Maisha ya leo sio ya jembe na panga lakini jasho lake ni kali.Wengi tuna kazi nyingi na muda ni kidogo.Japo stress kidogo yaweza kuimarisha utendaji wetu,stress ikizidia au ya muda mrefu huwa ni hatari kwa usalama. Msongo na mfadhaiko wa kiakili (Stress) tunaohisi, ni jibu au tokeo la mwili uliotahadhariwa kuwa hali inayoendelea imefika kiwango kinachozidi na kuelemea na hivyo mwili wapewa tahadhari kujiandaa kukabiliana na hali yeyote itakayojitokeza (defence mechanism). Hali hii hupelekea maumbile ya mwili kujiandaa kwa kuzalisha hormones ziitwazo; adrenaline , cortisol na norepinephrine ambazo kwa haraka hupandisha shinikizo la damu ( blood pressure), mapigo ya moyo, pumzi na kuongeza sukari mwilini ili misuli ipate nguvu ya...
Community Health Innitiaves