Skip to main content

PATA PRESCRIPTION MEDICATION KWA BEI NAFUU!


Bofya:
Jina kamili la dawa 
Zip code
Chagua Milgram na Idadi ya  dawa kifuatia agizo la daktari 
Print coupon
Wasilisha katika pharmacy ya anwani  husika

FUATA HATUA SAHIHI ZA  UTUMIAJI  WA DAWA
  • DAWA SAHIHI;
 Dawa huweza kuwa na majina yanayokaribiana hivyo kuwa mwangalifu na kusoma kila mara

  • DOZI SAHIHI;
Vifo vingi husababishwa na utumiaji wa dawa kwa kiwango kisicho sahihi.

  • NJIA SAHIHI
Ili kuepuka madhara, hakikisha unafuata njia sahihi katika matumizi ya dawa mfano dawa ya kumeza, kupaka au kuchoma sindano itumike ilivyokuwudiwa.

ZINGATIA VIPENGELE VIFWATAVYO;
  • Dawa ya kumeza isiyoruhusiwa kutafunwa au kuvunjwa, 
  • Dawa inayotakiwa kutafunwa
  • Dawa inayohitaji kutumiwa na chakula
  • Dawa inayohitaji kutumiwa na kiwango kikubwa cha maji
  • Dawa inayohitaji kutumiwa kwa muda maalum kabla au baada ya chakula 
  • Dawa, vyakula au viywaji vya kuepuka wakati wa matumizi ya dawa husika
  • Kabla ya matumizi ya dawa yeyote mfahamishe daktari wako dawa ambazo unatumia
  • Mfahamishe daktari na nesi kuhusu tatizo lolote la  allergy
  • Ripoti dalili zozote baadaya matumizi ya dawa mpya ikiwemo;kuwashwa, vipele,kuvimbe etc.
  • Soma na uliza maswali kuhusu dawa uliyoandikiwa kabla ya kutumia



  • MUDA SAHIHI
Ili dawa ifanye kazi inavyotakiwa ni vyema kutumika kwa muda uliopangwa, mfano dawa za maumivu endapo umepangiwa kila baada ya masaa manne hadi sita, ukapitiliza maumivu hurudi na huwa magumu zaidi kuyatuliza.

                                                                   


  • KUMBUKUMBU
Baadhi ya makosa katika matumizi ya dawa ni usahaulifu. Mara nyingi usahaulifu utokea pale mtu anapotumia dawa, kisha anasahau kuwa ameshatumia na hivyo  kurudia matumizi na kuzidisha dozi aliyopangiwa. Tatizo lingine  ni kwa WAZAZI  KUTOWASILIANA ; mzazi anaweza  kutoa dawa kwa mtoto na kusahau kumtaarifu mzazi mwenzake. Bila kuwa na mfumo wa kufahamishana, mzazi mwingine anarudia utoaji wa dawa na kuhatarisha uhai.  Hivyo yashauriwa kutumia nyezo za kusaidia usahihi wa matumizi ya dawa kama pills kit, calendar, diary etc.





































Images;
www.halifaxexaminer.ca
askabiologist.asu.edu

http://www.ruanemedical.com/
http://www.ebay.co.uk/

Comments