,kukimbia au kupata butwaa (“fight , flight or freeze response.”) 

Tatizo ni pale stress inapokuwa ni ya muda mrefu na kusababisha homoni tulizozitaja hapo juu kuwa katika kiwango cha juu kwa mda mrefu mwilini. hali ambayo hufanya mwili usimamishe baadhi ya shughuli nyingine za kawaida kama usagaji wa chakula,kinga ya mwili, na kuelekeza nguvu katika pambano linalohisiwa kwa kuzidisha hormone za stress mwilini ambazo ni chanzo cha magojwa yafuatayo;
- high blood pressure
- magonjwa ya moyo
- Kisukari
- Kupunguza umahiri wa kinga ya mwili(immune system)
- Kupunguza uchujaji wa maji mwilini kama ADH hormone
- Msongo wa mawazo( depression)
- Eczema au vipele vya kuwasha vay ngozi
- Matatizo ya kulala au usingizi
- Maumivu kwa ujumla
- Kuongezeka kwa uzito wa mwili au unene
NI VIPI KUKABILIANA NA STRESS ?
- Weka ratiba ya mazoezi ya mwili ya mara kwa mara(Kwani mazoezi husaidia uzalishaji wa hormone za kujihisi vizuri na hata kuondoa maumivu kama (Endorphins,Dopamine,serotonin)
- Chukua mda utoke kwenye desk na kutembea
- Chagua fikira safi na zenye kukupa nguvu ( think positive)
- Weka mziki mwororo kama office yaruhusu
- Jifunze kutokuza mambo wala kuchukulia vitu kibinafsi (personal)
- Tumia chai au kahawa
- Kuwa na marafiki au watu mtakaotegemeana na kusaidiana na kushauriana
- Epuka mazingira ya kukuleta stress
- Pata usingizi wa kutosha
- Weka ratiba na kuifata ili kuepuka kazi za kukurupuka ( do not procrastinate)
NINI DALILI ZA STRESS
- Hasira za haraka
- Wasiwasi
- Kutoweza kuwa makini( poor concentration)
- Ugumu wa kutulia ( inability to relax)
- Huzuni
- Kulia bila sababu au kwa urahisi
Nukuu
Centers for Disease Control and Prevention CDCPicha:
www.blackhairinformation.com
www.huffingtonpost.com
Thinkstock / Maridav
OWN
Comments
Post a Comment